Arsenal (The Gunners) | Special Thread

No, kiwango chake kilishuka baada ya injury, alivyorudi akawa siyo yule tena.

Akawa anapigwa benchi.

Siku hizi anaanzia benchi. Hata game ya juzi
Sema jamaa ni bonge la mchezaji,ile kasi yake sio ya mchezo inabid akabiliane na mchezaji aina ya Saka kwel, maana saka akili mingi zaid
 
Tutaacha nafasi ya mashabiki 20 tu,

Chelsea wa5

Man united 10

Liverpool 5..
 
Huyu jamaa Bado Arsenal inamsumbua akili kama mashabiki wake ,

Mechi ya Liverpool lakini anaizungumzia Arsenal,

Sijawahi ona kocha wa hivi

Kila mechi akishinda anadai atafunga yeyote , atadai alitakiwa aifunge Arsenal
 
Davies kapoteza nafasi katika first IX kutokana na majeruhi na kushuka kiwango. Game nane za mwisho za Bayern, kaanza moja vs Mainz, na kacheza dk 18 tuuu.
Humu mpira wengi hawajui ,hata backline Yao kwasasa ni De Ligt na Dier,maana Upemaguire na Kim wanachoma sana
 
Hyu kwni sisi tumemkosea nn jmni...maana kama point tumempita za kutosha lakini bdo anatufatafata tu...yaani Arsenal haikauki mdomoni mwake...kiwango chetu na chao ni mbingu na ardhi...akae akijua hilo
Huyu jamaa Bado Arsenal inamsumbua akili kama mashabiki wake ,

Mechi ya Liverpool lakini anaizungumzia Arsenal,

Sijawahi ona kocha wa hivi

Kila mechi akishinda anadai atafunga yeyote , atadai alitakiwa aifunge Arsenal View attachment 2937943
 
Kwa hiyo mnataka hamis77 aje na ID mpya tena next season?

Acheni roho mbaya. Sisi tunapambania UCL. Bayern mwaka huu ndiyo nina imani tunaweza kumbonda kuliko misimu yote tuliyokutana nao. Na hapo tayari tumeshawahi kumfunga Bayern, ni kwamba tu wana historia ya kutupiga nyingi nyingi 😂😂.

Livakuku walikosea sana kuwaachia nyie muwapige huku semi final kunakukutana na Coventry City. Yaani fainali nje nje wazi kama ya mbuzi.
 
Huyu jamaa Bado Arsenal inamsumbua akili kama mashabiki wake ,

Mechi ya Liverpool lakini anaizungumzia Arsenal,

Sijawahi ona kocha wa hivi

Kila mechi akishinda anadai atafunga yeyote , atadai alitakiwa aifunge Arsenal View attachment 2937943
Hajasema uongo lakini, goli tulilowafunga lilikatiliwa kidhuluma sana kwa kisingizio cha offside wakati haikua offside, pili tulinyimwa penalty ya wazi kabisa baada Gabriel Magalasa kucheza netball badala ya football kwa kumshika na mikono na kumuangusha Højlund ndani ya box wakati akielekea kufunga.
Refa pamoja na wahuni wenzake wa VAR alitumia juhudi kubwa sana kututoa mchezoni na kweli walifanikiwa baada ya wachezaji wetu kupanic kwa dhulma za waziwazi zilizokua zinaendelea pale Emirates, bila ya ule uhuni mliotufanyia kwa kushirikiana na marefa ile mechi mlistahili kufa kwa goli zisizopungua 5.
Hii dhuluma yenu ya kuwahonga marefa pamoja na wale wahuni wa VAR lazima mtailipa kwa uchungu mkubwa sana pale kwenye dimba la Old Trafford.
 
Masingeli ana roho nyepesi sana kama bua timu yake ikifungwa, Msimu ulioisha baada ya kugongwa dakika za mwisho na kutema bungo, alikuja kutuaga humu jukwaani kwa kisingizio cha kuibiwa simu, akadai hatakua na access tena ya kuingia JF, wahuni wakamuhoji hio access ya kuingia Jf na kuaga ameipata wapi wakati simu yake imeibiwa?
Akatudanganya kua eti ameazima simu ya mama ake mdogo

Kuna msela alijitolea kumnunulia Iphone ili tu Masingeli asikimbie Jukwaa, lakini Masingeli alichomoa huku akimtuhumu huyo mtu hana nia njema na yeye

