Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Tuiite hii kazi ya Arteta awamu ya pili. Ya kwanza ni kuimarisha ulinzi na kiungo kupunguza magoli ya kufungwa (eti kwa sasa tuna beki bora kwa EPL kwa kufungwa magoli machache). Ya pili itakuwa kuimarisha ubunifu na utengenezaji wa nafasi nyingi na kuzimalizia pia ili kuongeza magoli ya kufunga. Ya tatu ni kuchanganya hizi mbili vizuri na kucheza mpira unaovutia kiasi cha kumtoa nyoka pangoni au kumfanya shabiki wa timu pinzani kutamani kwenda kibanda umiza kuangalia chama letu kama ilivyokuwa zamani. Bado tuko awamu ya kwanza.
 
Katika mechi tano tulitarget kukusanya points 15. Tukapoteza kwa liva tukapoteza kwa city na tukapoteza kwa leicester.

Tumepata points kwa man. Next fixture ili kukamilisha zile games tano ni dhidi ya Aston villa. Villa kapigwa jana lakini aliuwasha moto kiasi kwamba ilikua a matter of time before kupata sare.

Tukishinda itamaanisha katika games tano Arteta kamanage kupata points sita. Ni rekodi ya kutambia? Definitely "No" scorer ni Auba pekee na mabeki wote wamehamia kwake.

Shot takers hatuna. Jana Partey na Elneny walijaribu ila ilikua ni mara moja na hawakurudia tena.

Naamini kocha anaona timu yetu ikiwa na watu katikati inakua inao mpira ila haina mtu wa kusogea na kuigawa mbele. naona 3 4 3 ndiyo formation inayotufaa kwa sasa.

Wakati mwingine ni kumuamini kocha kuliko hata wachezaji.
 
Fact
 
Rob alikuwa anamchezea kihuni huyu dogo, akiruka anaruka nae,

Hii combo ni nomaView attachment 1617898
Kiukweli kwa game na Utd na hawa defenders wetu wote ambao hawana uzoefu wa kutosha then wamewadhibiti manyumbu mwanzo mwisho, sikutegemea kabisa.

Kuna mdau hapo juu kasema huyu Gabriel ni kama tumewatapeli Lille, kazi anayopiga na bei tuliyo mnunua havina uwiano kabisa. Ukimlinganisha na Halima gwaya dah.... lazma uamini uchawi upo.
 
Zile hat trick ni kwa sababu alikutana na wavimba macho, jana kakutana na wazee wa kazi hii ndo utajua wa epl😂😂😂😂😂
na wewe unakuwa kama dada poa, nimekuona kwenye jukwa la Man U ukiisifia Arsenal ilivyomtandika jana, halafu unakuja huku kuonyesha your hypocrites. Be like a man simamamia unaloliamini.
 
True
 
jana nilimsikia Auba na Leno wanasema wapo kwenye process ya transformation, kawaida ukiwa kwenye process unamaliza moja before embarking on another.
 
Ni sahihi mkuu, tuwe wavumilivu. Watu wanasahau huyu Arteta hana hata Managerial experience lakini so far hakuna kocha mkongwe pale EPL ambaye hajaonja shubiri yake.

Kitu kingine bado hatuja maliza kuimarisha kikosi (usajili), kila fan anakiri tunahitaji creative attacking midfielder(s) ili tuweze kunyumbulika kule mbele.

Lakini Arteta bado ameweza kushow case uwezo wake wa kufundisha mifumo mingi tofauti kwa players walewale na anaitumia against different opponents na anafanikiwa, that's a complement.

Kwangu me hiki ni kipimo kizuri kuwa tumepata kocha wa kumrithi Wenger, unaanza na average players ila matunda yanaonekana.

Jamani nendeni pale Chelsea mkaone timu ina strikers wa £200m+ na wanastruggle kufunga/kushinda, wito wangu kwa fans ni kuwa tuendelee kupiga mtori, nyama ziko chini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…