Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Tunakosa sana nafasi za wazi kiasi kwamba unaanza kuhisi tuna nafasi ndogo ya kusonga tukikutana na Elite teams kwenye hatua ya mtoano... Kwasababu haziwezi kukupa nafasi nyingi hivyo. Nafasi chache utakazopata inabidi uzitumie.
 
Kuna vitu Jesus anakupa Kai Havertz hawezi kukupa kamwe.. Kuna vitu Kai Havertz anakupa Jesus hawezi kukupa kwa sasa na amepoteza uwezo huo hasa anapokuwa 1vs1 na kipa. Hatuwezi kwenda mbele na aina hii ya wachezaji ambao wanabeba roho ya timu pale mbele. Arsenal wanamuhitaji namba tisa Kariba ya Alexander Isak.
 
Yani sisi kwenye transition ni sifuri sifuri kabisa na ndio sababu tupo kwenye nafasi tuliyopo, mtu anakwambia leao hana maana tena sababu kasajiliwa Harvertz, kwa nafasi hizo za trossard, ode na Martinelli?
 
Leao dhidi ya Napoli kwenye UCL semis nadhani ilikuwa mwaka juzi, afu imagine na namna monaco wanavyocheza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…