Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal ana Ratiba ngumu OCTOBER hawez kutoboa

WACHAMBUZI UCHWARA WA BONGO BHANA

Arsenal’s next six fixtures:

FK Bodø/Glimt A
Leeds A
PSV Eindhoven H
Southampton A
PSV Eindhoven A
Nottingham Forest H

#afc
Saa hii ndio ratiba ngumu haha unacheza na timu za mtaani uko ulaya ..eti timu inaitwa FK BODO ndo unaita hii ratiba ngumu hahahah🤣🤣🤣🤣 kweli hii arse8 bado timu ndogo sana.
 
Jumapili tupo away na Leeds yatupasa tukaze tushinde,naamini Liverpool atamkazia city pale Anfield,Inshalah 🙏🏾#coyg
Livakuku hii takataka?? Kwa wewe unaona kabisa utaweza shindana na city ama Chelsea? Kweli maskini akipata matacko ulia mbwata.
 
Sijui kwanini watu wanawachukulia Liverpool kiwepesi, labda sababu wapo 10th, binafsi naona mechi yetu dhidi ya Spurs hata kabla ya red card ilikuwa nyepesi kuliko mechi dhidi ya Liverpool. Mechi dhidi ya liverpool ilikuwa ON hadi dakika ya mwisho.

Kitu ambacho Klopp alistruggle dhidi ya Arsenal ni utengenezaji wa nafasi, liverpool walirecord the least XG ndani ya misimu miwili, forward hawakuwa na tatizo kwenye finishing, nafasi nyingi walitengeza kutoka deep lengo lilikuwa kuexploit Arsenal's high line kwa kumtegemea TAA/ henderson, baada ya kutoka TAA approach ya Mikel ilibadilika akajiamini zaidi kushambulia. So Liverpool si wepesi sababu wamefungwa na Arsenal, Liverpool si wepesi km Ollachuga unavyotuaminisha, wakiwa fully fit utahitaji kuwa organized mwanzo hadi mwisho ili kuwafunga.

Kama shabiki wa Liverpool unaiona hii Liverpool ni mbovu basi ujue tu Arsenal tushacheza Anfield na backline ya Sokratis, Bellerin, Mustafi, lichsteiner mzee kutoka Juve, kocha akiwa Unai emery, midfield kuna Guendouz, LT11, foward tukiwa na lacazette, benchi yupo Joe willock , Firmino anafinya anavyojisikia, Mo Salah anapiga anavyojisikia, ilikuwa inatia uchungu sana.
 
Mnaongoza ligi afu hampo CL sasa umuhimu wa kuongoza ligi uko wapi.? C bora muongoze kikundi cha akina mama cha kwaya.
 
Dear Arsenal Fans...👂

Naona Asilimia Kubwa Yetu tumetumia Wiki hizo Mbili Kumtupia Lawama GABRIEL MAGALHAES..

KWANZA KABISA Nakiri Hata mim Gabriel Amekuwa Beki mwenye Makosa mengi mno Ya Kujirudia na anahitaji Kurekebisha Pale Anapokosea ili awe Bora Zaidi.

Lakin Ukiangalia Mpira Kama Mtu Mwenye upeo utagundua Kwanza pale Arsenal Hakuna Namba 4 yaani beki anakaba Tough na Haogopi Kama Yeye..Yan Kwa kifupi Saliba White na Holding ni aina moja ya Mabeki no 5 yan wanausoma Mchezo na kuspweep na kupanga Team kwa ujumla

Ila Gabriel Yeye anatumwa kufanya kazi ndo maana mnaona Makosa yake Mara kwa mara ingawa sio lazima akosee..Leo Arsenal Wakicheza na Team Yeyote Kubwa mfano City Liverpool Spurs na Chelsea Bas Kaz Yote ya Hao Top Strikers Halaand Auba Kane na Kina Mitrovic mara nyingi ataifanya Gabriel..

Jaribu Kuvuta Picha Hakuna Goli bila makosa na Jaribu Kujiuliza Tena Huwa ukiangalia Mechi za Arsenal ni Beki gan anayeenda kwenye battle nyingi kuliko Gabriel tena Battle na world class Players...

Ukitumia Muda mwingi Kukimbizana Kukaba ni rahisi sana kufanya makosa ndo maana Ukiangalia Namba 5 weng wanaonekana Smart sana sababu muda mwingi wao wanasoma mchezo kuliko Kukaba..wanakaba mara chache sana na wao hutumia muda mwingi kichwani kuliko nguvu...

Gabriel ana nafasi kubwa tuu ya kupunguza makosa yake ila ni beki wetu Bora kwenye kukaba kwa mabeki wa kati..Labda kama Tomiyasu akija kucheza pale tuone atachezaje..Hawa wakina Holding wamekaa miaka yote wanawekwa Benchi mjue kuna sababu sio bure..

Nimejifunza sana Uvumilivu kupitia kwa Arteta,Xhaka na Baadhi Ya Wachezaji Wengi tuu ..
 
Livakuku msimu ulopita hajabeba point hata moja kwetu. (Ukiondoa zile finales) kwa sasa hii Livakuku ni takataka hamna timu pale adi ninyi arse8 munajipigia tu halafu ulikuwa “unapata uchungu?” Iv mwanaume na yeye anapataga uchungu? Halafu umeona jana tumemnywa Ac milan ..jipangeni sana moto unakuja. Taratiiibu hatuna haraka sisi
#CFC💙💙💙
 
Jumapili tupo away na Leeds yatupasa tukaze tushinde,naamini Liverpool atamkazia city pale Anfield,Inshalah 🙏🏾#coyg
Kila mtu ashinde mechi zake, ya Liverpool na Man city waachie wenyewe
Naona mwaka huu mko serious na Ubingwa
Msije tu mkamtukana mamba wakati ligi bado mbichi sana
Safari ni ndefu mno
League contenders bado wako wengi
January ndio itajulikana kama contenders ni wawili au watatu
Mkliwemo kwenye list January basi, Arteta ni mwanaume tena mbabe
 
Alibeba point, labda kama ulimaanisha point 3
 
Gabriel huyo ni beki hatari sana, hajui namna ya kufanya clean tackle. Kusababisha penalty ni jambo la kawaida kwake
Mimi nawashangaa wanaokuja na dhana ya kumsupport, yule hatabadilika kwa style yake ya uchezaji
Yuko too much physical na hayuko tactical kwenye kukaba. Akiwa peke yake ni mchezaji mzuri ila kwenye kutackle ni dangerous. Kama mna mwingine hapo mwekeni tu. Akikutana na timu inayofanya mashabulizi sana, atatoa penalty kibao na red card juu
 
Kuanzia msimu wa 2024/25 UEFA itakuwa inatumia coeficient factor kushiriki UEFA, hii ya top 4 itakuwa haina kazi tena
So timu zenye coefficient ndogo mtaisikia UEFA kwenye redio tu
 
Poa. Ingawa sijaweza kuangalia games season hii ila nikitumia uzoefu wa previous seasons, sijawahi kuwa na tatizo na Garbriel. Alitusaidia sana kupunguza magoli ya kufungwa. Labda fans wanaona jinsi Sasa tumeongeza kufunga kuliko last season maana Kuna Gabriel wawili kule mbele wanakiwasha hatari, wanashangaa iweje tunafungwa pia? Na tukifungwa hizo mara chache wanatafuta mchawi. Wanapoona ni Gabriel wanawaka moto balaa kuliko ingekuwa Saliba. Huenda Gabriel Kawa scapegoat wetu wa Sasa kama alivyowahi kuwa Xhaka na Mustaphi kabla yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…