mbati nenga
JF-Expert Member
- Feb 18, 2017
- 276
- 348
Kazi ya shabiki ni kushangilia na kukosoa sio kujitia wewe ni mtaalam wa ufundi wa benchi la arsenal..Sasa hivi kuna baadhi ya mashabiki wa Arsenal humu ndani mmeanza kua matured na kuanza kujielewa, tatizo kuna mashabiki wengi humu hua hawapendi kabisa kusikia jambo lolote negative kuhusu wachezaji, kocha na timu yote kwa ujumla.
Wao muda wote wanataka kusikia mambo matamu tu na shabiki anaejielewa akijaribu kuzungumza kuhusu uhalisia wa mambo anaanza kushambuliwa kwa matusi, kebehi na kejeli na kuonekana ni mamluki.
Ukienda kwenye majukwaa ya Chelsea, Man United na Liverpool unaona jinsi mashabiki wake walivyo huru kukosoa iwe ni mchezaji, kocha au timu kwa ujumla pasi na kushambuliwa na mashabiki wenzake.
Timu inapopata matokeo mazuri shangilia inapopata matokeo mabaya kosoa..
Sasa unakuta mtu yeye matokeo mazuri anakosoa matokeo mabaya anakosoa utadhan umu ndani kuna arteta ama edu.