Arsenal (The Gunners) | Special Thread

2011 upo form one halafu unaandika matusi kila siku humu.

Anyway, kama tukifuata mfumo wa la kwanza mtu anaanza na miaka 7 mimi ni mkubwa kwako. Arsenal ya Wenger nimeiona.

Kaka yangu ni nyumbu, baba yangu ni Liva. Baba yangu ni Simba kaka yangu ni Yanga. Mimi bongo sina timu.

Mimi naanza kushabikia mpira mechi moja moja inaonyeshwa DTV. Matokeo mengine tunafuatilia magazeti kulikua na gazeti linaitwa Spoti Starehe na jingine Alasiri.
 
Humu ni kigenge mashabiki wote tunakutana humu kwa ma false hopers hatupendi kuwaona mnaishi na false hope hamjui hata ladha ya epl ikoje vile captain anavyonyanyua makwapa kwa furaha huku ameshika epl 🏆. Nyinyi kombe kwenu ni zito sana thats why miaka 20 mmeshindwa kunyanyua.

Hilo la kwamba winger akifunga goli anafananishwa na saka au martineli hii ni false hope nyingine.
Martineli huyu huyu ambaye hata goli 10 hajafika ana goal 6 😀 kamzidi goal 1 barnes mchezaji ambaye ni injury msimu mzima
 

Attachments

  • Screenshot_20240522-221113~2.png
    330.6 KB · Views: 9
Wewe ni ushahidi namba 1 umeleta sana vituko vyako humu ukivifananisha na Arsenal au wachezaji wa Arsenal.

Sasa Lete reference za winger yeyote duniani akifananishwa na winger wa Newcastle
 
Chelsea kuchukua ubingwa aitaji kuwa dominant anatoka from no where anachukua na next season anavuruga kocha atatimuliwa ataletwa mwingine maana chelsea sio team ya project,huo umekuwa utamaduni wa chelsea kwa miaka 10+ kinachowabeba ni mentality ya team haswa wakiona kuna uwezekano wa kuchukua .Nikuambie chelsea haiwezi kukubali iache ubingwa mechi kumi za mwisho patachimbika .
 
Ndio msana sipendi kubishana, sababu mnaweza ishia kutukanana, unaweza mtukana mwanso au baba yako.

2011 form 1, sawa bwana mdogo una haki ya kuishabikia city.. Je ndio mwaka ulianza kupenda mpira, au miaka ya nyuma ulikuwa hufuatilii?
 
Ndio msana sipendi kubishana, sababu mnaweza ishia kutukanana, unaweza mtukana mwanso au baba yako.

2011 form 1, sawa bwana mdogo una haki ya kuishabikia city.. Je ndio mwaka ulianza kupenda mpira, au miaka ya nyuma ulikuwa hufuatilii?
Niko primary muda wakufuatilia mpira na toa wapi ,hio miaka access ya madogo kuangalia mpira haikuwa rahisi kama saizi..........movie John Rambo ,jet lee ,jack chan ,vanndame ...ndio ilikuwa habari ya mjini Enzi hizo kwangu...
 
Niko primary muda wakufuatilia mpira na toa wapi ,hio miaka access ya madogo kuangalia mpira haikuwa rahisi kama saizi..........movie John Rambo ,jet lee ,jack chan ,vanndame ...ndio ilikuwa habari ya mjini Enzi hizo kwangu...
Dogo acha kujivua nguo?
Form one 2011 maana yake darasa la 4 ni 2007.

2007 hakuna access ya TV?

Naangalia kombe la dunia 1998 karibia mtaa mzima watu walikua na TV mitaa niliyokua naishi.
Ukiachana na DSTV, baadhi ya game za ulaya zilikua zinarushwa chanel10/DTV/ITV
 
Niko primary muda wakufuatilia mpira na toa wapi ,hio miaka access ya madogo kuangalia mpira haikuwa rahisi kama saizi..........movie John Rambo ,jet lee ,jack chan ,vanndame ...ndio ilikuwa habari ya mjini Enzi hizo kwangu...

Ushabiki wa timu una vyanzo vingi. Mimi Arsenal nilianza kuikubali 1995 (darasa la 5 😄) kwa sababu ya Denis Bergkamp. Nadhani hapo amekuja kutoka Inter Milan, hata Wenger bado hajaingia Arsenal. Nikasema kama huyu bro ameenda huku, mimi naenda nae. Enzi hizo tunapenda timu kwa sababu ya wachezaji. Mpaka leo nazipenda Barcelona, Real Madrid, Inter Milan kwa sababu timu aliyokuwa Ronaldo da Lima ndiyo timu yangu enzi hizo 😄😄😄

Kwenye movies za 'mkono' acha nikurekebishe kidoooogo. Ni Jet Li na Jackie Chan. Van Damme enzi hizo tumamwita Dameeee.
 
Yess Kwa miaka hio 2007 Kwa mim niliishi tofauti kidogo ...

Nyumbani Hakuna tv ya kuangalia mpira ,labda movie ya kutumia mikanda .......
Nachungwa nyumbani ,napewa Kazi za kuosha vyomba ,kufagia uwanja,kutumwa sokoni ..

Ukirudi nyumbani saa mbili Ni fimbo, ,...

Mipira ya ulaya ilikuwa inaoneshwa usiku ,Mara nyingi ,......Rudi nyumbani saa moja uone kichapo utakachokutana nacho ..

Access ya mpira ilikuwa inawafavour wakubwa kuangalia kuliko Sisi madogo ... Kwa wakati huo ,ndio maana mim mpaka nilipofikisha umri WA kuwa huru home ndio nilianzia kuangalia mpira sasa .....

Umeme wenyewe ulikuwa WA generator,hata wanapoonesha mpira ,kujua tu ratiba Kwa dogo kama mim ilikuwa ngumu ...

Dogo kama mim kukomaa kwenye Banda eti naangalia mpira Tena jenereta imewashwa saa tatu usiku ,kudadeki utasikia mle kibanda umiza " hivi Huyo dogo Ni WA Mzee Nani ,Kwan hajui kama kesho Ni Shule anakaa humu mpaka sasa NNE usiku😂" baba yako akisikia ulikuwa unakula kichapo ,kiufupi ilikuwa kama haramu kajichanganya na wakubwa et unaangalia mpira ....

Wewe kama ulikuwa unaangalia mpira ukiwa na miaka 8 au 9 ya ulaya ,iliyokuwa inacheza usiku ,basii Ni malezi yenu ....
 
kwani siti ikichafuliwa unapungukiwa nini? Unaimiliki? unahisa? au ni utumwa tu fikra man?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…