Arsenal (The Gunners) | Special Thread

OK great nimeelewa now
 
Mimi kwa upande wangu nipo sambamba na Arteta.

Nimewahi kumfuatilia William Saliba kwa kiasi ( including YouTube clips) nikarudi na jibu kuwa jamaa bado hajakuwa mchezaji wa kuichezea Arsenal.

Naona ana makosa mengi anapokuwa kwenye nafasi yake, hasa akicheza CB.. Bado naona ana mengi ya kujifunza ukizingatia bado umri unamruhusu.

Pia naona Arteta katumia akili sana kutotengeneza hiyo combo ya Saliba na Gabriel kwa kipindi hiki, ambayo mashabiki wengi walikuwa na hamu kuiona..

Kwa sababu itawalazimu wawape muda zaidi wa kuzoeana, hivyo wanaweza wakatuchelewesha ukizingatia msimu huu tuna jambo letu!


Ungekuta mpaka muda huu tusharuhusu more goals than what we expected, kwa kusubiri watu wazoeane.. Hata hii nafasi tuliyopo sasa sidhani kama tungekuwa nayo ukizingatia W zetu zimekuwa nyembamba wiki za mwisho.

Naona Arteta kaona atumie resources zilizo tayari kama wakina D. Luiz (ambae hana muda mrefu mpaka kuondoka), Rob Holding na wengine..
Hata combo ya Holding na Gabriel ni nzuri japo ni immature sana.

Mi naona tumpe muda Saliba afanye improvement kwenye soka lake.
 
Dah umeni attack sana aisee

Sina la kusema , nadhani wewe ni mgeni , nimeonesha wapi chuki kwa Ozil zaidi ya kuleta taarifa ya kinachoendelea ?

Unaletaje shutuma za udini ? Una hangover ? Kuna mtu kakuuliza hapo juu umekunywa kilevi ?
 
Nimesikitika sana Huyo ndugu kusema namchukia Ozil, wakati nimeleta taarifa ,tena awali nilikuwa sijui kama hili la China lina athari kubwa

Na msimamo wangu nimekuwa nikisema Ozil yupo sahihi 100%

Lakini Na Arsenal wapo sahihi 100%.

Kwahiyo Arsenal wakajitenga wasiendelee kukosa mapato ambayo hayo hayo wanayatumia kumlipa Ozil

Angalia hapa chini Jinsi Arsenal alivyoanza kukosa mapato ...

 
Correct. Hauwezi kuliangalia hili kwa wepesi. Timu zinaajiri 'social media consultants' na wana 'public relations officers' kwa ajili tu ya kuongezea mahusiano kati ya timu na mashabiki kwa nia ya kuongezea timu faida. Kuhusu wanawake wa ManUtd, sijui lakini nahisi kwamba kwa sababu ni wamarekani na huko kwao pia jezi za timu ya taifa za wanawake zimepita kwa mauzo jezi ya wanaume so kuna support kubwa kule. Nadhani media za USA imesupport sana mchezo wa wanawake kuliko maeneo mengine. Pia labda imechangiwa na hawa wawili kuwa wapenzi so wanapata support kutoka kwa wanaofuatilia mahusiano yao?
 
Hili la upenzi ndiyo nimejua kutoka kwako muda huu. Ingeku lesbianism ni factor katika ununuzi wa jezi hauoni na jezi ya Greenwood ilitakiwa kupaa kimauzo?

Arsenal ilitenga jukwaa la gays, lakini sales haikua kubwa. Notisi kwamba jezi ya Arsenal imepaa kimauzo baada ya Arteta, kuitransform timu na hizo trophies mbili. Same kwa liva.

Nahisi mafanikio ya timu na mashabiki kua na imani na timu ni factor kubwa kuliko kua gay au lesbian.
 
Kweli. Najaribu tu kujiuliza maswali maana United wamekuwa na timu ya wanawake juzi juzi tu, sijui 2017 or so kwa hiyo ningetegemea wao wategemee nyota ya timu ya wanaume so nashangaa imekuwaje. Ndiyo maana nikaanza na kuhisi kuwa kutoka Marekani ni factor pia. Swala la upenzi kwenye soka la wanawake ni la kawaida sana , nahisi 40% wanaweza kufika. Greenwood sijui lolote kuhusu yeye.
 
