Arsenal (The Gunners) | Special Thread

The club is looking to add 1-2 players in January: A wide player and a DM on the agenda.
The board won't panic and won't be affected by Jesus's injury.

Hizi kauli za kiburi ndio zinatukwamisha, eti won't be affected!!! As if haikujulikana kwamba Hana sub ya kueleweka. hapa napo watasubiri mpaka Saka au Gabriel aumie ndio watafute LCB na RW!!

Hii timu ipo kwenye trajectory nzuri ila wakijichanganya hili dirisha sio tu tutapoteza top 4 ila tusahau kuingia UCL milele maana Newcastle will be serious contenders next season and ahead.
 
Mkuu Tafiti kibao zinaonyesha injuries ukubwani zinahusika na game management kwenye youth set up.

Kingine hakuna mchezaji anazaliwa injury prone ila mazoezi, mechi anazocheza na fatigue zinaweza affect miguu au misuli yake in the long run.

So unaweza sema Saka sio injury prone ila hata Wilshere hakua injury prone ila baada ya kucheza mechi kibao below 20 ikaja ku catch up naye ukubwani.

Ukiona Ansi Fati hachezi Kila mechi sio sababu Hana umuhimu ila Wanaenda naye taratibu otherwise yatamkuta ya umtiti, Allen Halilovic au Nabil Fekir!!
 
Sawa nitarudi hapa in a few years time tuki assess what went wrong with Saka!!
 
Mkuu fuatilia vizuri, lisandro Martinez mbona anafahamika tokea ananunuliwa akiwa na Alvarez wa mexico kureplace de light na de jong Wala sio sababu ya scouting ya arsenal.

2. Atletico ipaki basi ikicheza na Getafe au Almeria? Kuwa serious kupaki basi ni UCL pekee ila La Liga haijawahi kupaki basi maana inacheza na vitimu vidogo so vinakaba tu na kutegea counter. Formation ya Atleti La Liga ni 3-1-4-2 Sasa hapo inapaki vipi basi? Unajua msimu 2020/21 wa ubingwa Atletico walifunga magoli mengi kuliko Real Madrid!!!

3. Gomez wa Anderlecht anafahamika sana tu alikua potential replacement ya Tagliafico Ajax. We kutokujua wachezaji kusikupe upofu hata huyo Danilo mnamjadili humu ni level ya Lokonga lakini Kuna watu mna matumaini eti ndio mrithi wa Partey?? Are we serious??

4. Pepe alikua a good player ila sio level ya EPL whether kocha ana say au lah unadhani Murdyk ndio solution?? Yule ni level za timu kama Brighton zinazo tegea counter sio Arsenal more over kwa 70M!!! Mtakula.

5. Mnadai hamsajili kwa mihemko Sasa mlipata Nini last season kwa kiburi hiko? Mlitucost tu UCL position na msimu huu pia jeuri hii hii itatunyonga Tena. Why don't we learn from mistakes??
 
Mimi nakushauri Tena kawekeze majukwaa ya siasa ,

Arsenal walishasema na. Wamekuwa wakirudia kupitia Arteta hawawezi kusajiri Tena mchezaji ilimradi tu , walipomkosa Raphina na Neto ,option ilikuwa Ni kwenda January kuangalia option nyingine ambayo Ni Winger anayecheza both flanks ,kumbuka hapo pia Kuna Smith Rowe anacheza LW na no.10 ,Kuna Fabio Vieira anacheza No.10 na kwa Xhaka .

Jesus anacheza both flanks ,

Kwenye backline Bado utaratibu Ni ule ule ,Hakuna Mapungufu Kama unavyodai

Kwanza tambua model ya Arsenal Sasa Ni kusajiri Versatile Players ,

Arsenal Ina mabeki wakati WHITE , GABRIEL, HOLDING,SALIBA ,

katika hao White anacheza RCB na RB , SALIBA pia anacheza RB apart from RCB .


Kuna Tomiyasu Huyu anacheza LCB,RB,LB,RCB,

Kuna Kieran Tierney na Zinchenko Hawa wanacheza LB ,lakini ukitaka au Ukibanwa kabisa kwenye kiungo ,Zinny anacheza CM, NA AM. ,


Nakushangaa unaposema Aletwe beki mwingine Wakati kipaumbele Ni WIDE FORWARD ambaye utaratibu Ni ule ule awe anacheza flanks zote mbili, rejea Kwanini alitakiwa Raphina ,Neto .


