Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Huyu Isak ndiye top scorer wa Newcastle?
 
Castr akiijibu hii nitag
 
Nielewe nilichoandika. Sijasema haziuzi wachezaji, fuatilia style ya Palmer kuuzwa, alimuambia Pep anaondoka kwaajili ya game time. Pep akajibu subiri Mahrez akiondoka utapata namba dogo akagoma.

Trophy oriented team, mchezaji kama ni potential haimuuzi labda atake mwenyewe. Angalia Beckha, ilibidi apigwe na kiatu usoni ndiyo aende Madrid.

Kwa misimu miwili mfululizo Silva anamuomba Pep aondoke ila Pep anagoma, hapo hapo Pep anauzw wengine.

Mata aliyeenda United alicheza mechi ngapi?

Katika timu zilizo busy na kusaka trophies ni City tu ndiyo inauza sana wachezaji, na siyo wa pesa nyingi misimu yote. Mara ngapi umesikia City anaongoza mauzo ya jezi? Mara ngapi umesikia City anajaza uwanja?

Nyumbu na form yake mbovu aliyonayo kampuni ngapi zinakimbilia kuipa deals za matangazo mbele ya City? Vitu vitatu vinavyochangia mapato kwa City havipo kwa 100%, ni ajabu wakiuza wachezaji kuliko trophy oriented wengine?
 
Kai n alternative sasa hivi anapata namba sababu Partey n injury akirud kiungo atakua Partey, Rice, Odegard
Sasa partey anacho kipi cha kumzidi Bruno,Elite coach ukimpatia Bruno na Rice atafurahi ,phalihna na Rice atafurahi,Rice na Enzo atafurahi,kiufupi Rice anacheza na midfield yoyote awe DM,CM
 
Hoja yako naona kama umeificha, ni kweli hatujawai kuuza wachezaji kwa gharama kubwa so what?
usije ukawaza kwamba ndo haatujawai kuuza mchezaji wa profile kubwa, maana naiona hoja yako kama imejificha hapo kwamba mchezaj mkubwa ndo pesa kubwa. Wakati flani hizi deals zina mambo mengi haziendan na uhalisia kuna wachezaj wameuzwa/kununuliwa hawaendan na thamani zao. Tuseme Arsenal kwa namna flan tume feligi kwenye deals za kuuza wachezaj tumeuza wachezaj wa viwango vikubwa zaidi ya lukaku kwabei ndogo ukilinganisha na lukaku kutoka manchester kwenda inter mfano Vanpersie. Kuna Sanchez pia angewezwa kuuzwa kwa bei nzuri tu kulingana na kiwango chake wakati ule lakin ndo hvo, na mifano kama hiyo ipo mingi. Kwahiyo na kubali kwamba hatujawai uza mchezaj kwa bei hiyo lakin tumeshauza wachezaj wenye profile kubwa zaid ya pesa hiyo.
 
Huyu Isak ndiye top scorer wa Newcastle?
Yah! Wamefungana Wawili Pamoja na Wilson Goli 7 kila mmoja. Nyinyi kwenu anayeongoza kwa Magoli ni Nketiah na SAKA wakiwa na 5 kila mmoja.

Wewe ni moja ya Mashabiki wa hili jukwaa mnaokuwaga na Hoja mara nyingi na Mkorea na Smith Rowe! Changamoto kuna muda mahaba kwa timu yanazidi.
JESUS Ana Michezo 11 sawa kabisa na ISAK ila wanatofautiana dk chache ila ana Goli 2 na ISAK ana Goli 7.

Tuweke Mahaba pembeni sawa Umemwona ISAK la Liga, na amekuja EPL bado anacheza Poa. "Toons" Kikosi chao kina wachezaji wachache sana wenye Kipaji cha Asili na Mmoja wao ni ISAK. Huyu Bwana angekuwa ni CF/ST wa Arsenal angekuwa na mchango mkubwa kuliko Mnaoupata kwa JESUS.
Katika timu zilizo busy na kusaka trophies ni City tu ndiyo inauza sana wachezaji
Nimezungumzia CITY, CHELSEA NA LIVERPOOL. Kuuza haimaanishi huwezi endelea tafuta Makombe. Liver Imeuza Coutinho ikapata Balance ya timu na alikuwa Key Player Ikaenda win Mpaka UCL, Chelsea imeuza Hazard akiwa key Player bado wameendelea tafuta makombe. JESUS kaondoka kama Plan B ya Pep lakini wameenda chukua "TREBLE"

Kifupi kama Huuzi Huna Bidhaa Bora inayohitajika Sokoni. UTD kwa sasa unadhani kuna wangapi tunaweza Uza thamani inaeleweka? ARSENAL ya Miaka kadhaa ndo kundi walilokuwepo.
 
Huyu Isak ndiye top scorer wa Newcastle?
Ndio ana goli saba,pia Wilson ana goli saba Hawa viumbe wako mbele sana ya Jesus kuuweka Mpira wavuni na ni injury prone wote .
 
Unaruka ninachoandika.

Let us go with baby steps kutoka nilichoandika.

