Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal boss Mikel Arteta:


"I am a very methodical, routine person. When we are winning, I don't like to change my clothes, I like to maintain exactly the same jumper, trousers and shoes as before. If we lose, I change to something different."View attachment 2536357
 
Sawa mkuu. Ahsante kwa ufafanuzi
 
Carragher juu ya biashara kati ya Arsenal na Man City!

Carragher
" Manchester City hawatarudia kuwauzia Arsenal Wachezaji, Zinchenko kuuzwa Arsenal ilikuwa ni biashara ya kirafiki baina ya Pep Guardiola na Mikel Arteta!

Pep alijua Arsenal watakuwa wakawaida tu hakujua anatengeneza Arsenal kuwa tishio kwake".

Jamie Carragher mchezaji wa zamani wa Liverpool!
 
Zinny kwenye hii picha alikuwa na options kibao za pasi daaah. Angemuona Martinelli na kumpa reverse pass, kuna Ode sijui hapo kati karibu na Saka, kuna mtu free kule namba 11...hiyo pass Kwa Saka tena inaonekana ndiyo ilikuwa pass ngumu Kwa sababu ya positions za mabeki ila ndiyo hivyo tena.....Kambaaaaa
 
Sijajua kwa nin mawazo yangu yalikuwa sana kwa caicedo kuliko yalivo kwa rice, nahisi itakuwa mahaba tu
 
Sijajua kwa nin mawazo yangu yalikuwa sana kwa caicedo kuliko yalivo kwa rice, nahisi itakuwa mahaba tu
Mchezaji kusaini mkataba ni formalities tu na haimaanishi hataki kuhama. Usupumbazwe na hili. Caecedo kasaini mktaba ili awe kwenye safe side. Inaweza kuwa terms mpya za mkataba zinamnufaisha yeye akiendelea kuwa Brighton au akiuzwa. Huo ndio mpango kamili. For me Caicedo ni mzuri kuliko D Rice
 
CF sio striker wala no. 9. Huwa watu wanaconfuse sana. CF ni kiungo mshambuliaji anawewalisha mipira striker au wingas. Hii ndio maana halisi ya center forward. Hii inafaa zaidi kumuita CAM
 
kabisa aseeee caicedo kwangu ni bora zaidi ya rice
 
Lakini tambua tayari ni ngumu kumtoa hapo

Kama January hii walimbania kuondoka , na Sasa kajitia kitanzi ,sio rahisi kuuzwa kwa hivi karibuni


Nimeona taarifa nyingi timu zimeanza kupigana vikumbo kwa Rice , maana Bellingham haieleweki anaenda Madrid au Liverpool wataweza kumpata
 
Overview yake hii hapa

Hapo Kuna Overload Kuna Positional play

Wachezaji 6 wameenda kushambulia

Kuna mbadilishano wa position

Zinny amekuwa no.10 kuungana na Odegaard

Saka kaingia kwenye box kuchukua nafasi ya Trossard

Martinell kachukua nafasi ya saka

Trossard kachukua nafasi ya Martinell

Beki wa Everton Mykolenko na wenzie walikuwa wana mtarget saka na Martinell

Baada ya position play walichanganyikiwa wasijue wamkabe nani
 
Huyu mjinga huyu kama Douglas Luiz tu, angetulia akalinda kiwango summer tungeweza rudi ila ndo atazeekea hapo kama Richarlison.
 
Wachezaji wote wazuri, wachanga kama Caicedo ni wagumu kumtoa lazima ukavunje benki wacheni ubahili ndugu. Hizi timu kama Brighton ubingwa wao na trophoies zao ni kununua wachezaji na kuwauza kwa bei nzuri. Mchezo unaochezwa kwa Caicedo ndio huo. Kumpa Caicedo mkataba mpya na motisha nzuri ni kama kumpoza ili acheze kwa moyo maana aliashavunjika moyo kuzuiliwa kwenda Arsenal au Chelsea ambapo aliamini kule angebeba makombe, angelipwa vizuri na jina lake lingepaa zaidi. Hata Enzo walikuwa wanajiandaa kumfanyia hivyo hivyo kama asingeuzwa wangempa mshahara bora zaidi na mkataba wenye motisha zaidi. Mimi sioni kama Caicedo au Brighton wamefanya kitu kipya hapo. Mkimtaka Caicedo Summer mtamchukua tu ila sio kwa bei rahisi kihivyo
 
Ebwana eeh hii ndiyo najua hapa kwamba CF ni AM.
AM ni general, anaweza kutokea pembeni kama winga hasa zile formations ambazo hazitumii winga ndio wale wa pembeni wanaitwa AM. CF anaweza kuwa AM lakini sio kila AM ni CF. Jina zuri la CF ni CAM

CF kama neno linavyosema lazima atokee katikati
Mfano kwenye 4-2-3-1 ambayo Potter anaitumia sana CF ni Felix ambaye anatokea katikatiu kuwalisha mipira hasa no. 9 ikishindikana anawapa mipira winga ili attack itokee pembeni
 
Najitaid kusoma na kurudia mara kwa mara nakua mgumu kuelewa hili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…