ARSENAL, COVID-19 NA CAGIGAO
Habari za jioni wadau.
Leo mchana klabu yetu ilitangaza mpango wa kuwapunguza kazi wafanyakazi wapatao 55. Sababu kubwa iliyoelezwa ni kuwa klabu imepata hasara kubwa na itaendelea kupata hasara kutokana na janga la Covid-19.
Hii sasa inafanya arsenal kubakiwa na wafanyakazi wanaokadiriwa kuwa ni 600 na kitu kutoka 700 na kitu. Hata hivyo idadi hiyo inaweza kupanda kwa kuwa kocha Arteta anatarajiwa kuongeza baadhi ya wataalumu ktk benchi la ufundi.
Nilipoiona hiyo habari mchana nikaanza kujiuliza ni watu gani watapunguzwa. Katu sikufikiria kuwa Cagigao (head of international recruitment atakuwa mmoja wao.)
Baadae kidogo magazeti ya Uingereza yakaja na habari kuwa Cagigao ni mmoja wa watu walioambiwa kuwa watapunguzwa. Habari hii ikawashtua watu haswa kutokana na sifa nzuri ya kuscout wachezaji ambayo Cagigao anayo pale arsenal. Ikumbukwe pia Cagigao amewahi kufikiriwa kupewa kaz ya technical director pale arsenal.
Binafsi nilishtuka kusikia habari hiyo na sikudhan kama Cagigao anaweza kuwa ni mmoja wa watakaopunguzwaa. Hata hivyo baada ya kufikiria kwa makini zaidi nikaelewa kwann Cagigao amekuwa mmoja wa muhanga.
Naamini kabisa kuwa Cagigao amekuwa muhanga wa hili kwasababu majukumu yake yanaingiliana kwa kiasi na majukumu ya Edu na pengine klabu imeona sasa kazi yake inaweza kufanya na Edu.
Ikumbukwe kuwa Cagigao alikuwa ni head of international scouting. Kazi yake haswaa ilikuwa ni kusafiri huku na kule kwenda kuwaona live wachezaji ambao alipewa taarifa na scout waliosambaa sehemu nyingi dunian. Na kisha yeye anatoa ushauri kwa klabu juu ya kusajiliwa au kutosajiliwa kwa huyo mchezaji. Kwahiyo kifupi kila mchezaji aliyetoka nje ya Uingereza ambaye alisajiliwa arsenal basi Cagigao alihusika.
Sasa kwasasa kazi kubwa ya usajili ikiwa ni pamoja na kujua ni aina gani ya mchezaji anayesajiliwa na arsenal inafanywa na Edu kama technical director. Hapa ndipo ninapoona kuwa majukumu yao yanaingiliana.
Ingawa sijapenda na sijafurahishwa kwa Cagigao kuondoka, napenda kuamini kuwa kama taarifa ya klabu ilivyosema kuwa kupunguzwa huko kwa staffs kutaiwezesha timu kuweza kuwekeza kwenye kununua wachezaji wazuri.
Tumaini langu kuwa klabu itafanya kama ilivyosema na nitoe pole kwa wafanyakazi waliopunguzwa. Natumai hali ya uchumi ikiimarika wataweza kurejea
Arsenal players who were scouted by Francis Cagigao:
-Lauren
-Cesc Fabregas
-Jose Antonio Reyes
-Santi Cazorla
-Nacho Monreal
-Mikel Arteta
-Emiliano Martinez
-Granit Xhaka
-Alexis
-Carlos Vela
-Hector Bellerin
-Robin van Persie
-Gabriel Martinelli
-William Saliba.