Hivi kuna mijitu hapa kumbe furaha yao katika mpira ni kuona Arsenal inakosa vikombe eti ehee??
Yaani kuteleza kwa arsenal kwao wanaona ndio mafaniko na jambo la kuwapa furaha kuliko hata mafanikio ya timu yao?
Maaana kuna maposts marefu marefu hapa yamejaa ushuzi mtupu pamoja na chuki, mpaka najiuliza hivi huyu mtu yuko sawa kweli kichwani?
Kweli gunners tumeimprove pakubwa sana, hizi chuki nilikuwa sizione kabisa miaka ya nyuma wakati tunashika za 8,6 na 5 huko.
Watu mnaichukia Arsenal kuliko hata mnavyozipenda timu zenu, dalili za ukichaa hizo