Haya poa.
Arsenal hatuna shot on target.
Man City walikua na on target 1 tu.
Mpira muda mwingi alikua nao Arsenal, usitishike tho, ilikua ni kuurudisha nyuma kuuleta pembeni kwa Cedric ambaye hakupiga hata cross moja yenye macho yet hakuacha kuendelea kupiga hizo cross na tukapoteza mpira unnecessarily.
Tulikua na watu 4 pale kati na wingers means watu 6 wangeweza kua pale. Ila mipira ilikua haikai, hatuna kiungo mwenye akili na ubunifu hatuna striker anayeweza kuamua kuibeba timu kwa kutembea na mpira na kushuti.
Tactic tuliyoitumia kwa City imetumiwa dhidi yetu. Beaten on our newfound game how about that? Na hatukua na cha kutunasua. Tulikua tunachekesha.
Juzi nilisema Lacazette siyo mzuri akiwa hana mpira as hawezi kukaba ila leo amekua hovyo hata alipokua na mpira.
Arteta alikuja gundua late kua kikosi alichokianzisha kina maandazi yapo mule mpaka anakuja kushtuka Asto walishaamua kuachana na 4 3 3 na kujipakia basi lao. Inanikumbusha Man U na Barca msimu uliopita Man U succesfully transformed 4 3 3 into 5 5.
Nataka nimuone mtu ambaye atasema Watford wameshinda kibahati. They deserved it, tulikua butu mno yaani hamna aliyeonekana anataka ushindi. Hata katika PS 3 au 4 mchezaji kama Nketiah huwezi kumuweka atokee pembeni as anakua na safari ndefu ili kuingia kati na hana pace, skills na nguvu so hua anaachwa kati kabisa.
Niliwahi sema Kolasinac na Tierney bora Tierney nikaambiwa mimi sijui kitu Kola anajitoa na ana nguvu, leo mtu kataka kuscore mbele yake tena mtu alivyomtoka mpaka nikashangaa.