Kama hao wachezaji waislamu uliowataja wanaangalia maslahi zaidi ? Je ni jambo bora kutanguliza maslahi badala ya utu?

Sent from my TECNO-N2 using JamiiForums mobile app
Angetaka kuonesha huo utu, angekuwa Sheikh kwenye mimbari kama Masheikh wengine wanavyo fanya.

Amechagua mpira sababu anapenda maslahi manono, asituletee unafki wake.

Alikataa kusign mkataba Arsenal akidai maslahi makubwa then leo anaivurugia Arsenal mapato ambayo ndiyo yanamfanya alipwe eti kwa kujifanya mswalihina.

Miongoni mwa pesa anazolipwa zinatoka kwa hao anaojifanya kuwapinga ila hela zao anapokea, binafsi ningemuelewa km angeachana na soka aingie kwenye uanaharakati wa dini.
 
Wanatunishiana misuli jamaa.

For the first time this season, kuamkia leo ndo wameonesha game ya NBA kupitia CCTV (China TV).

View attachment 1595624
Kwa population iliyopo China (1.5b+) ambayo ni almost robo ya dunia nzima na ukichanganya na uchumi wao lazima awe na power sana, ndio maana hata US anaufyata na pia China ana influence kwenye mataifa mengi ya Asia.

India na Africa zina nusu ya population ya dunia ( 1.5b+ @) lakini hawana jeuri sababu ni masikini, hawana sifa timilifu ya kuitwa 'soko muhimu'.
 
Nimecheka sana ulivyomaliza hapo
Ha haaa, nadhani aliambiwa kabisa anyoe, tactically nywele zinaupoza mpira kwa hiyo defender akipiga header (tofauti na paji la uso) mpira utaangukia karibu na kukaribisha shambulizi zaidi.

Hata strikers wengi hawatimui manywele kama Willian kwa sababu hiyo pia, zinaathiri direction na speed ya mpira wanapopiga header.

Huyu Luiz ndio beki kiburi hataki kunyoa
 
Mbona Arteta alikuwa very clear, ni sahihi kwamba alikuwa kwa mkopo last season lkn muda mwingi alikuwa majeruhi kisha issue ya covi-19 ikazuka kwa hiyo hakuwa na successful loan spell.

Unapopeleka mchezaji kwa mkopo mahali kwa tactical issues unamueleza akaimprove attributes zipi na unachagua club itayo msaidia kufanikisha hilo.

Saliba ameambiwa akajirekebishe kudefend set pieces na aache kutumia diving tackles. Kwa EPL kama huwezi kudefend set pieces vizuri timu ndogo zitakuua kila siku na kwa tackles zake ataumia almost kila mechi.
 
Jana Xhaka katoa boko huko kwao akapigwa goli. Hii midfield ya xhaka tutafika kwel!?
 
Nmeona tetesi mahali flani mtandaoni... Kibabu Arsene Wenger anahimiza na kudai ya kwamba özil bado anaweza kuisaidia pakubwa sana Gunners...
 
Nmeona tetesi mahali flani mtandaoni... Kibabu Arsene Wenger anahimiza na kudai ya kwamba özil bado anaweza kuisaidia pakubwa sana Gunners...
Me pia nimemsoma, anasema kuwa akijengewa defensive unit nyuma yake ili asiwe na majukumu ya kukaba kama alivyo mtumia yeye atacheza na kusaidia timu.

Ingawa anakiri kuwa he is not the best player tactically hasa timu ikiwa haina mpira.

Sioni hilo likifanyika kwa Arteta, kwa nini ubadili mfumo wako ili kumchezesha mchezaji fulani tena ambaye hana future na club na wakati una players kibao wanao cheza mifumo tofauti, wako full committed na wana future na club?

Yaani mnakuwa 9 mkiwa mnakaba ila mkianza kushambulia ndio yeye anaongezeka. Badala yeye abadilike ili kufit kwenye mfumo anataka mfumo ubadilishwe kumfit yeye. Hata kina Messi na ubora wao wanatii mifumo, ye ni nani labda?
 
Umeongea ukweli mtupu, na ndicho alichosema Arteta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…