Wakati naanza kuishabikia Arsenal mid 90s, nilikuwa napata maumivu sana tunapofungwa, hiyo ilinifanya niwe nacheki analysis baada ya mechi(uzuri tulikuwa na SuperSports home).
Nikagundua kuwa hata kufatilia uchambuzi wa kabla ya mechi na half time ni muhimu sana, inakufanya uwe na matarajio yanayo endana na uhalisia hivyo kuweza kucontrol hisia za matokeo. Baada ya ujio wa internet nikawa nafatilia mengi sana kabla ya game nayo ikanisaidia sana kumudu mihemko yangu ya kishabiki.
Nilichogundua fans wengi hawana uelewa mpana wa haya mambo, timu yake ina injury za kutosha bado anaweza hata 'kupinga mke mke'



unamcheki unaona huyu muda si mrefu mke wake anaweza kufanywa house girl kwa watu sababu ya 'unazi' wa kijinga.
Tukijifunza kufatilia haya mambo, kuna lawama nyingi humu ndani zitakufa 'natural death'. Atleast mashabiki wengi wa Liver huwa hawana mihemko, ila kwa haya mafanikio wanayopata sasa tutegemee mihemko kutokana na kupata mashabiki wafata mkumbo.