Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Noted
️ Sir
 
Ngoja tujipange msimu ujao.

Ila nilichojifunza kama tutaendelea na ubahiri wa kutofungua Pochi na kusajiri wachezaji wenye viwango tunaweza kupata aibu Kule Champions league
Kule ni kwa magiant na I don't see kama Arsenal ataweza kupambana kule imagine Europa league pekee Arteta amefeli to the maximum na yupo na kina sporting,lyon,PSV je huku ambako kuna Bayern, Madrid,Manchester City (
huyu katupiga home and away ligi na katutoa FA cup)
 
Kwanini ashindwe kupambana sababu zako ni nini???
Uyo city unaemtolea mfano kachakaza kila mtu iwe buyern, kumbuka uyo city ni timu bora dunian aisee, nashindwa kuelewa yan unaona kama city ni timu ya kawaida sana ambayo ni dhambi kubwa sana kuifunga arsenal home and away? Au mie ndo sijaelewa maana yako
 
Unajua bwana mdogo uwe una reason vitu,that's why nikiongea naonekana nipo against na Arsenal fans but nina akili na ninajitambua unataka kuniambia Arsenal ataweza kucompete champions league ?na squad ipi?ambayo kusajili ni tatizo?miaka mingapi Europa league tumetolewa mfululizo chini ya Arteta ambako kuna teams za kawaida tu na tumeshindwa?ukiachana na City sisi tunaweza kucompete na Bayern Munich?Real Madrid?Manchester City kwenye champions league?sometimes usiwe among Arsenal fans ambaye unapenda kuongea ili mradi uonekane umeongea wakati ukweli unaujua season hii kwa wanaonijua nilisema ni heri Arsenal akomae na Europa league tupate kombe la ulaya nikaonekana mjinga na nilishaona mbali kuwa kwenye ligi ni maajabu tukibeba sasa imagine kwa squad ya Arsenal icheze Champions league kisha ligi kwa squad ile ile tutatoboa?Arsenal Europa league imemshinda licha squad ilikuwa inabadilika cha muhimu Arsenal anaenda kushiriki champions league aingize fedha that's it hapo nitakubaliana na wewe
 
Ni kweli Mkuu, ila ngoja tuone dirisha la usajiri tutaletewa watu gani kutusaidia.

Nimesoma mahali Xhaka anaondoka, hivyo atahitajika mrithi wake pia
 
Brother kuna uzi mmja nahis kama sio wa liver alikuja na hoja ya kusema "anaona arsenal ikiporomoka zaid msimu ujao tena hata top 4 ni ngumu kuingia" kwa kutoa sababu kama zako izo izo ila kauli yangu ya mwisho ni kua asubilie sajili za timu zote ndizo zitaamua,.. Nashangaa baadhi ya mashabiki wa Arsenal hawana imani kabsa kama usajili utafanyika kwa kulingana na pale tulipojikwaa msimu huu ila wao wanaona kuliko hata viongozi wanavyoona,
" Em subili sajili maingizo mapya ndipo utaanza kutoa maoni yako kama tutashindana ama hatutashindana" maana naona kama wengi mnaamin hiki kikosi ndicho icho icho kitaenda msimu ujao.
 
Swali langu kwako Arsenal ni lini ishawahi kutoa fungu la pesa kwa ajili ya usajili?mean fungu la maana?pia inategemea na coach na wachezaji anaowataka but Arteta atawapata anaowataka?Kroenke hela atatoa?yes tunakubali sometimes usajili unaweza ukalipa au usilipe but Arsenal inatakiwa kusajli no matter what tuna mapungufu mengi sana kuanzia Golini (Ramsdale anatakiwa apate ushindani) hadi wafungaji
 

Timu pekee unayoweza kusema imeimarika ni Newcastle kwa eddie howe ameichukua timu ikiwa inakaribia kushuka daraja kutoka kwa steve bruce now ipo champion league ,wewe unasema timu imeonyesha mafanikio kwa kuongoza ligi siku 248 kwa point 8 then siku 14 baadae imezidiwa kwa point 8
. Uefa mnaenda kushindana au kushiriki hapo ndo tatizooo linapoanzia , wewe binafsi tu as arsenal fan unahisi uefa mnafika hatua gani?
Usajili wa arsenal sasa huwa ni vichekesho zaidii utasikia wamemsajili takuma, sanogo, miyaichi, kallstrom na park chou young mavropanos , lokonga , tavares tukaambiwa ni young players wana potential
hawa wote wako wapi . Arsenal haijawahiii kuwa serious kwenye kitu chochote
 