Murdky anacheza LW na RW na Ni goalscoring player,

Unapomleta Huyu unauhakika wakumtumia LW au RW , Kumbuka hapo Kuna Smith Rowe ambaye Ni hatari akicheza LW (inverted winger) .

Martinelli anaweza pia kucheza Kama False 9 .Hata Tite amesema Kuumia kwa Jesus ,Martinell atamtumia pia Kama False 9.


Depth ya Timu Sio kujaza wachezaji wengi wasio na msaada ,ndio maana HUWA nauliza Kama kuwa na wachezaji ,Basi Pepe angebaki Kama backup ,kwa kiwango Cha Pepe Ni backup kabisa nzuri, ila mwalimu kashasema Anataka mchezaji wakuingia na kutoa A performance.
 
mwambie hamis77 hizi kinda za Academy bado hazijakaza vizuri mifupa, hivi zinavyopelekewa moto kila siku lazima zitapata matege.
 
Tatizo uko emotional Sasa niambie Formation ya Atletico La Liga ni ipi? Na Hilo basi wanapaki kwenye mechi zipi? EPL fanboys you know nothing outside EPL no wonder mtu humu kadai eti Lisandro Martinez alikua hajulikani before arsenal scouts kumuona!!!

The formation is 3-1-4-2 with Koke ambaye sio DM ndio deepest player na hiki ndio kilimtoa Partey Atletico maana midfield walikuepo Torreira, Partey, Saul, Herrera, Koke ila anacheza Koke peke yake!! Wengine wote ni attacking players say Felix,Lemar, Llorente, Suarez, Correa etc Sasa basi Gani hapo utapaki!!!

2. Unasifia sana sajili ila zinchenko mljua ni injury prone huku sub yake Tierney naye Yuko kitandani but u still bought him madhara yake umeona? Hapo Bado Midfield mkamsifia Lokonga weee Yako wapi Sasa? Mbona mmekiri kuwa DM kuna udhaifu? Vipi Vieira ana lolote la maana Toka amesajiliwa kwa 40M? Au Bado Bado hamjakubali ni average?

Arsenal in potential nzuri ila tushukuru hatuna majeruhi otherwise we'll be exposed badly na kama hawatasijili depth eti kisa panic buys sijui future-oriented tutarudi hapa mkilialia kumaliza nafasi ya 8.
 
Lisandro ulimfahamu Kama Ni mchezaji mzuri ? Kwenda Ajax ,Ni timu gan kubwa zilipigana vikumbo?

Unajua hata Arsenal walikuwa wanamfatilia wao pekee kabla Man u hawajaingia mwishoni?

Unasema Arsenal ilikukost kwenda UCL

Kwanza Nan alikuambia Arsenal mwaka Jana malengo ilikuwa kurudi UCL ?nyie sindio mlisema inashuka daraja?

Mpira Ni project na process Sio zima Moto


Malengo ya Arsenal mwaka Jana ilikuwa kuingia Top 6 ,Arteta aka achieve more akawa namba 5,

Akaitwa ofisini akapewa mkataba mpya


Unasema Danilo Ni sawa na lokonga , kwa skauti gani umefanya ?Arsenal wameanza kumfatilia Danilo na kutuma Skauti toka mwaka Jana .


Wewe upo bongo unasema Wa kawaida


Watu wanalipwa wamekuwa wakienda kumfatilia Murdky Ukraine kila mechi , wewe umemuangalia YouTube unasema mbovu kisa unamtaka Joao Felix


Kocha hawez kusajiri kwa matakwa ya mashabiki , klabu zinazojielewa zimeshatoka huko
 
mwambie hamis77 hizi kinda za Academy bado hazijakaza vizuri mifupa, hivi zinavyopelekewa moto kila siku lazima zitapata matege.
Shida ya mashabiki maandazi Wana wachezaji wao wa mfukoni ,wanataka waje kwenye timu ,hawajui hata timu inachezaje ,Sio kila mchezaji mzuri anacheza popote ,Hasa kwahawa morden coaches


World class wangapi wamekuja man u kwa matakwa ya mabosi na Sio makocha ,wameishia wapi?
 

