Arsenal (The Gunners) | Special Thread

mkuu uko sahihi, na hilo bango watu wanatakiwa wakumbushwe maana kuna muda wanajisahau wanaanzakuwa na matumaini hewa.
January unatakiwa umuache point 15 kama alivyofanya Liverpool alivyochukua ubingwa round ya kwanza kashida mechi zote kasare moja tu na man united.
 
Umezingatia na factors Nyengine kama Declining phase ya Wachezaji after age 25, Injuries, Transfers?
Kwa kiasi fulani, ndiyo. Ukiangalia hayo mambo amefanya huku akipambana na mambo ya kukosa wachezaji muhimu kwake, huku akijitahidi kupunguza wasio na manufaa (Ozil, Aubameyang, Tierney, Bellerin, Maitland-Niles...).

Yaani, kama makocha wote tu kwenye ligi, anafanya hayo huku akijitahidi kujenga timu inayomfaa kila msimu.
Mfano, unaona kawaleta Rice na Kai baada ya Xhaka kuondoka. Anajua ana mmoja wa makipa bora kabisa kwenye ligi, Ramsdale, lakini bado akamleta Raya, na Raya kadaka Golden Glove. Hii inaonesha kuwa dogo anataka kuimarisha kila sekta awezayo kadri awezavyo.

Kazi ipo kwenye kuleta wachezaji bora na bora zaidi kila msimu. Akifanya vizuri na kuendelea kuingia michuano ya Ulaya, atazidi kuvutia wachezaji wazuri.

Then linakuja suala la mbinu uwanjani. Ni wazi kwamba kwa mchezaji mmoja mmoja, Arteta hana akina Watkins, Doku, KdB, Olise, nk,. baadhi ambao wangeanza mbele ya wachezaji wake alionao , ila ukiangalia jinsi alivyowatumia alio nao, unaona ni kocha aliye vizuri kidogo kimbinu. Na factor ya mbinu ni muhimu maana ndiyo moja ya vitu vinavyotenganisha mafuta na maji kwenye hili game.
 
Tunaanza phase 4 muda si mrefu. Yaani kwa wachezaji itakuwa ni mwendo wa 'toa chuma, weka chuma'. Hao akina Nelson, Tierney, Nketiah...hawatakuwepo. Utakutana na akina Sesko, Xavi Simmons....

Kama mkorea anavyosema 'maji mtaita mma'
Mkuu, Usianze kutoa Siri za kambi mapema
 
Binafsi nafikiri tunaongea lugha moja.

Kati ya vitu ambavyo arteta na technical bench walivijua mapema ni ukweli kwamba wasingeweza kuleta top top class players wakati walipoanza kuijenga timu

kwa arsenal ilivyokuwa ilikuwa ni kazi mno kumpata mchezaji kama declan rice hata kama tungekuwa na hela.

Walianza kwa kubadilisha image ya team kwanza ili kuvutia top talents,kwa ambaye haelewi hili ajaribu kuiangalia man u na chelsea kwasasa zinavyohangaika kupata wachezaji wazuri.

Ili upate world class player unahitaji proper image ya team na pesa ya maana.ndo maana mardrid hateseki sana akimtaka mtu,Mbape ameachwa ajipambanie mwenyewe tena na kwa mshahara waliompangia na sio anaoutaka.

Swali ni kwanini humsikii mbape analilia man u,chelsea,arsenal,man city,bayern au liverpool wakati hela huko zipo tu.ishu ni image.hapa ndo nakaa na kumuelewa mno EDU kwanini alisimama na arteta wakati dunia ikimkataa.alitaka mtu wa ku reclaim image ya club ili kuvutia top talents

Niliandika mwanzo wa msimu kwamba arteta kuna watu anawatumia kama first starter ila ukifika muda akapata quality anayoitaka watashangaa na leo narudia tena kuandika

Zinchenko,gabriel maghales,jesus,odegard hawa wanatumika kuipa hadhi team ili tufikie level ya kusajili bila shida toptop quality players.

Usinitajie kina nketiah,nelson,lokonga,tavares,elneny,kiwior,jorginho nk.hawa wanatumika kujaza kikosi na akija mtu mwenye hela wala arteta hatawaza mara mbili.

Pep akae hata miaka miwili mbele na arteta aweze kupata technical quality anayoitaka,nawaambia mtashangaa sana.

Kwangu mimi naweza sema baada ya wenger hakuna kocha nayeheshimu mbinu zake kama PEP,Ila haka kajamaa ketu ka arteta kakipata quality kanayoiota hawa kina "I'm running out of energy" ndani ya epl tutawasikia wengi
 
Kila msimu mnasema hivyo hivyo, unataka uniambie tangu 2005 nyie mnajenga tu timu?.

Mbona Leicester city kaja kachukua kombe nyie mpo tu, Liverpool kafufuka kachukua makombe nyie mpo tu, hivi ujenzi gani wa timu wa miaka 50?.
 
Kila msimu mnasema hivyo hivyo, unataka uniambie tangu 2005 nyie mnajenga tu timu?.

Mbona Leicester city kaja kachukua kombe nyie mpo tu, Liverpool kafufuka kachukua makombe nyie mpo tu, hivi ujenzi gani wa timu wa miaka 50?.
Chelsea ilichukua miaka 50
 
Kila msimu mnasema hivyo hivyo, unataka uniambie tangu 2005 nyie mnajenga tu timu?.

Mbona Leicester city kaja kachukua kombe nyie mpo tu, Liverpool kafufuka kachukua makombe nyie mpo tu, hivi ujenzi gani wa timu wa miaka 50?.
Labda wanajenga mnara wa England premier league.
 
Reactions: K11
Ila Arsenal vita mmevipiga vizuri
That mentallity monster naiona ndani ya Arsenal. Game ya united imeonesha jinsi gani Arsenal wame komaa, 1 step closer Arsenal watashinda EPL.
 
Ifike hatua tukubaliane Epl walau kuanzia mechi 3 za mwisho kuelekea msimu kuisha ziwe zinachezwa kwa muda sawa.

Hii itasaidia kuongeza ushindani katika ligi na kuepusha uelekea wa maamuzi ya matokea ya baadhi ya mechi.

Waiweke katika kanuni zao kabisa bila kujali hali msimamo wa ligi.

Nawaza pengine hizi game 3 za mwisho zingekuwa zinafanyika kwa namna hiyo, mbali na kuleta msisimko lakini zingweza kuwa na matokeo tofauti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…