Suala si la city kuwa timu bora hapa ni kuwa 8 points ahead of city na zimebaki game 8 . Hatulalamiki arsenal kufungwa na city tunacholalamika ni game na soton home, game ya westham na liverpool wote hawa walicheza midweeks na arsenal alikua yupo rest tu. Its not only this season fuatilia 2007, 2013,2016 ujue hii arsenal hakuna ilichobadilika hata kwa wenger ilikua inacheza pasi kibao kama hivi lakini mafanikio sifurii. Kuna game arsenal ilitakiwa ishinde pale emirates vs Brighton ili iwe top 4 lakini ilipigwa
vipi this season nayo Brighton hajafanya kama alivyofanya kipindi kile!!
Arteta akamzingua guendozi dogo yule akatuletea lokonga . Arsenal ni special list in failure kuikibali kushabikia ni kukubali kuwa failure
 
Mbona hujaraja martnelli, martin, saliba nk? Arsenal inahitaji nyongeza kidogo sana kutoboa
 
Mbona hujaraja martnelli, martin, saliba nk? Arsenal inahitaji nyongeza kidogo sana kutoboa

Arsenal haitakaa itoboee mkuu hii!!. Kwa chance ilizopata ni mwendawazimu pekee atasema arsenal itabeba ubingwa.Bora dortmund yeye mwaka 2012 amechukua kuliko arsenal 20 years!!
 
Arsenal haitakaa itoboee mkuu hii!!. Kwa chance ilizopata ni mwendawazimu pekee atasema arsenal itabeba ubingwa.Bora dortmund yeye mwaka 2012 amechukua kuliko arsenal 20 years!!
Watu wamekomaa na Liverpool Yao 30+ yrs sembuse sisi, poa tu. Mm nimeipenda Arsenal kwa mapenzi, mengine ni changamoto tu, miaka Ile man city ni weak tungekuwa tumebeba ubingwa kwa points za mwaka huu!
 
Watu wamekomaa na Liverpool Yao 30+ yrs sembuse sisi, poa tu. Mm nimeipenda Arsenal kwa mapenzi, mengine ni changamoto tu, miaka Ile man city ni weak tungekuwa tumebeba ubingwa kwa points za mwaka huu!

Mwaka gani man city alikua weak?. Vipi 2016 timu kibao zilikua weak ikabaki nyinyi na Leicester mlibeba nini?
Husifananishe liverpool na arsenal ziko mbaliii kweli ni ardhi na mbingu . Liverpool 2005 kacheza uefa final kabeba , 2017/2018 ni finalist na 2018/2019 kachukua uefa na 2021/2022 kacheza final njoo kwa vituko arsenal mara ya mwisho kufika tu robo fainali ilikua 2008
ndo hatua kubwa iliyofika ukitoa final ya 2006. Hapo kuna mfanano kwelii yani mwenzako kaingia na kubeba kombe la mabingwa na kacheza final kibao unamfananisha na Arsenal. Mafanikio yake ilikua quater final
 
Watu wamekomaa na Liverpool Yao 30+ yrs sembuse sisi, poa tu. Mm nimeipenda Arsenal kwa mapenzi, mengine ni changamoto tu, miaka Ile man city ni weak tungekuwa tumebeba ubingwa kwa points za mwaka huu!

Kimbia huko toka arsenal huko utakufa na msongo wa mawazo. Wewe unadhani wakina aroon arsenal, khamiiss hawataki kujitokeza humu wanapenda ? Hapana wakija humu wataonekana vituko. Mwanetu aroon alikua hazipiti dakika kapost mara ooh jesus kafanyeje mazoezini sijuii arteta kafanya nini . Leo jezi imetoka mpya lakini kajificha huko ndani
hataki hata kutuletea uzi tuone ulivyo mkali. Uzi umetengenezwa kupitia recycle bottles. ARSENAL THE BOTTLERS
 
Mimi siwezi kuhama timu, hama wewe ila usinilazimishie akili za Manara, once a gunner always a Gunner! Hamia man city mkuu ukale Raha! Kupanga ni kuchagua! Kuna watu ni mashabiki wa Newcastle kufa (Including JK) their highest performance in 40yrs ni Kumaliza no 2 mwaka 1995, Leo hii wanarudi UCL kwa Kumaliza top 4! Nimeridhika na Arsenal yangu, USINILAZIMISHE MKUU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…