Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arteta says Havertz form has forced a change of plan at Arsenal

@sr_collings
Hyu mhuni hatakaa atoke tena first eleven...Partey atakuwa anatumika kwny special mission...ili tum manage na majeraha yake....ila natamani sana Zinchenko awe anakula benchi mechi ngumu maana yule ndo weak link yetu...ule upande kule ni wa Super Hiroshima Tomiyasu au Polish monster Kiwior
 
Player of the Match, Arsenal's @kaihavertz29


1 goal,

1 assist

8 touches in Brighton's penalty area

13 sprints,

4 chances created

9 goals & 5 assists in @premierleague this season - highest totals in his PL career
 
Arteta ana mifumo hatari sana asilimia kubwa ya makocha na wachambuzi wameshaanza kumuogopa.
Kocha wa Luton anasema ,ukitaka kucheza physical,Arsenal wanakupa hiyo game ,ukitaka Total football wanakupa hiyo game,ukitaka Haram football ndio mafundi wenyewe ,

Angalia hapa picha ya kwanza , Wachezaji 9 wa Arsenal wapo kwenye zone ya Brighton ,hii Total football


Halafu angalia picha ya Pili

Wachezaji 9 wa Arsenal wapo kwenye zone Yao wameweka low block vs mancity
 
Zile dakika tano za mwsho kipindi cha kwanza...kuna mbinyo ulipigwa pale mpk nikawaonea huruma Brighton 🤠🤠...yaani kila wakitaka kutoka wanakwama...walikula ngeta moja metata sana mpk De Zerbi akawa anashangaashangaa haelewi kinachoendelea
 
Brighton wamekua na matokeo mabovu hivi karibuni mpaka siku hizi hausikii De Zerbi akifananishwa na Arteta wala hawaendi kusikiliza falsafa zake za mpira.

Ila walikuja na kuamua kutaka kufufukia kwetu. Yule Enciso kwangu alikua wa moto ila De Zerbi akamtoa, Jesus big chances 3 zote kamiss, mwanetu Kai ana shortcomings ila assist na goli vimeziba shortcomings zingine.

Our lethality in front of a goal is seriousl questionable at this point. Zingatia tupo kwenye title run, mwisho tutakuta wachezaji wetu wanaitwa Maagent kama Erik kichwa ngumu anavyosemwa ni jasusi toka Ajax
 
Yan Clean sht inashangiliwa hadi na Trossard nimeshangaa sana leo
View attachment 2955975
Usiwapangie watu furaha Yao mkuu.......let them celebrate...that is what they train and play for!......kwanini wasipongezane kwa kazi nzuri ya kumlinda kipa wao aondeke na clean sheet?........yaan hapo wametimiza jukumu lao kama forward anapofunga TU....wewe unaumia Nini sasa........umeangalia game ya city....umeona Ortega alivyouchukua ule mpira kwa nyuma akiwa under pressure?.......washabiki wakati mwingine tunapenda kuona moment kama hizo....let people enjoy the game.... don't kill joy!
 
Umeongea maneno mengi yasiyo na maana kwangu
 
Mikel anasema Kai amebadili mfumo wa Arsenal,kwasasa hakuna wakumtoa pale CF, Jesus imebidi arudi pembeni akapambanie namba kwa Martinelli na Saka ,

Kai as CF anachofanya ni ngumu kuona usipokuwa makini


Ni mcheza rafu za kimya kimya kwa mabeki, urefu wake unawasumbua sana mipira ya juu ,mabeki hawapend hicho kitu


Silaha yake kubwa ni movement,

Nilimtabiria Goli 15 all competition


Hadi sasa nadhani ana goli 13 kama sikosei

Assist 5


G/A 18 hivi Hadi sasa

Arteta anasema Bado hajampata Kai anayemtaka

Reminder that,Kai ana miaka 24 tu Bado hajafikia peak yake ,


Kitu kingine Kai , Availability yake ni kubwa ,huwezi kusikia eti ana injury,
 
Unajua nini bro...

Ushasikia mtu anaitwa "kibonge mwepesi"? Yaani mtu ana mwili lakini matendo yake katika mambo flani hayaendani na mwili wake na kukushangaza?

Kai naye anakitu kama ukibonge wepesi kwa jinsi alivyo alivyo tu. Kwa wembamba wake anaonekana kama hana nguvu lakini anazo vizuri tu na anaenda bega kwa bega na kina VVD.
Anavyokimbia ni kama hana mbio lakini anazo. Anaopopokea mipira anaonekana kama hana ball control nzuri ila ball control yake si haba (tena sometimes anakuwa under pressure ya mabeki).

Anakasura ka upole na ka kizembe zembe ila uwanjani jamaa ni mhuni mhuni na katili, kama Saliba na Gabriel. Nilishangaa kuona jamaa ana kadi 8 za njano. Marefa wakimuadhibu kwa faulo au kumpa kadi unaona kama wanamuonea.

Maybe, kama ilivyokuwa kwa Ozil, jinsi jamaa alivyo alivyo tu unawafanya watu wa mjudge tofauti na uhalisia. Ndiyo maana mimi najitahidi kuangalia uchezaji wake zaidi ya jinsi alivyo alivyo, na kuna mambo jamaa huwa anafanya yanaudhi mashabiki balaa 😄.

Nilishakiri kuwa miongoni mwa wasiomkubali Kai na huwa natafuta na kuona machache mabaya anayofanya kwenye game kati ya mengi mazuri anayofanya 😄😄
 
Arsenal waliniudhi sana kwa kutofunga bao katika ule mbinyo aisee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…