Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Bado hana kikosi cha kuhimili kuusaka ubingwa. Wamepita na mkeka wangu bila huruma.
Tuwape muda. Son naye kaumia. Kocha mpya mbishi mbishi labda watu wameanza kumsoma na kumuelewa.
Sisi pia tunapaswa kupambana maana tuna majeruhi kadhaa pia na tunatakiwa kuwatumia vizuri wale walio fit. Kina Castr walisema wanaona sisi tutaanza ligi January. Acha tufike January vizuri.
 
Nilisema juzi hapa baada ya Nick Pope kuumia , Newcastle walete haraka £50m kwa Ramsdale, lasivyo watapigika Sana


Na Arteta kasema hataki kumuachia January,labda ije hela ya kueleweka

Kwanza Hana haraka ,alimsainisha mkataba mrefu mwaka huu

Alimnunua £30m , bila £50m hauzwi
 
Spurs Kuna watu walikuwa wanasema Ni title contender
Kwa namna walivyoanza Spurs niliona inastahili kombe lolote msimu huu.

Ile game na chelsea ange alivyotetea high line kwa jeuri huku akiwa pungufu nikaamini they have their own Erik. Juzi hivi nikasoma sehemu Ange anasema anashangaa makocha wanaosema hawana wachezaji sahihi kwaajili ya mfumo fulani.

Nafikiri he is too eccentric for Spurs. Itamsumbua na maneno yake yatabackfire
 
Nyukesto ni Westham yenye hela anabisha. Akitoa suluhu na timu za farmers' league anaona kaiva anakuja hapa na khanga kiunoni kubishana kwamba eti wao ni timu tishio kwa sasa.

Hiyo timu ya ligi ya wakulima uliyosuluhu nayo nyumbu na ubovu wake alishinda game
 
Mnaona kama kazi mliyotutuma tuliishindwa kwa hiyo mmeamua kuifanya wenyewe?
Kazi tuliyowatuma iliwashinda,na mlipita njia tulizopita msimu juzi.
Tukawaambia yule jamaa ni mwehu,msiridhike mapema
Nyie mkalewa misifa😂
Kiukweli niliumia sana Aseno kukosa ubingwa EPL last season.

Safari hii iwe Kwa kuvunja mifupa, machozi,jasho, na damu tunabeba.
 
Nyie wenyewe juzi juzi tu hapa mlikuwa hamjiamini kwa sababu ya midfield na defence yenu. Mmepata viungo wanaosaidia ushambuliaji wenu ila bado upande wa ulinzi. Labda kuumia kwa Matip ni bahati kwenu kwa kuwa mtalishughulikia suala la ulinzi January. Nyie pia ni wa kuangaliwa mnavukaje January.
 
We subiri utaona mafekeche yetu😂
Kama tulishinda na wale mababu..sasa safari hii ndio kivumbi.

Sifa yetu ni kikosi finyu,,tunafanya njia pasipo njia.

Kwanza waulize hata wenzio,balaa letu wanalijua🤣🤣🤣🤣🔥
 
Usiwastue mkuu....Hawa inatakiwa tuende nao hivihivi...fumba na kufumbua gepu la point nane ndo wataelewa shoo vzuri...sasahv acha tukimbizane taratibu....niliwahi kusema humu kipara asijaribu tena kuacha lile gepu la mwaka jana likajirudia....atajuta na ameshaanza kutepeta mapema...Hawa Liver wao wanajifanya wabishi...wakipata key injuries mbili tu tutaelewana mdogomdogo
 
Hadi sasa tuna injuries nyingi tu na tunakimbiza
Hivi nyie ndio wa kutustua sisi kweli?
Ama lile kuti kavu pale juu linawapa jeuri mnaona mmemaliza?

Pale hammalizi round 2 mnatoka.


Subirini moto,mmsiyempenda kafika😂
Ukweli mchungu...
Magap ya kipara mliyochezea sindimba mwaka jana akawapokonya tonge mdomoni,sie hatuna msalia mtume 😂
 
We subiri utaona mafekeche yetu😂
Kama tulishinda na wale mababu..sasa safari hii ndio kivumbi.

Sifa yetu ni kikosi finyu,,tunafanya njia pasipo njia.

Kwanza waulize hata wenzio,balaa letu wanalijua🤣🤣🤣🤣🔥
Sisi tupo mbele hapo tunawatimulia vumbi. Nyie mnatukimbiza huku mnatafuta majibu nje. Sisi tunaonekana kama tuna majibu yetu ndani na majibu hayo kama yote yatakuwa yamepona January. Tukimpata Palhinha au Douglas Luiz tu, tunajihesabu kama ubingwa tumeshauchukua. Mkiharibu tu January, hata mkitupita kidogo tutakuja kuwafanyia kile Kipara alichowafanyia mara kwa mara na kile alichotufanyia sisi msimu jana.
 
Nadhani wewe hii timu hujaisoma vizuri😂😂😂
Hizi ni tabia za hii timu,title contenders ..ndio wale wasafiri wanebeba masanduku na tiketi hawana🤣
 
Nadhani wewe hii timu hujaisoma vizuri😂😂😂
Hizi ni tabia za hii timu,title contenders ..ndio wale wasafiri wanebeba masanduku na tiketi hawana🤣
Sasa mfano wa masanduku si unawafaa nyie? Ngoja February ifike tutakuwa tumeshaelewana.
 
Nadhani wewe hii timu hujaisoma vizuri

Hizi ni tabia za hii timu,title contenders ..ndio wale wasafiri wanebeba masanduku na tiketi hawana
wasafiri wanaobeba masanduku halafu hawana tiketi wala nauli.
Kwa huu mfano uliowapea arsenyau unaitwa vivid example yaani hata wale raia wa mirembe lazima waelewe somo.
 
wasafiri wanaobeba masanduku halafu hawana tiketi wala nauli.
Kwa huu mfano uliowapea arsenyau unaitwa vivid example yaani hata wale raia wa mirembe lazima waelewe somo.
Mmeshinda kwa kubahatisha,tayari ushaanza kurandaranda humu



UCL mnaburuza mkia
 
Watu Wana underrate Sana eneo la GK , Newcastle kaumia Nick Pope ,wameambiwa watoe £50m wamchukue Ramsdale wanajivutavuta wanataka wavuzie Degea wabure

Sasa kufika February watakuwa wanagombea kucheza conference league na kina Chelsea ,man u
 
Andre wa Fluminense anaenda Fulham kuziba pengo la Palhinha anayeondoka


Arsenal wataongeza watu wawili January Kiungo na Beki


Ile kauli tunaanza Ligi January ina mashiko ,tuombe Mungu tuwe kwenye title race ,hata Kama nafas ya 2 tusiachwe zaidi ya point 3


Leo kwenye Press ya Arteta baadae ,inasemekana atatoa taarifa za majeruhi Partey na Smith Rowe

Kama itakuwa vzr ,Partey awepo kwenye mech ya Dec 23 ,Anfiled ,


Tomiyasu atakuwa nje wiki 4-6 , January akiwa fit anaenda kwenye michuano ya Asian Cup , Partey anaenda AFCON


Ndio maana kipaumbele cha kwanza tutasajili Beki mmoja na kiungo mmoja .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…