HENRY14 wewe ni miongoni mwa mashabiki wachache wa Arsenyau wenye roho ya paka, ambao hata timu ikufungwa bado utaoneka kwenye majukwaa yote humu ya Sports ukijibu hoja tena kwa kujiamini kabisa, ila Masingeli na hawa chawa wake ndio maana kuna watu hua wanawatuhumu humu kua ni mamluki, wanaonekana timu ikifanya vizuri tu na kujimilikisha hili jukwaa huku wakiwachamba wazalendo wakweli wa hii timu kina computerarsenal , Will Jr ,dadamlamayao , verifaidi yuza Castr na wengineo ila timu ikiboronga hua hawaonekani humu.
Poor Masingeli na chawa wake
 
Zile ni issue serious kabisa ndiyo maana akabadili ID, wala siyo kwa sababu ya timu kufungwa 😂😂😂. Pia Hamisi hapendi kukurupuka. Atasubiri watu na mihemuko yao waongeeee weeee. Halafu ndiyo atakuja na majibu. Timu ikifungwa na watu wakimponda Arteta, Hamisi anakuambia kwa utulivu kabisa kwa nini Arteta ni master. Watu wakimponda Kai, Hamisi atakuambia kwa utulivu kabisa kwa nini Kai ni mwamba, siyo kama kina Masebene, Mason Mount kina Vegosti na Sabisa. Na mwisho wa siku mwamba huwa anaonekana yuko sahihi na alikuwa sahihi na alichosema.
 
🅱️USARA ZA GWIJI WA HIGHBURY

✍🏾 Arsenal Tangu 2018 (KSE) kroenke Sports & Entertainment Wanunue Hisa Zote za Arsenal Ambazo kikawaida zinamilikiwa Na Arsenal holding PLC kwa sasa KSE ni Parent Company inayomiliki hisa 100%

✍🏾 Baada kukamilisha Ilo Ndio Kroenke ambae Arsenal Fans Wengi wanamtambua kama Bahiri Sababu Miaka Mingi alikuwa Mgumu kutoa pesa

✍🏾 Ila uyu Bwana pia alisubiri awe mmiliki Wa jumla aweze kucontrol Cash flow yote sio kushare na Share Holders wengine kwenye maamuzi.

✍🏾 Baada 2018 tunaona jamaa wakianza kuinvest kwenye Club kipindi Covid jamaa alisaidia team baada kununua madeni ya Club Ambazo zilikuwa Ni interest rates za mabenki mikipo kipindi kile ujenzi uwanja

✍🏾 Alinunua Rates ili sasa Arsenal ije imlipe yeye kwa riba ndogo tofauti Awali riba za kibenki jamaa akaanza onesha Commitment. Lengo ilikuwa kufanya Cash flow Club wakati huo Covid ambao mapato vilabu yalipata misukosuko

✍🏾 Usajili tukaanza kuona pesa inatoka kina Partey , Kai, Rice, Peoe Nk ni pesa nyingi ambayo awali ilikuwa ngumu sana Arsenal kutoa

✍🏾 Mpaka Sasa KSE wameweka pesa Nyingi tu Arsenal na bado wanaweka

✍🏾 Ila jambo ambalo bado Arsenal hatupo Vizuri ni mauzo wachezaji hii inafanya Net spending inakuwa kubwa sana itafika stage financial status itatuzuia kusajili kama hatuna biashara nzuri mambo FFP

✍🏾 Je unafikiri Summer tunaweza kuuza nani ili kuweka Vitabu vyetu vizuri team inapofanya vizuri pia itaongeza Value wachezaji hili eneo kuuza nalia nalo sana

Amigos
 
Kikubwa nilichokigundua ni kua Masingeli ana kipaji kikubwa sana cha ushawishi, huyu jamaa anaweza kukuanimisha Manara ni mzungu baba yake ni mDenmark na mama yake ni mCanada na asilimia 98 ya Arsenyau humu wakaamini.
Huyu jamaa angekua ni mwanasiasa angekua ana kula tu mema ya nchi, kwa huu ushawishi wake kuna wakati akili yangu inaniaminisha huwenda huyu muhuni ni Makonda, tunakaa kupigizana kelele humu kumbe huyu mwenzetu ni Katibu Mwenezi wa chama

Huyu muhuni hata akiamua mwenyewe nyumbani kwake kufungua kanisa la upako ni atapiga pesa ndefu sana, jamaa lina ushawishi wa hali ya juu sana.
 
