Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Mkuu na we unakua mgeni ktk soka nn? Starting lineup itatokaje sahv ilihali game inachezwa SAA 2:30 huko?
Pengine labda nimekosea kuuliza swali, ilitakiwa niuulize possible starting line up

Na sio lazima itoke muda mchache kabla ya game, mbona ni kawaida sana kutoa hasubui na game inapigwa jioni
 
Kwahiyo mzee baba umehama kabisa Zebra United au ni kwa kipindi hiki tu
 
Nilifanya makosa sana siku ile kukuacha hivihivi na ndio unaanza kunitambia hapa☹️☹️

Shughuli yako inakuja lazima heshima irudi
 
Pengine labda nimekosea kuuliza swali, ilitakiwa niuulize possible starting line up

Na sio lazima itoke muda mchache kabla ya game, mbona ni kawaida sana kutoa hasubui na game inapigwa jioni
WE ulisikia wapi......Sijawahi kuona hyo kitu labda hapa bongo....kwamba game inachezwa jioni afu official starting eleven inatoka asubuhi....labda ligi za china
 
Kuna watu waliibuka kipindi fulani wakasema msimu huu kombe letu. Sijui wamepotea wapi.

Arsenal ni timu kubwa sana hii rough road inayopitiwa saa hii haitaiangusha Arsenal. Wataanguka makocha, bodi, wamiliki na wachezaji lakini hii timu itabaki hapa.

So kama kuna nigga anatarajia timu kuyeyuka kama Kajumulo FC miaka ya 2000 kwa Arsenal hapana, too much a giant kurudishwa chini. Timu kubwa hushuka daraja kwa sababu nyingine nyingine ila siyo kufungwa. Juve, Inter na wenzao hiko ndiyo kiliwatoa serie A na siyo vipigo.

Kuanzia 2008 mpaka 2014 liva ilikua inashika nafasi ya 6, 7 na 8 lakini wote tulijua haitashuka daraja. So hatutashuka daraja lakini ili kujinasua inabidi tupitie ruti wanazopita wenzetu.

Liva ilinunuliwa na wamiliki wapya cash ikamwagwa.

Chelsea ilinunuliwa na wamiliki wapya cash ikamwagwa.

New Castle hiyo ruti wamebaniwa.

Wolves ina wamiliki wapya ambao demand yao ni timu kubaki ligi kuu tu.

Levy kajiongeza kwa kumwaga cash.

Everton, Aston n.k

Van Gaal alisema kwa United ilikua ngumu kutoboa kimpira as CEO wao hana historia na mpira hata wetu ni hivyo pia hajali kitu kuhusu mpira.

Tunahitaji mwingine mwenye maono zaidi anayejua what matters in football.

Morali ya timu is shaken.
 
Ukiwa unacheza PES au FIFA iwe ya PS 4 au 3 halafu unatamani utumie kikosi chetu katika hiyo game tumia 4 3 1 2.

LB anakua Tierney.

CB ni Gabriel na Luiz.

RB Bellerin.

CDM Elneny

CM Partey na Ceballos.

AM Pepe

ST Auba na Laca.

Subs: Nketiah, Willian, Runarrsson,Nelson, Willock, Niles

Kwenye PES set

Attack : Tiki Taka.
Maintain formation.
Support level 50%

Defense: Deep Defensive Line.
Defense line unaishusha mpaka bar mbili.

Kwenye FIFA
Defense: Balanced
Attack: Balanced.

Anza kugawa vipigo.
 
Kwahiyo mzee baba umehama kabisa Zebra United au ni kwa kipindi hiki tu
Ha ha haa. Mie ninayo falsafa yangu moja hiyo. "Huwa sikai upande mmoja na kitu ambacho hakitafuti mafanikio". United ilinitesa sana kwani hata Woodward kaendelea kusisitiza hapo juzi kati kuwa malengo yanatekelezwa vizuri kabisa; kujenga timu kupitia vijana chipukizi, kucheza mpira wa kushambulia, na kucheza mpira unaovutia!

Sasa mimi nilizoea kipindi cha SAF lengo lilikuwa ni moja tu, kushinda mataji. Iwe kwa kushambulia, comeback, au kilinda goli moja kama mwali vile. Kwa hiyo baada ya kuvumilia vituko vya timu kwa miaka 6 tangu 2013 mpaka 2018 nikasema inatosha mimi nimezoea kushangilia timu inayolenga mafanikio ya uwanjani.

Bahati nzuri nikaishia kuipenda project ya Spurs. Siyo shabiki maandazi!
Ni Spurs asilimia
.

Kwa kifupi ni hivyo. Nipo sana tu.
 
Nilifanya makosa sana siku ile kukuacha hivihivi na ndio unaanza kunitambia hapa


Shughuli yako inakuja lazima heshima irudi
Msimu uliopita mlibahatisha kwa kuwa timu ilikuwa ya kuungaunga ila msimu huu, ngoja kwanza nicheki game na nyie lini niandae mahindi ya kukaanga mapema. Moja baada ya jingine, mjini wanayaita pop kon.
 
Mbona kwenye picha yenu hamna kombe? Wekeni hata chupa za chai
We bwana wewe
. Makombe yako mengi tu pale juu mwanzoni mwa "sredi" yetu sema ni makombe ya mbuzi kwa kweli. Sema siyo ishu maana hata Chelsea Jose alipoishika ilikuwa na kakombe kamoja tu tena ka miaka 50 iliyopita (nusu karne!).

Respect Jose
 
Kusoma koment kutoka kwa shabiki anayejua mpira kuna raha ya bwana. Ukweli mtupu. Hapo kwa Levy ongezea nyama kidogo. Jamaa ni football genius na malengo yake ni vyote viwili: Kufanikiwa uwanjani na nje ya uwanja. Hivyo kafanya ubahili kwa miaka takriban 10 ili kujenga miundombinu ya klabu (hasa uwanja) kisha sasa karudi kiwanjani.
 
Msimu uliopita mlibahatisha kwa kuwa timu ilikuwa ya kuungaunga ila msimu huu, ngoja kwanza nicheki game na nyie lini niandae mahindi ya kukaanga mapema. Moja baada ya jingine, mjini wanayaita pop kon.
Mimi ni shabiki wa damu siwezi hama timu yangu kwa matokeo mabaya ina maana wale mashabiki maandazi wa karne hii ya 21 wanaweza kuhama huwezi kumbadili chui ngozi yake au huwezi kubadili kabila lako au huwezi kumbadili mtoto wako wa kumzaa hii yote ni mifano ninakupa hili chama langu nimetoka nalo mbali sana toka 94 mpaka sasa na mpaka naingia kaburini nitabaki kuwa The Gunners au washika mtutu wa London mlio kuwa mashabiki maandazi mtaondoka na mtatuachia chama letu tutaendelea kusonga mbele hakuna barabara isiyokuwa na mabonde na milima ya kupanda na kushuka ninashangaa sana mwanaume mwenye mke na watoto analilia lia na kuhama timu eti kisa kufungwa hakuna timu isiyofungwa duniani kama wewe ni shabiki kindakindaki mwanaume lazima ukubali kuwa matokeo yapo aina tatu kushinda, sare na kufungwa haya yote ni matokeo lazima uyakubali.
Always I support The Gunners and London is Red for ever and ever!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…