Bado narudia kawekeze kwenye siasa ,Mliponda project ya Arteta ,akianza na Hawa watoto ,leo mnaleta ujuaji kutaka alete wachezaji wenu wa mfukoni Kitu ambacho hawezi kumskiliza mtu,

Alifanikiwa kufukuza kina Auba ,Ozil n.k makelele yakawa Mengi ,mkatulia


Huyo Atletico unayetaka kutudanganya ana possess Mpira sijui Ni wa wap

Atletico Ni timu ya 7 laliga kwa umiliki wa mpira


Partey Aliondoka Atletico sababu kuu Kwanza Ni Arsenal fans ,pili maslahi , Atletico walikuwa wanamlipa 65k pound ,Arsenal analipwa 200k pound .

Hiyo unayosema wewe Ni UZUSHI tu.


Zinchenko Ni injury prone ,mwenye uwezo mzuri tu, na Sio mara zote chance ya yeye na KT wanakuwa majeruhi

Habari njema Sasa LB Ni Zinny anakuja Tomiyasu ndipo nafata KT,


Unaponda Sajiri ya Fabio Vieira ,ambaye hakuwa na pre season , alikuwa injury, bado mechi alizocheza kafunga na ku assist ,na ana miaka 21 tu ,anacheza nafasi karibu 3, RW,LW na AM .

Kama hujui mechi ya mwisho alicheza role ya XHAKA akapika Goli .
Au mwenzetu tayari Unataka useme Ni mchezaji mbaya ?


Hii inaonesha jinsi gani humfatilii Arsenal ,

Uliikimbia ,now inatembea unadhan Ni Fluke , it's project and process
 
Narudia Tena usiongozwe na hisia, LCB ukimuweka tomiyasu nani acheze RB?? Utasema white ambaye huyo huyo umesema ni RCB. Sasa FA cup, UEL, na ligi zikichanganya huku Gabriel akiwa mgonjwa Ina maana Tomiyasu atacheza Kila siku (Either RB or LCB as you suggest)??

Pepe aliondolewa sababu Marquinhos na Nelson walikuwepo otherwise wasingemtoa mkopo bila "depth" in RW.

Funny enough January ulisema maneno haya haya kipindi tunalilia replacement ya Auba. Yakwapi mbona ukarudi kulalamika Tena msimu ulipoisha!!! Punguza hisia kwenye ukweli ushaambiwa Jesus kaumia eti Martinelli!!! Wakati huo LW acheze nani ESR ambaye Hana mechi Toka msimu umeanza??

Kwa fanbase ya aina hii no wonder hatujafika UCL mwaka wa 7 Sasa
 
anamtaka Joao Felix, aliambiwa anafiti kwenye mipango ya kocha?

Huo upuuzi wa kusajiri ilimradi mchezaji mzuri hata man u wameanza kuuacha ,

Chelsea wametumia £300m lakin kikos dhaifu ,sababu Kuna wachezaji mule walikuwa wanasajiri bila kujua wanacheza style gani .
 
Mkuu nisiseme sana ila tutarudi hapa February ukikiri kuwa Lokonga is better than Danilo. Hao scouts unaowasifia si ndio walimleta Vieira ana lipi la ajabu? Walimleta Lokonga ana msaada Gani? Hao scouts mnawasifia sababu ya matokeo mazuri ila kuanzia March timu ilianza kupigwa sababu ya kikosi kidogo na obvious injuries kwa Partey, zinchenko na Tierney mtarudi hapa kulia Lia Tena kama msimu uliopita.

2. Kocha hasajili kwa matakwa ya mashabiki yes but depth sio takwa la washabiki ila takwa la kikosi. Ni mjinga pekee angekubali kuanza msimu bila DM wa kueleweka. Kesi ya Partey ikitolewa hukumu mtaanza Tena panic kutafuta replacement na dirisha limefungwa tutajikuta msimu wote tunacheza na Midfield pair ya Danilo/Lokonga alafu ndio unadhani inatosha kubeba ubingwa??
 
Mfumo Gani? Kwani Felix utamlinganisha na nani hapo Arsenal? He's better than Martinelli and Saka akija arsenal anaweza cheza nafasi ya Jesus, Odegaard au Saka or Martinelli Sasa mfumo Gani huo unique wa arsenal asicheze??

