Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Mkuu unaongeleaje game zetu 8 zijazo maana game 2 katika zile 10 tushaziona zilivokuwa
 
Nadhani kocha wa arsenal amekosa plan B,ukiangalia aina ya kikosi anachokichezesha hakibadiliki na nirahisi sanaa timu pinzani kwa sasaa kuwasoma wachezaji maana ni round ya pili imeingia.
Mchezaji aliewafungia goli anapaswa kuanza,badala ya kutokea bench,hivi vitoto aanze kuvipumzisha,vitakata pumzi mapema wakati bado wana mechi ngumu mbeleni.
Amedondosha point 5 kwa mechi 2,asipoangalia anaweza kushuka ghafla kutokana na mwendo huu.
Hizo sajili walizofanya mbona hatuoni wakitumika,au hawaamini?
Poleni mashabiki wa arsenal,Ila kama mna platform ya kumfikia kocha mwambieni ajitafakari,hawa kina benn,martinel,saka,saliba aanze kawafanyia rotation.
 
Nilijaribu kusema kuhusu aina ya magoli tunayoruhusu tangu ungwe ya pili imeanza na ndio goli tuliloruhusu na leo pia, wakuu walisema sio set pieces lakini tunaendelea kuangusha points kwa aina iyo ya magoli
 
Mkuu unaongeleaje game zetu 8 zijazo maana game 2 katika zile 10 tushaziona zilivokuwa
Binafsi nadhani ni muda sasa kocha aanze kufanya rotation ya kikosi, timu pinzani wameshatujulia maana wachezaji ni walewale tu kila mechi

Toa White weka Tomiyasu aanze
Toa Martinelli Trossard aanze au kama vipi Nketiah apishe pale kati Martinelli acheze hapo

Si tunasema tuna Versatile players? Ndio muda huu tuone iyo versatility la sivyo tutakuja kutukanana humu sio muda mrefu
 
Hii ni picha ya dada mla mayai punde tu baada ya kutoka kuangalia game ya Arsenyani vs Brentford.
 
Makocha wa EPL washamsoma Arteta wanachofanya sasa hivi ni wanapita kwa kudesa mle mle kwa Everton kazi mnayo mjiandae kisaikolojia. Sema kisingizio mnacho mlisema ubingwa sio malengo yenu malengo yenu top 4

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…