ARTETA NI MASTERCLASS kwenye Mbinu na Kiufundi.
Kuna namna Arsenal ya Arteta ime-perform beyond expectations (Inafanya vizuri kuliko matazamio ya wengi). Kuna namna Arsenal imeimarika mno. Sio kwenye uzuiaji, kumiliki mpira, kushambulia na hata namna inavyocheza dhidi ya timu zinazocheza kwa Low block (Rejea dhidi ya Chelsea na Wolves). Zamani Arsenal ilipata shida sana kuzifungua timu za namna hii. Tulilia sana kuhusu Creativity (Ubunifu) hasa kwenye Final Third.
Mwaka 2020 wakati Arteta anahojiwa kwenye PRESS moja alisema βAlihitaji sana kubadili mfumo kwenda 4-3-3 lakini kutokana na ukosefu wa wachezaji 5 mpaka 6 muhimu basi haweziβ
Arteta alibadili sana mifumo kulingana na wachezaji alionao na shortage ya ubora kikosini. Aliwahi kwenda na 4-1-2-1-2 huku Auba na Pepe/Laca wakiwa kama Double strikers, pia 4-2-3-1 huku Auba/Laca wakisimama kama Main target au 4-4-2 (Auba na Laca kama Double strikers). Kuna kipindi Arteta alitumia mpaka 3-4-3 yenye Hybrid shape huku Tierney akipanda kwenye Midfield iliku-push timu ingawa bado haikua msaada hasa kwa timu zilizo compact sana kwenye uzuiaji.
Arteta alikua na Vision lakini hakua na wachezaji. Arteta hakuwahi kuishiwa mbinu (Tactical) bali aliangushwa na ubora na aina ya wachezaji (Technical point of view).
Leo hii hatuimbi tena kuhusu Low block teams. Tunaimba kuhusu ubora wa Arsenal kwenye ku-press na kufanya Build up play. Tunaimba juu ya bora wa Arsenal kwenye ku-switch position, transition play (Defensive transition na Attacking transition). Leo hii tunaimba na ubora wa Arsenal kwenye Counter Attack. Na bado tutaimba sana.
Ubora wa Arsenal kwenye Counterpressing ni sawa na ule wa Liverpool wakiwa kwenye ubora wao. Ubora wa Arsenal kwenye Build up play ni sawa na ule wa City kwenye ubora wao. Ukubali au ukatae, Arsenal ni bora kiufundi na kimbinu kuliko Man City msimu huu. Subiri game yao pale Emirates. Kuna namna Arteta ananishangaza sana.
Man City wapo direct sana. Wanacheza direct football. Namna wanavyokushambulia unajua kabisa nini kinaenda kutokea. Lakini kwa Arsenal?β¦Vipi kuhusu Arsenal?β¦Unpredictable..! Huwezi kutabiri namna watakavyo kufungua. Namna wanavyokuja ni vingine kabisa na namna watakavyo kuadhibu. Nasubiri mechi kati ya Arsenal na City. Kama msimu uliopita Arsenal ili outplay City vipi kuhusu Msimu huu?
Arsenal inacheza 2-3-5 dhidi ya low block teams hasa ambazo ziko compact tena ambazo haziruhusu spaces za kushambuliwa kama Wolves na Chelsea. Nyuma Saliba, Gabriel. White, Partey na Zinny kwenye midfield ku-overload, Martinelli, Vieira, Γdegaard, Jesus na Saka kwenye Attacking. Kwanini usifunguke?
Kwenye Attacking phase, kuna muda Jesus alitokea pembeni kisha Vieira akiingia ndani kutokea Left [emoji23]. Asee tutaona mengi sana.
Uzuri nawakumbusha tu. Arteta anadai kuna mashimo sana pale Arsenal. Uwepo wa Γdegaard na Vieira kuna namna Arteta anataka uwepo wa Bernado na KDB wake.
Nitalipia gharama yoyote ile kutazama game bora msimu huu. Game ya kiufundi. Game ya kimbinu zaidi. Game itakayoamuliwa kwa ubora. Hata kama gharama yake ni kukosa kipindi chuoni. Nitaangalia.
Arsenal Vs City ni mechi ya msimu huu. Tukutane baada ya World Cup InshaβAllah.
#COYG