Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Mara nyingi sana nimejaribu kumuelewa Jorginho lakini huwa nashindwa.. Kila mara anapoanza katikati huwa tunakosa balance na flow nzuri ya mchezo... Kuna vitu vingine Arteta huwa analazimisha tu lakini havina tija kwenye mchezo.. Ni kwanini Kieran Tierney asianze left back then Thomas Partey akaenda katikati.. Una left back wa asili unamuacha nje then unachezesha wachezaji out of position.
 
Katika kitu nimegundua Arsenal tukicheza na timu ambayo tayari iko kwenye mkao wa kushambuliwa tunastruggle.

Ila tukicheza na timu ambayo inafocus kudefend tunakua wazuri. Timu ambayo ipo tayari kushambuliwa inakua ina wachezaji hadi mbele so they can also score.

Ila viazi vinavyotaka kukaba kama nyumbu ni easy kuvipiga bila majibu
 
Hata mimi najiuliza kulikoni kuhusu Tierney
 
Ndani ya box la Fulham tumeingia mara 22 wao mara 2.

Hawa wapuuzi hawajui kama kuna kushoot?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…