Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Wazee wa lisupa kompyuta linasemaje huko, asenali atachukua kombe lolote msimu huu?

Masingeli tayari kashawaaminisha msimu huu wanachukua Uefa, tena kawathibitishia kabisa hakuna kombe rahisi kuchukua kama Uefa.
Ukimuuliza kama kuchukua Uefa ni rahisi hivyo kama unavyotuaminisha kwenye kabati la Arsenyau kuna makombe mangapi ya Uefa?
Anakuita wewe uliohoji hilo swali ni anti semitism
 
Mtachukua manjesta ,huoni mnaongoza kundi lenu la UCL

Geuza msimamo mnaongoza kundi
 
Mpaka leo Mkuu bado una mentality ya kuwa nyumbani na ugenini mbona mpira siku hizi hauna hiyo. Mtu anapigwa popote pale akikaa vibaya.

Nyumbani na Ugenini ilikuwa kipindi cha miaka ya 2000, Ferguson na Mourinho walivyojijengea ngome zao. Lakini Mourinho mwenyewe siku hizi hata akiwa nyumbani anapingwa tu
 
Timu yetu na ubovu wake , nimeanza kupenda tu kuona mpira wa kushambulia
Pochetino kaanza kubadilika polepole , ule ushamba wa back pasess kaacha ,sasa hivi vijana wanawasha moto
Utafurahia zaidi pale Nkunku atakapopona na kusimama pale mbele, huyu Wacko Jacko naona anawachelewesha tu.
 
Nyie kondoo hivi mna uwezo hata wa kumfunga City goli nne kweli? Au mpo hapa kudanganyana kuwa mna timu y kubeba ubingwa.

Labda utumie hizi hesabu za std one zinaweza kukusaidia kuelewa:
Arsenal v City = 1-0 = (Arsenal 3 pts, City 0pts)
Chelsea v City =4-4= (Chelsea 1pt, City 1pt)

Kati ya Arsenal na Chelsea, nani kamfunga City?
 
Labda utumie hizi hesabu za std one zinaweza kukusaidia kuelewa:
Arsenal v City = 1-0 = (Arsenal 3 pts, City 0pts)
Chelsea v City =4-4= (Chelsea 1pt, City 1pt)

Kati ya Arsenal na Chelsea, nani kamfunga City?
 
Msimamo wa PL kuelekea International break!

Tukirudi, Man City watawakaribisha Liverpool!

Man United watakuwa away dhidi ya Everton!

Chelsea uso kwa uso na Newcastle United!

Wakati Brentford akikutana na Arsenal!

Ligi inazidi kupamba moto, na wanataka ubingwa wanaonekana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…