Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Kitendo cha wana arsenal kushika nafasi ya pili msimu huu nyuma ya city haiwapi guarantee kwamba msimu ujao pia mtabaki kuwakimbiza hao jamaa kwa karibu kama hivi sasa. Niweke rekodi sawa hapa kuwa Man united ya Ole imewahi kuwa ya pili lakini msimu uliofuata ikapoteana, liverpool wamewahi kuwafukuzia city mara mbili mfululizo ingawa leo wamepoteana kama sisi tu.
Ninachotaka kusema ni kwamba kipara peke yake pale epl ndiye mwenye dhamana ya kukaa ndani ya top 2 msimu hadi msimu.

Mwakani chelsea na united zitaleta upinzani kwenu tofauti na matarajio yenu.
Punguzeni matarajio ili mzeeke bila magonjwa yasiyoambukiza
 
Wanakuja humu wanajichekesha na kutishia watachofanya msimu ujao leo usiku kocha wao kasema anaondoka
 
Ole 🤣🤣🤣 irrelevant coach
 
Arsenal ni kichekesho ndiyo maana unaona watu wanaizungumzia sana si unajua kicheko nacho chaongeza siku za kuishi.

Kama unahisi watu hawazungumzii 4 in row ya man city basi inaonekana hujichanganyi na fans mbalimbali unakaa na false hopers wenzako tu .

Suala si kwenda Uefa cha muhimu ni unaenda kufanya nini? Group letu tunawakilishwa na Dortmund mwanetu .
Nasikia mlikua mnafanya rehearsal ya kuchukua kombe kabla ya match ya everton sasa unaona hio ni team au kikundi cha comedy.

Haina haja ya kufunga na kuomba arsenal asichukue kombe wakati unajua kabisa hachukui.
 
Umetaka tofauti nimekupa.

Streamers walikua wengi kuangalia speech ya Klopp akiaga kuliko channel ya city kuongelea 4 in a row. Hili kombe itakua unaliongelea wewe tu.

Humu JF hakuna uzi wa mpira unaovutia kuingia zaidi ya huu. Nyumbu, kenge, liva, city watafungwa na wote mnaassume ni kawaida.

Akifungwa Arsenal wote mnaacha kazi zenu mnakimbilia huku. Winger yeyote akifunga magoli mawili mfululizo atafananishwa na Saka au Martinelli.

That's the difference. Hii timu ni SI unit ya ubora. We mwenyewe ulikua umejificha ligi imeisha haujaenda jukwaa la waliochukua kombe badala yake unakesha humu.

That's the difference
 
Cap🧢
 
Ndugu mnataka mataji ambayo hamjayafanyia kazi ?Haland na foden wafunge magoli ubingwa wapewe wengine ,kila team ipambane hakuna dezo ,kulia lia kama vitoto ni ujinga
 
Kwa sasa city kuchukua ubingwa ni kawaida kipara akiendelea kuwa england hakika kwa miaka kumi ana wa bless wengine mara mbili hapo ni chelsea au liverpool wanaojua ubingwa unachukuliwa namna gani.
 
Kwa sasa city kuchukua ubingwa ni kawaida kipara akiendelea kuwa england hakika kwa miaka kumi ana wa bless wengine mara mbili hapo ni chelsea au liverpool wanaojua ubingwa unachukuliwa namna gani.
Liver kabla ya hapo juzi walikaa miaka 30. Amekuja kocha mpya, sidhani kama wataanza kua on fire right away kwa mbinu za kocha.

Chelsea kocha kaondoka. Means anakuja mpya akiwa na kundi la wachezaji wengi watengeneza nafasi kuliko wafungaji.

Siamini kama Chelsea anakua dominant next season
 
Na msimu ujao tena mtakuwa na Best season, End with ZERO Trophies Again. Maisha yenu yatabaki kuwa hayahaya.
 
Yani wakiitwa mawinga bora epl Martinelli ambaye ni bench warmer wenu nae ataenda??
 
Na msimu ujao tena mtakuwa na Best season, End with ZERO Trophies Again. Maisha yenu yatabaki kuwa hayahaya.
Na tutabaki kuwa na furaha. Tukiendelea hivi sisi tunajua tutakuja kutoboa tu. Nyie mnaangalia mikono mitupu yetu, sisi tunafurahia safari yetu. Hamwezi kutuelewa kwa nini tuna furaha na hicho kitu kinawauma. Hiki kichaka cha makombe mnachojifia, muda si mrefu tutakifyeka. Ila kama kawaida ya wachawi, mtatafuta kingine.
 
Hii ya leo itakua ni ya Unga LTD.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…