Hata Kai mlimkata kwny Penalt box refa akapeta....mstari inaonesha clear offside...tuliwabonda na tutakuja kuwabonda tena...bdo hamna kikosi cha kutuzuia kwa Sasa ..kipindi kile tunawafunga tulikuwa hatujazoeana sembuse Sasa King Kai kashakaa sawa....hesabuni maumivu
 
🅱️USARA ZA GWIJI WA HIGHBURY

*Bukayo Saka True definition of Inverted winger"

✍🏾 Kwa Jinsi Saka anacheza Winger ya kulia kuna watu wanaweza kufikiri ndio Upande wa mguu wake Strong hapana Kulia ni Weaker Foot ya saka nikiwa na maana Saka ni Left footed player

✍🏾 Why Anacheza kulia? hapa ndio tunakuja kitu Modern football tactical Development tulizoea Winger wa kawaida lazima akiwa mguu kulia acheze kulia

✍🏾 Mpira wa kisasa sababu una deal na Roles ( Majukumu ) zaidi ukatuletea Inverted winger mguu wa kushoto anacheza kulia au mguu kulia Anacheza kushoto

✍🏾 Lengo kubwa Ni kuongeza uwiano wa kutengenezaji nafasi na mashambulizi bila kusahau kufanya mashambulizi yako yasitabilike

✍🏾 Ni ngumu sana Beki anatumia Mguu kulia kukaba Mshambuliaji anaetumia Mguu kushoto sababu movements zake azitabiliki

✍🏾 Inverted Winger kama Saka ana umuhimu mkubwa sababu uchezaji wake hautegemei tu kupiga Cross kwenye box kamaTradition winger walivyo.

✍🏾 Saka anaweza kucut inside akaingia katikati kufanya link up na viungo au kutengeneza nafasi kushuti na mguu wake ambao ni strong

✍🏾 Fatilia magoal mengi ya saka anavyo funga akiwa katokea pembeni kushoto uwa ana cut inside kwanza then ana shuti

✍🏾 Hii ni moja faida kuwa Inverted Winger Saka anatimiza majukumu haya kwa ufasaha kabisa akifata nyayo za kina Arjen Robben one among of the best Inverted Winger

Bukayo Saka one of our Own📌

Amigos
 
Nyie tutachapa sana nacho wapendea Wenger orphans hata tuwe unga vipi nyie ni kati ya mboga yetu pendwa sana pale uingereza.

Ben White vile akimuona Rashford round hii mumpumzishe ben jamani rashidi atakuja kuua uyu bwana.View attachment 2938299
Mara ya mwisho kutufunga kiungo alikuwa lokonga


Nyie tutapiga 3 half time

Haya manafas mnayoacha ,Arsenal atawapigeni nyingi,

Kwenye kushambulia Arsenal wanakuwaga watano kwenye 2-3-5


Liverpool waliwadharau wakajua hamuwezi kujipapatua


Arsenal ya Arteta ukicheza hivi na mtacheza hivi, mkipona sana half time goli 3 ,sikufichi
 
Nyie tutachapa sana nacho wapendea Wenger orphans hata tuwe unga vipi nyie ni kati ya mboga yetu pendwa sana pale uingereza.

Ben White vile akimuona Rashford round hii mumpumzishe ben jamani rashidi atakuja kuua uyu bwana.View attachment 2938299
Suala la kutufunga safari hii msahau 🤠🤠..zile 3 mlizokula raundi ya kwanza zilezile tuna copy na ku paste
 
Huyu kocha ana mdomo sana ,inatakiwa siku hiyo ni kuwapiga Pini ,piga msako sana ,


Erik Ten Hag after beating Liverpool YESTERDAY:

“At Arsenal, the fourth game of the season - we should have had a penalty in the 87th minute, we scored with Garnacho, disallowed. Then we concede a goal that should always have been disallowed.” 🥱 #afc

Bora Chelsea Huwa Wana turn up na wanaweza kukupa game ngumu, sio Hawa manjesta, Jana Liverpool walipoongoza 2-1 , wakawa wanacheza tu muda uishe ,walikuwa wanaweza kuwapiga hata goli zaidi ,


Huo ujinga Arsenal hatuna ,ukiingia kwenye mfumo tunakulamba za kutosha


Cheki wanavyoaacha manafasi halafu sio mara moja ,


Unahitaji pasi 1 had 3 kufika golini kwao


Kabla msimu haujaisha ,manjesta atapigwa 5-0 had 6-0


Bado Kuna timu zinafanya utani sana


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…