Trophy oriented team kama Bayern.

Hukuti kauza mchezaji 60M+ kwa misimu minne mfululizo.

Timu ya hivi.

Ikiuza mchezaji wa hivyo, haitajirudia kila dirisha la msimu.

Kwa United Ronaldo aliuzwa mwaka 2009 lukaku akauzwa 2019. Ikapita miaka 10 kufanya deal kama hilo.

Chelsea wamemuuza Hazard 2019, Kai 2023, Mount 2023.

Niliandika 60M ila naona umetumia 55M kwa City, well let us go with this. Ukiachilia Torres waliouzwa kwenye hii list wawili ni majeruhi nje nje mmoja anastruggle na form. Na hata Torres huko alipo anastruggle kuanza. Unaelewa nini nikisema mchezaji mwenye mchango haachiliw? City alimtoa Sterling Liva kwa sh ngapi?

Kuhusu Barcelona. Niliandika hivi 'Barca kauza Neymar kwa pesa kubwa, haijauza mchezaji mwingine kwa nusu ya ile pesa. Hata nikiikubali mifano unayotoa, unaelewa nini nikisema time frame ya hizi deals haiwezi kufuatana?

Kwa Madrid ukiachilia Ronaldo na Morata waliobaki walikua wameenda kumalizia career, also notice time interval ya hizi deals.

Liver/ Klopp alimuomba Coutinho abaki, ikabidi amchezeshe mechi UEFa ili Barca waghairi ila Barca walikomaa. Pesa ya Coutinho ndiyo imeileta Liva ilipo leo.

Jitahidi kuelewa usiandike kwakua una MB. Liver ile pale, Salah msimu uliopita katakwa na timu za kiarabu, umeona Liva ikiconsider hizo offer?

Madrid inatoa 90M kununua mchezaji, kisha jezi zamchezaji zinarudisha hela yote au nusu na robo ya hela ndani ya wiki. Hii timu hata bila kuuza mchezaji itajiendesha bila wasiwasi.

Unajibu ndiyo, lakini unajibu bila kuangalia kila ninachosema
 
El Tiger jibu lako la Coutinho lipo hapa
 
Mara nyingi hua nasema humu kwamba kwa Jesus ni ngumu kutegemea magoli. Yeye pia amewahi kujisema hivyo.

Liva ya Mane na Salah top scorer walikua ni Mane na Salah ingawa Firmino alikuepo, Isak ana shot power kubwa kuliko Jesus na anaweza piga mpira sehemu hauitarajii. In terms of skills na game involvement Jesus kwangu kamuacha Isak.

Siwezi kujudge kama Isak angefaa Arsenal ama la kwakua Arsenal anacheza JDP na tangu la liga mpaka EPL Isak hajachezea timu inayotegemea JDP.
 
Ndio ana goli saba,pia Wilson ana goli saba Hawa viumbe wako mbele sana ya Jesus kuuweka Mpira wavuni na ni injury prone wote .
In terms of scoring Nketiah ni clinical kuliko Jesus pia lakini mashabiki na kocha wanakubaliana kwamba Jesus anatakiwa kuanza.
 
Namba gani ndo majukumu hayo mzee, ukishasema namba tisa majukumu yake yana julikana, havertz ni versatile player unaweza ukamtumia mpaka false nine nafasi ambayo siioni guimaraes hakiimudu, Guimaraes ndio ana kipiga kuliko havertz lakin katika nafasi gani!? box to box teyar tunae Rice na Partey haya mtoe mmoja mweke Guimaraes,
Kumbuka Rice, Partey, Ode, Havertz wanaweza wakaanza wote Havertz akacheza kama striker(false nine) lakin guimaraes hayo majakumu hayawez itabidi asubiri kati yahao wawili(partey na rice) atoke mmoja aingie Sub. Kila mmoja ana tamba pande zake, usimchukulie poa Havertz
 
Hapo kwenye Skills angalia Tena ,ISAK ukimuacha na mabeki wawili umekwisha ,anafunga soul goals kama Hazard au Messi hiki kitu hauwezi pata Kwa Jesus ,naona haujamtambua huyu msomali ,kwenye skills Jesus hafiki hata nusu niambie kitu kingine .Ndie namba Tisa Epl mwenye skills ya kuwatoka mabeki Kwa kuwafuata.
 
But position pia inahitaji profile ya mchezaji ifit na mnachotaka mfano AM anaweza kucheza LCM/ RCM au LW/ RW kwakua mahitaji ya hizi nafasi yanakaribiana.

Now what if ukamchukua AM umfanye DM? Ni disaster. But Bruno na Rice wanaweza cheza pamoja kwakua Rice anaweza yabeba majukumu ya 8. Ila tukisema Rice akae benchi kwaajili ya Bruno hapo siwezi kukuelewa
 
Jesus hafuati mabeki?
 
Mikel Arteta on Kai Havertz:

"I think he's felt especially the support of all of his teammates and the club behind him. Now he's feeling as well all the support from our people, which is extremely important.

That's why we've seen now a great version of him." [sky]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…