Arsenal (The Gunners) | Special Thread

The Mighty Arsenal still on top of the table and nobody can take us down, i sound arrogantly tho.
Mashabiki wa ArseNyani banaaaa, nyie ni Comedian by nature.
Haya on top of the table tayari ameshakaa mwenye ligi yake, kesho mnang'atwa na nyuki halafu wiki ijayo Spurs nae anawashikisha ukuta.
Tena mnatakiwa mshukuru kifo cha Malikia Elizabeth ndio kimewabakiza hapo kwa wiki moja, la sivyo hizo mechi zenu zilizoahirishwa za Man City na Everton ndio zingewaondoa hapo juu.
 
Unaumia ukiwa wapi?
Kesho nyuki anapigwa 6 kavu
 
Brentford sio timu rahisi kucheza nayo tena ukiwa ugenini.

Tunaenda kucheza mechi ambayo kwa haraka naweza kusema ni kama ile ya Newcastle ya msimu uliopita, ni ngumu na inahitaji nguvu kubwa kuondoka na points zote 3.

Mbali na kuwa na wachezaji wazuri, Brentford ina moja kati ya mwalimu mzuri sana kwenye EPL, Thomas Frank ni bonge la kocha (tactically) japo kwa Mikel bado haingii.

Okay, iko hivi.. Kwa kidogo nilivyowaona Brentford, watajaribu kuanzia kucheza nyuma ila kwa jinsi tulivyo na system nzuri kwenye kukabia juu lazima tutawalizimisha kupiga mbele huku wakitegemea mipira ya kutua (second balls) ili wachukue washambulie.

David Raya na Ivan Toney watakuwa sumu kwenye hii mechi, hivyo inabidi tufanye kazi sana kuiwahi mipira iliyotua kwa ajili ya kupanga mashambulizi au kucontrol gemu.

Matokeo kwenye hii mechi yatapatikana baada ya kuvuka hatua ya kwanza na hatua ya pili kwenye kupanga mashambulizi (kwenye letu na katikati) ni mechi ambayo tunahitaji defense na midfield ziwe kwenye ubora wa 101%.
 
William Saliba arrived with the rest of the squad at the team hotel ahead of Brentford this morning. Thomas Partey also with the team. Oleksandr Zinchenko not spotted.

#BREARS
 
Yaani wewe jamaa hua nnahakikisha kwanza na like comment yako kisha ndio nnaanza kuisoma, yaani mashabiki wa Arsenal wote wangekua kama wewe hii timu ingekua inapendwa kuliko timu yoyote duniani.
Binafsi hua nnakukubali kinoma hamis77 yaani laiti kama mashabiki wangekua wanasajiliwa na timu ningekupambania kwa Glazers family wahakikishe wamekusainisha kwenye timu kubwa zaidi duniani, ni hazina kubwa sana kwenye timu kua na shabiki mwenye kaliba yako.
Hakika wewe sio tu shabiki wa mpira bali ni mpenzi wa kandanda ila nasikitika tu hilo timu ulilochagua kulishabikia linaweza kukusababishia magonjwa ya moyo au bipolar disorder.
 
Sisi kama Brentford tuna jambo letu leo hatutawaangusha mashabiki zetu tutapiga pale pale kwenye mshono viva Brentford
 
Unataka uhamie arsenyeto nn
 
Nahisi kuna mchezo nyuma ya pazia unaendelea
Martinel, Jesus, Gabriel
Hapo edu katia ngumu wachezaji waziende kwenye hiyo mechi ya kirafiki

Zinchenko unaambiwa kaumia, na timu ya taifa hatakuwepo

Odegard unaambia nae kajichuna kidogo kwenye mguu, leo hatakuwepo na timu ya taifa pia

KUNA MCHEZO UNAENDELEA

Unaweza kusikia baada ya game partey nae kaumia ili abaki London
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…