Ama kweli nimeamini ata iweje maji hayawezi kusahau Asili yake, ata yachemshwe kiasi gani yatarudia tu ubaridi...! Kuna ndugu yetu asharudi kwenye Default mode kama kawaida yake, Ashaanza hoja zake ambazo hazina kichwa wala miguu
Hivi kwani mchezaji Mkubwa anapimwa Kwa vigezo gani maana isije kuwa tunachanganya Kati ya mchezaji Mkubwa na mchezaji maarufu
Kwa Akili zangu tu za kuvukia barabara naamini kuwa Gabriel Jesus ni mchezaji Mkubwa kuliko Auba, naamini kuwa Bobby Firmino ni mchezaji Mkubwa kuliko Auba nk
Kama kuwa top scorer ndio kuwa mchezaji Mkubwa basi Auba ni wachezaji Mkubwa kuliko kina Tevez,Eden Hazard,Wayne Rooney,Ian Wright nk
Umuhimu wa Gabriel Jesus pale Arsenal ni mkubwa sana maana yeye Kwa sasa ndio anachange atmosphere ya dressing room,ameletea nguvu na hali ya kupambana,ameleta mentality ya upambanaji na ata akiwa anaongea wachezaji wenzie wanamskiliza maana ameshinda mataji kibao pale England kuliko wao, sasa sijui mchezaji atamskiliza Auba Kwa kipi?
Kwa tafsiri rahisi kabisa na isiyokuwa na makando kando Jesus ni mchezaji Mkubwa katika ligi ya England kutokana na contribution zake akiwa City, kuwa top scorer hilo linawezekana Kwa mchezaji yoyote Yule na kutoka team yoyote ile ktk ligi, ila kuwa mchezaji mkubwa sio rahisi kama kuwa top scorer