mkorea
JF-Expert Member
- Aug 16, 2016
- 8,592
- 19,228
Mkuu hapo chini ndio umeua kabisaDah hili jukwaayaani hatuna mechi ila uzi uko no 1 trending.watu wanapigana spana balaa na ni nzuri kwa afya ya jukwaa.
Kuna mtu aliwahi nambia yafuatayo.
1.ukitaka kwenda mbali kimbia,ila ukitaka kufika mbali heshimu watu unaoongozana nao katika safari yako maana huenda wanajua huko mbali unakotaka kwenda.mashabiki tupendane.activenes ya group inamhitaji kila mtu.
2.kama hujawahi kusikia au kuona jambo isiwe sababu ya wewe kuamini halipo.tusiamini tu katika mifumo tunayoijua kwamba ndo italeta mafanikio bali mifumo ilitengenezwa,inatengenezwa na itatengenezwa na itatushangaza.
3.ndoto na maono(dream & vision) vinaufanano mkubwa katika tofauti zao.kocha wetu na wachezaji wetu tusiwalinganishe na wengine maana wanafanana lakini hawalingani.
4.milango yote ya fahamu(macho,masikio,pua,ngozi) vimewekwa nje na vinaonekana wazi muda wote iwe vinatumika au havitumiki,jiulize kwanini ulimi umefichwa na unaonekana wakati wa matukio pekee(kuongea).
Kila mtu na aangalia anavyozungumza hapa jukwaani hasa anapotoa ulimi wake kwa njia ya maandishi.
#Arsenal ndoo
#Nketiah kiatu
Arsenal NDOO
hiyo ndoo inaandikwa hivyo