Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Sasa hivi tumebakiwa na Europa tu. Siku tunatolewa Carabao nikaona kwahiyo timu inabakiwa na priorities mbili Fa na Europa. Ila ilitakiwa iwe funzo, juzi hivi nilisema tumeshinda kwa newcastle ila siyo timu ngumu kwa sasa kisha nikasema Sotonaliikamia gemu na timu ambayo haijatrain kwa wiki 3.

Tulitarajia game na timu inayotrain kila siku apange watu gani?

Jana shots nyingi zilikua blocked, forward iikua haioni hata inapiga wapi ilikua ni kushuti kisha mtu wa Soton anajitupa mbele ya mpira, ni kama kucheza Ultimate team kwenye FIFA 21 inawezekana unapiga zako shuti unajiona uko 1 v 1 ila beki uliyemuacha hatua nne nyuma unashtuka yuko mbele anablock hilo shuti it's weird.

Kipindi cha kwanza tumepoteza nafasi mbili au tatu za kuscore, kipindi cha pili tumepoteza nafasi mbili. Hii inatuambia nini? Hii inatuambia Balogun ni bora kuliko Nketiah, Nketiah anahitaji akakomazwe. Edu na wenzake ni miyeyusho wangeweza kuwachukua kwa mikopo ST wengi waliokua wanatolewa kwa mikopo, inatuambia kwamba Pepe anahitaji game time kwenye ligi.

Pia Willian anatakiwa aende sasa.

Kila timu hua na talisman wake, siyo lazima ila hua inatokea. Unakuta huyo mchezaji akiwepo timu ni ama ishinde au isuluhu hakuna option ya kufungwa. Kwa united ni Bruno, Liva alikua Henderson, chelsea wanafikiri talisman wao ni Ziyech, kwa Arsenal talisman ni Tierney.

Yaani huyu inabidi iwe iwavyo apangwe. A kind of player anasababisha wapinzani wasijisahau na Mungu anakuumbua kila ukimuweka nje. Ni komedi watu wa jf tunakubaliana timu inahitaji LB na AM ila wenye timu wameleta kipa, ama kweli cha mtu gogo.

Mwanampotevu alivyorudi wote tukashangilia kisha akatuchoma kwa bao pekee. Anyway hii haimaanishi kwamba kiwango chake nina mashaka nacho mipira get deflected kwa yeyote so he is still good. Jumanne tunaruka nao tena Soton kwenye epl, itakua ni komedi nyingine amabyo itabidi twende na uso serious.

Mimi naamini timu inayomiliki mpira inahitaji watu watatu au wanne wenye akili za runs na kutoa pasi kutafuta nafasi mbele regardless kama kuna AM au hakuna. Ndiyo maana Emile, Saka, Tierney na Partey wakiwepo unaweza ona game inakua ya kushambulia zaidi.

Anyway, kama itakupunguzia machungu ni kwamba Arsenal kaifunga Soton mara 24, kasuluhu naye mara 13. Soton kaifunga Arsenal mara 9 na jana ameifunga Arsenal kwa mara ya kwanza kwenye FA.
 
Ninacho wapendea mashabiki wa aseno, wakifungwa huwaoni week mbili.
Jukwaa wanamsusia Castr.

Leo wale wapenda tetesi za usajili kutoka kwa AronArsenal imekula kwetu, jamaa hatotokea humu, labda Kuku (Livapunga) anyee manati.

Hongereni wazee wa nduki kali.
 
Hivi kuna mtu anae amini kua aseno gari limewaka?
Aseno ni kama maiti aliye piga chafya, kwahiyo asitutishe tuendelee na maandalizi ya kumzika tu.

NB: Maiti anaweza hata akajamba, ukiwa mgeni wa maiti lazima utajipa imani kua mshikaji bado mzima, kumbe kude.
 
Tarehe 30 sio tu nita tamba! Bali nitafungulia koki ya maji machafu mulowe.
Southampton wamekukaanga, sisi tutakufanya kitu mbaya mpaka majirani zako watakukataaa.
Endelea kuota uwezo huo huna, Soton ngoja ntachomfanya nxt match ili uogope zaidi
 
Hivi kuna mtu anae amini kua aseno gari limewaka?
Aseno ni kama maiti aliye piga chafya, kwahiyo asitutishe tuendelee na maandalizi ya kumzika tu.

NB: Maiti anaweza hata akajamba, ukiwa mgeni wa maiti lazima utajipa imani kua mshikaji bado mzima, kumbe kude.
Gari kuwaka ndiyo nini wewe brazamen? Hii timu inategemea mbinu haitegemei bahati na kubebwa.
 
Back
Top Bottom