Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Kwa Aina ya uchezaji wa Wolves lazima umpigwe mkijitahidi Sana Ni draw save hii comment utakuwa kuona wewemwenyewe.Wale jamaa wanakaba wanakupa mpira umiliki alafu wanatumia counter attack kukumaliza na nyinyi Ni wabovu Sana mkipewa nyinyi mmiliki mpira na mnaacha magepu wenzenu watayatumia.
 
Wolves hua haina mpango wa kumiliki mpira ilimiliki mpira kwa man u. Kwa city ilishinda bila kumiliki mpira.

Kama tulisurvive kwa Leeds ambao at any given time kunakua na wachezaji wanne golini kwako na wote wanataka kushinda na huku tupo pungufu sioni Wolves ya 3 4 3 itashindia wapi kwa hizo counter.

Huu usemi wa kuna timu wewe ziachie mpira zinakua hazina la kuufanya mwanzo niliuona uzi wa man u leo naona umeuleta huku kwa logic yenu City anavyofungwa huku anamiliki mpira sitoshangaa siku mkisema "City mpe mpira hatojua cha kuufanya"

Sasa acha tuone.
 
Tofautisha Wolves na Leeds mzee Wolves Wana clinical finisher Jimenez alafu Wana uzoefu against big team compare to Leeds so msijipe matumaini hewa.
 
Tofautisha Wolves na Leeds mzee Wolves Wana clinical finisher Jimenez alafu Wana uzoefu against big team compare to Leeds so msijipe matumaini hewa.
Mara ya mwisho Wolves kushinda goli zaidi ya 3 ni lini? Leeds mara ya mwisho kushinda goli zaidi ya tatu lini?

Jimenez ana hat trick tangu msimu uanze? Je Bamford wa Leeds?

Bamford ana magoli mangapi na Jimenez ana mangapi?

Clinical finisher?

Namna pekee watashinda ni kwa kupaki basi, kuvizia counter na long range shots. Yaani wacheze kama Leicester.

Bob tulia
 
Usije baadae ukakimbia tu Huu Uzi tupo hapa me nakupa fact wewe unaleta ushabiki wewe si umeona mashabiki wenzako wamegoma kuangalia game ya leo
 
Usije baadae ukakimbia tu Huu Uzi tupo hapa me nakupa fact wewe unaleta ushabiki wewe si umeona mashabiki wenzako wamegoma kuangalia game ya leo
Wewe ni member mpya.

Hata haujui wtu wanaokimbia majukwaa yao wakipokea vipigo.

Kwahiyo unafikiri mimi nilichokua nauliza hapo ni ushabiki? Kwahiyo facts zako zinakuambia Jimenez kamzidi magoli Bamford na ana hat trick? Au unazungumzia facts gani mzee?

Leo Mourinho atawajaribu na hizo counter unazozisema. Now ndiyo utajua Jimenez na Kane nani ni clinical finisher.
 
huu ni mtazamo tu, sasa unapofeli kutumia maneno "ni lazima mpigwe"
 
Usije baadae ukakimbia tu Huu Uzi tupo hapa me nakupa fact wewe unaleta ushabiki wewe si umeona mashabiki wenzako wamegoma kuangalia game ya leo
Wewe nikuombe baada ya mechi uje hapa kutoa uchambuzi wako, Gunners ikishinda ipe sifa usiwe tu bitterness
 
Ngoja tuone!!
 
Tofautisha Wolves na Leeds mzee Wolves Wana clinical finisher Jimenez alafu Wana uzoefu against big team compare to Leeds so msijipe matumaini hewa.
Kwamba Wolves wanauzoefu
against big team,
Unaandika kwa kutumia nguvu sana wewe jamaa
 
Pamoja na yote, hatuko vizuri na hali sio nzuri. I love my team but tupo vibaya.
Tupo vibaya sana na tatizo kwa sasa haliwezi kitatuliwa may be wachezaji wajitoe kweli kweli na hicho kitu kwa sasa hawakifanyi 5 matches 1 goal tena la penalty kwa haraka haraka hatuna uwezo wa kufanya comebacks kama tukianza kufungwa goli hata kama ni dk ya 1 thats means mpira kwa upande wetu unakuwa ni Full Time naona Robbie na wenzake wanajaribu kupanga kikosi cha leo ila kila wakipanga wanaona pana mapungufu ceballos naye tangia atoage assists 2 last season kawa yupo yupo na Xhaka ana homa ya vipindi hatabiriki kwa ufupi hatuna midfield ya maana kwa sasa tuwategemee defenders kuzuia tu midfield haizuii wala kupeleka mipira kwa wafungaji wetu ni kuomba tu beki ifanye kazi yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…