Blades walicheza 3 5 2 ila Arsenal imepata goli tatu, mechi iliyopita dhidi ya Slavia Arsenal ilikosa chances nyingi za kuscore. Auba na Pepe wakaleta tofauti walipoingia sub waliokuepo hawakua na uhusiano mzuri na nyavu ama hilo au ni kwamba Blades wana defense ya kiwango cha chini ukiwalinganisha na Slavia.
Game ya jana ushindi ilikua ni kama unacheza PlayStation FIFA/ PES ilikua ni L1+X+∆ na []+R2.
Jana Xhaka kachezeshwa LB Ceballos kakaa namba ya Xhaka surprisingly kila mmoja kacheza vizuri. Nilivyoona Xhaka na Chambers wameanza kama fullbacks niliona ni mpango wa Arteta kuwalinda Cedric na Bellerin kwa ajili ya game ya Alhamis.
Now Xhaka defended but he wasn't good in attacking this means Cedric ni ataanza tu hiyo Alhamis as hiyo siku kinachohitajika ni ushindi. Same kwa Chambers, so as good as Dani performed tusishangae akala mkeka au la akawekwa kama AM nafasi ambayo aliwekwa siku fulani hivi na hakuperform ipasavyo.
Arteta ana wakati mgumu, anahitaji ushindi Europa na EPL na ana majeruhi ila akipanga kikosi haonyeshi hivyo. Tuone Alhamis itakuaje.