Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Huyu Leo tunamuwekea Havertz Mzee wa 0 shots on target na ikitokea hajapaisha basi kipa kadaka au inamgonga post Ili kuwadanganya. Kwenye ligi tunamuweka bench afu tunamuweka mbappe Ili tuwaadhibu kisawa sawa
eti kwenye ligi tunamuweka Mbappe.
Timu maskini kama Arsenyau unafikiri itakua na uwezo wa kumlipa Mbappe mshahara?
Labda nyie mumsajili halafu Man Utd tuwe tunawalipia mshahara wake la sivyo hamtoboi mwaka hio Academy yenu inafilisika, halafu Majembe Auction wanakuja kupiga mnada hayo mabenchi ya Emirates stadium ili kupata pesa kumalizia kulipa mshahara.
 
Oya hiv unajua Graza hawauzi Tena timu ?

Wale jamaa wanajuaga kucheza na akili zenu
 
Pesa kwetu ni nyingi mpaka zinafurika. Huyo Onana mwenyewe leo tukimwambia tunamtaka awe back up wa Ramsdale, kesho tu unamuona kavaa ', Emirates fly better' kifuani
 
Naamini mchezaji yeye kama bidhaa hapati kitu kwenye kuuzwa kwake. Yeye ni mishahara, madili ya matangazo ya soda, njumu, etc. Pesa za mauzo wanakula club na agents wa mchezaji
Sasa inakuaje mchezaji anakua amebakiza mwaka mmoja halafu anauzwa timu nyingine kwa mkataba wa miaka4 bila ya kupewa chochote kwenye mauzo yake?
Yaani hapo anakua ameongezewa miaka 3 tena mbele.
Ndio maana Waswahili kama Mbappe wanataka kutegea kwanza mkataba uishe ili akarambe pesa ya mkataba mwingine.
 
Rice hapati hata Mia , hiyo ni ya klabu husika yote

Akiwa free ndio anapata signing fee
Sasa huoni kama mchezaji anakua amedhulumiwa?
Mfano Rice alikua amebakiza mkataba wa mwaka 1 na Westham halafu anasajiliwa kwa mkataba wa miaka 4 na Arsenal, huoni anakua ameongezewa kandarasi ya miaka 3 mbele bila kupewa malipo ya hio nyongeza ya mkataba wa miaka mitatu?
 
Oya hiv unajua Graza hawauzi Tena timu ?

Wale jamaa wanajuaga kucheza na akili zenu
Hilo dili la Mbappe hao Glazzer wanaweza litumia kunyamazisha kelele za mashabiki.
Wakimnunua Mbappe mashabiki wanapoa wenyenyewe badala ya kuendeleza campaign ya "Glazzer Out" wanaanza kuzungumzia ukontenda mada faka.
 
Bei ya mchezaji ni mtakavyothaminisha tu

PSG wanajua mbappe akibaki aje aondoke free wao hawapati chochote., Na mbappe anaenda kunegotiate na timu yoyote yeye anakuwa Kama timu Sasa ,hapo anavuta mkwanja mrefu

PSG wanataka wao wapate chochote nimeona wanasema wanaziita klabu zote zinazomtaka na Bei haitakuwa kubwa

Tatizo la mbappe ni mvurugaji anaweza haribu timu nzima

Wafaransa huwa Wana ego ,refer Paul Pogba ,
 
Hilo dili la Mbappe hao Glazzer wanaweza litumia kunyamazisha kelele za mashabiki.
Wakimnunua Mbappe mashabiki wanapoa wenyenyewe badala ya kuendeleza campaign ya "Glazzer Out" wanaanza kuzungumzia ukontenda mada faka.
Sasa hivi kuelekea kufunga usajili watampa pesa Kocha wenu asajili ili msiwasumbue , wale jamaa kuiuza manjesta sio rahisi

Wale wa Liverpool waliweka timu sokon,w , mwisho wakasema haiuzwi na Sasa wapo wanaendeleza maujinga yao
 
Pesa kwetu ni nyingi mpaka zinafurika. Huyo Onana mwenyewe leo tukimwambia tunamtaka awe back up wa Ramsdale, kesho tu unamuona kavaa ', Emirates fly better' kifuani
mashabiki wa Asenyo aiseee
halafu nilichogundua mashabiki wa Asenyo Tanzania wengi ni wazaramo maana wana maneno kwelikweli.
 
mashabiki wa Asenyo aiseee
halafu nilichogundua mashabiki wa Asenyo Tanzania wengi ni wazaramo maana wana maneno kwelikweli.
Vice versa is true , mashabiki wa manjesta ndio mnaongoza kwa mdomo ,

Ila Arsenal na manjesta ndio wanaochagamsha hata mitandao ya kijamii, wote waongeaji , wote Wana arrogance na timu zao

Huko USA ,wanasema tiketi zimeisha asubuhi Jana

Sasa peleka mech sijui ya Chelsea ,mancity uone Kama watajaza uwanja , mechi za Madrid ndio angalau zinajazaga uwanja ,lakin Arsenal vs manjesta wanasema imeweka rekodi
 
Wanaotaka kuiona mechi bila shida

Kama una Startimes home Basi channel ya MUTv wataonesha,

Kama huna startimes Basi download app yao ,Kisha lipia kifurushi Cha Max ,kwa siku moja ,sh.2200 tu

Weka pesa kwa tigo pesa nunua kifurushi Cha siku moja

Utaiona mechi bila kutumia MB

Hizi link zitawasumbueni ,mtashindwa kuona flow za pass,
 
Hapa umeongea la maana sana, yaani anaweza kuja kuleta issues, akampa tabu Arteta kwenye kummanage..

otherwise ni mchezaji mzuri sana.., wa kuchukulia UEFA
 
Statistically, Rice ndiye anatakiwa aanze chini halafu Partey na Odegaard waanzie juu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Statistically, Rice ndiye anatakiwa aanze chini halafu Partey na Odegaard waanzie juu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Labda hujafanya utafiti vzr ,au sababu umemuona Sana Rice kwa timu Kama Westham wanaozuia Sana ,ila Rice ana statistics nzuri Sana za kucheza adv 8 , ndio maana hata Pep alikuwa anamtaka Kama mbadala wa Gundogan

Rice alikuwa kwenye timu yenye mentality ya kuzuia lakin ana takwimu za pass akishindana na Rodri , ana takwimu za magoli kuliko mawinga wengi EPL, ana takwimu za kupiga pass final third akifukuzana na viungo wengi wa juu


Partey ukimuweka nane Kuna vitu utakosa , kwanza sio mfungaji mzuri ,Raha ya Partey acheze chini asambaze mipira kwa double 8s
 
Naamini mchezaji anaangalia kulinda mapato yake binafsi. Yeye kama mchezaji anaangalia pesa atazopata Kwa kazi yake ambayo ni kucheza mpira, lakini pia na mambo mengine yanayohusu yeye kama 'brand'. Mfano mshahara wake ni 100 Kwa wiki. Je akienda kwingine atapata hiyo 100 Kwa wiki vile vile au zaidi? Je atapata madili ya matangazo? Kufanya appearance mahali, au movie, nk. Je akiumia? Atakuwa chini ya uangalizi wa elite medical teams ama la? Hii inampa confidence kwamba akiumia atawahi kupona na kurudi uwanjani. Je kocha ni mzuri wa kumpeleka next level Ili aimarike na kukuza brand yake zaidi na kupelekea kupata pesa zaidi?Kama mshahara wake utapungua kwenye club mpya, je kuna mahali watasubsidize? Na mambo mengine kama hayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…