Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Tumeipenda wenyewe acha ituumize naona sasa hivi tunapiga hesabu ya kiporo.
 
Awapumzishe akina nani??
Utajikuta relegation zone brother.
 
lembu eti kwamba unaona newcastle ndio inamchallenge zaidi arsenal kuliko city?!!

Ulikuwa unawajaza ujinga hawa ndugu zako.
 
Bado huwezi kukata tamaa ya Ubingwa eti kisa tumefungwa na Man City, mbona na yeye aliweza kupoteza dhidi ya Spurs, Liverpool, Man Utd ambao sisi tumeweza kuwafunga?
Man City kapoteza michezo 3 sawa na Arsenal na still ametuzidi mchezo mmoja zaidi.

Kuna mdau humu, alishauri tuongeze experienced striker mmoja pale mbele kuweza kuwa challenge Man City na wapinzani wetu wengine pamoja na kupata depth ya kikosi, lakini wenye timu hawakuona umuhimu. Sisi hatukuwa na nafasi ya kufanya chochote as hakuna anayetoa hela zake mfukoni kununua wachezaji na kulipia mishahara zaidi ya wenye timu.

Bado naamini ni mapema sana kukata tamaa, fanyeni ulinganifu wa Arsenal ya mwaka jana ilipocheza michezo 22 ilikuwa na alama ngapi kulinganisha na Arsenal ya mwaka huu iliyocheza michezo 22 sasa ina alama ngapi?

Iwapo tutajipanga bado tuna nafasi ya kushinda EPL, ligi bado hii Wakuu💪

COYGs
 
Mechi 8
Gape 15
Na bado wakakosa ubingwa


Bora niendelee kushabikia WAZEE fc ya ujiji sasa

Note
Wazee fc ya ujiji mchezaji mwenye umri mdogo kabisa ni kipa ana miaka 56
Ila hii tunu haijawai kupoteza mechi yoyote toka 2010 mpaka jana wamemchapa mwandiga fc goli 4
 
Arsenal Fans sioni sababu za kukata tamaa, kwasababu Arsenal bado ana nafasi nzuri zaidi kuliko Man city kuchukua ubingwa kama wakiwa serious na wakiacha papara na utoto. Ingawaje ni kazi ya ziada inahitajika na wala si ya kitoto. Through game moja mkononi na kurudi kwa Gabriel Jesus naimani kitaongeza kitu kuanzia dressing room mpaka uwanjani. Wachezaji kama Eddie Nketiah, Reiss Nelson na Folarin Balogun si wachezaji wakuja kuibadilisha Arsenal kule mbele hata wawepo kwenye form gani. Ni aina ya wachezaji potential ku-generate fund kwenye timu Kutafuta wachezaji wazuri ambao determination yao ipo juu. Hata huyo Balogun anaonekana kuwika huko ufaransa huu ndio wakati Arsenal kupiga pesa kuachana na nao. Hizi mishe za kitoto za kuwaamini hawa consistently - immaturity player ndio huwa zinakuja kuigharimu Arsenal kila siku..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…