Umegusia issue ya Leeds hapo na 4-1-4-1 yao, kiukweli nampenda sana Bielsa ni 'football genius'. Jamaa anavyoitumia hii formation natamani Arteta acopy baadhi ya vitu kisha aviboreshe, labda chanagamoto kubwa itakuwa kucope na speed na intensity ya game over 90mins.
Leeds ukipitia highlights zao utaona jinsi wanavyo shambulia, wanakuwa na watu hadi 6 wanao approach box ya mpinzani na wote hao hufika kwa speed kali ambapo huwafanya wawe ama 6v4 au 6v3.
Kuna viungo watatu ambao hawaingii ndani ya box au wanaingia na kutoka chap, wawili wanakuwa kwenye angle za 18 yard box na huyu mmoja yupo kwenye ile 'D' ya 18 yard box, then strikers/viungo wawili wanaingia kwenye 18 huku mmoja yuko na mpira.
Hapo wanaistrech defence na kuacha space pana ya ama kupiga penetration passes ama kupiga mashuti nje ya 18 na magoli yao mengi wanafunga nje ya 18.
Natamani style hiyo ili kutoa space ya kutosha kwa wingers wetu ( Auba, Pepe,Willian, Nketiah) na pia kubypass role ya AM ambaye kwa sasa hatuna lakini pia ni mfumo mzuri wa kushambulia unapocheza na timu kama Liver au City.
Hii style ya kushambulia aliitumia pia Klopp akiwa Dortmund kama utakumbuka partnership ya Auba, Reus, Mikhi na Lewandoski. Pia hata sasa anaitumia pale Liver japo kaifanyia maboresho kidogo.