Mnasema washabiki uchwara, Sasa wwe hapo Murdyk au Danilo unamjua au ndio akitajwa tu na tabloids za arsenal unaunga mkono hoja? Kila mtu anajua Danilo is average ila ni humu JF tu mnamkuza sana kuliko uhalisia.

I remember ulidai Lokonga eti ni understudy wa Partey na sifa kibao Leo utasemaje?? You should be the last person kutoa maoni kwenye technical aspects za wachezaji
 

Wewe kajikite kwenye Siasa

White Maga wamecheza Kama RcB na LCB , Bado Kuna option ya kuwatumia Saliba na white

Unapiga ramli Nan acheze RB?

HUJUI Arsenal msimu huu RB anacheza white , na alhamis Anacheza Tomiyasu as RB ,

Kabla hata LCB hujamfikilia Kuna Partnership ya Saliba White ,White magalhaes, White Holding , Saliba Magalhaes


Nani alimlilia Auba ? Baada ya Auba kufurumushwa Kwanza ndio Arsenal ilishinda mechi nyingi na Kufunga Sana ,

Kawekeze kwenye Siasa huku kwenye Soka unatia Aibu, Kwanza most of Arsenal fans walitaka Auba aondolewe , Huyo aliyemlilia utakuwa wewe.

ESR kukosa mechi ndio hawez kucheza? Kwanza ESR amecheza msimu huu mechi za awali, na ameshaanza full training

Wewe hao wachezaji wako wa mfukoni ,Hawawez kuja Arsenal

Kuna wenzako humu walimtaka Onana over Ramsdale, Emerson Royal over Tomiyasu, Buendia over Øde,

Mwisho walitulia ,na wewe utatulia
 
Hoja hapa ilikua msimu ambao Atletico imebeba La Liga Sasa hizo current stats za Nini? Nani asiyejua Felix msimu huu hachezi? Ndio maana nikakwambia season 202/21 ambako formation ilibadilika from 4-4-2 kuwa 3-1-4-2 Walifunga magoli mengi as much as Real Madrid Sasa unachobisha ni Nini? Huyo Murdyk Yuko proven kwenye lipi so far kiasi he's better than Felix?!

2. Hayo ya maslahi akikwambia wapi? Angalia dakika alizokua anacheza Tomas Atletico linganisha na za Rodri na Saul na Koke!!! Alikua Hana namba Atletico sijui unaleta ujuaji wa Nini hapa. Nimeshakuambia hata Torreira alipokuja hakucheza kabisa same to Kondogbia sababu formation ilihitaji CM mmoja tu wengine wote ni Attackers kwenye flanks.

Ngoja nifukue hapa post zako za January alafu ujitafakari kama unaongozwaga na hisia au objectivity.
 

Huyo Felix tafuta timu yako akacheze, wachezaji wangapi wazuri kuliko Huyo Felix , wameenda timu nzuri wanafeli sababu ya mifumo?

Huyo Felix ,World cup anafanya Nini Cha maana kuliko kina Saka?


Unamponda Vieira ,sababu hujui mpira , Vieira Ni potential na kila alipopewa nafasi alionesha uwezo regardnes Hakuwa na pre season na alikuwa injury muda mrefu .

Mechi ya mwisho katoa msaada mkubwa timu imeshinda ,wewe unaleta Siasa humu


Danilo anasajiriwa Kama mbadala wa Partey wa muda mrefu

Lokonga Kwanza sio backup ya Partey anacheza hapo sababu Elneny aliumia

Kama..una fikiria lokonga ni Backup ya Partey Ni umefeli

Kocha alisema Lokonga Ni potential na wanamkoch Kama no.8 advanced

DM Ni Partey na Elneny ,
 
kumbe nyie Wacongoman mmetimiza miaka 7 bila kushiriki UEFA.
Yaani mtoto anaanza darasa la 1 mpk anamaliza primary timu haijakanyaga kwenye michuano ya wanaume?
Halafu wakishauriwa wasajili wachezaji wa kutosheleza timu wanaleta janja janja ya Kroenke kua wao hawasajili ili mradi wasajili kumbe Mmarekani anabana matumizi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…