Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Kwa dakika chache nilizomuona mudry nakubali kabisa ni mchezaji mzuri ambae kuna uwezekano wa kuja kuwa bora mbele ya safari, tulikuwa sahihi kutoa pesa ile kama Anthony wa man u alitolewa mzigo wa 100, basi mudryk ni zaidi.
Jamaa hana mguu wa kupandia kitandani yote ni ya kuchezea mpira, kushoto anatumia, kulia anatumia...
Angetufaa saana arsenal ila ndio hivyo, anaweza akawa ana shine kwa mpinzani wetu.
2nd leg nahisi atatusumbua kinooma.

Kuhusu camavinga naona ni usajili mzuri, dogo kwa xhaka nahisi anaweza kufanya vizuri zaidi ya xhaka.
 
Game ya kwanza OT ,Zinny hakuanza ,Partey hakuwepo kabisa ,

Hawa ndio wanaunda mfumo wetu wakuzuia Kaunta kwa zile timu zisizoweza kumiliki mpira na kutegemea kaunta

Leo watakuwepo

View attachment 2491010
Sawa sawa mkuu naomba tu leo usikimbie tuna kupenda sana uwe hapa baadae kutupa maoni yako na uchambuzi wako.
 
Antony Man U wameliwa mchana kweupe
 
Ndg wana gunners

Kwa heshima na tahadhima napenda kutoa PONGEZI za dhati sana kwa klabu ya Arsenal na mashabiki wake wote na sera yake ile pendwa ya kutoingia kwenye bidding war na timu zingine wakati wa kumnunua mchezaji. Hiyo sera sisi Chelsea tumekuwa wanufaika wakubwa sana na tunaomba kwa mwenyezi Mungu hiyo sera idumu milele na milele.

Jana mlimuona kijana anawatapisha Nyongo akina Milner, Gomez na wenzake. Hata akina Galagher na Chunkuemeka kidogo watapishwe nyongo kwa sababu ya pasi za haraka haraka.

Huyu dogo amekuja kutuondolea ubishi tuliokuwa nao kwamba eti tuna wachezaji class.

Sasa hata pasi za Mudryk hawawezi kupokea, ni Ziyech tu naona wataendana naye.

Kwa hiyo tunatangaza rasmi sasa Ziyech not for sale.

Ujenzi huu wa timu sasa utajengwa chini ya msingi ambaye ni Mudryk, the next Messi and Chelsea Messiah.

Tukimaliza kumsajili RB na viungo wawili, tutazindua rasmi Chelsea kurudi kwenye ligi, sasa hivi tumewaachia tu turekebisha masuala yetu ya ndani.

Kwa heshima nyingi narudia tena kusema asanteni sana majirani zetu, mlichokifanya hakitasahaulika pale darajani.

London is Blues and Blue forever.
 
Dah haya bhana
 
Huyu ni media za UK zinatufanya tuonekane tunamtaka, ila siamini kama tunamtaka.

Kama kweli tungekuwa tunamtaka tungekuwa hata hii january tushapeleka ofa.

Huwez sema unamtaka mchezaj flani wakat ukipeleka ofa unapeleka ofa kwa wachezaj wengine (Caicedo na Enzo)
Ukiangalia Caicedo na Enzo wote wanamiaka 21&22 respectively

Wakala wake anataka kutumia njia ya shakhtar,
huyu ni kama option ya mwisho baada ya priority zetu kukwama.
 

Ukimtaka sasa hivi na ukitamka baada ya kuwa amemaliza mkataba Malipo yanatofautiana.
Ukimgusa sasa hivi lazima uvunje benki
 
Ukimtaka sasa hivi na ukitamka baada ya kuwa amemaliza mkataba Malipo yanatofautiana.
Ukimgusa sasa hivi lazima uvunje benki
Rice bado anamkataba na West Ham, nahis mwaka 1 na nusu umebaki

kama kweli ni top priority why tubid 86M kwa enzo na 65M Kwa Caicedo?

Ni media na agent wake wanatahusisha nae na siamini kama chelsea kweli tunamtaka,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…