Tatizo unalalamika sana mkuu!.. Tunajua unaipenda sana timu yetu na unaumia sana unapoona haifanyi vizuri!. Hata sisi tunaumia sana, lakini tofauti yetu na wewe ni kuwa wewe huangalii uhalisia wa mambo ulivyo!.. Baada ya arsenal kuflop chini ya Emery, sasa timu imempata Arteta ambae anajitahidi sana kuijenga timu, sio lahisi kwa kocha yoyote kwa Arsenal ile aliyoiacha Emery angeweza kufanya chochote, hata Guadiola angekabidhiwa ile timu angefungwa tu.. Mfano mzuri ni Mourinho, amerithi timu mbovu, na mpaka sasa bado tottenham haijarudia enzi zake maana wanashinda leo kesho wanapigwa. Sasa ukirudi kwetu timu yetu inaonyesha uhai japo hatuna beki wakutumainiwa na tuna upungifu wa midfield. Tunaangalia zaidi timu inachezaje hata kama tumefungwa! Kwa mfano leo kocha kapanga kikosi kizuri sana na tukapata matokeo mazuri lakini bahati mbaya Torreira akapata injury na jamaa wakasawazisha baada ya Mpira kumgonga Luiz kwa bahati mbaya na kubadili uelekeo na hatimaye kutinga kimiani! Sasa balaa likaendelea baada ya Auba kupigwa red card!. Kitendo cha kumaliza kwa kutoa draw inabidi tumpongeze kocha maana wale CP walikuwa wanacheza kama wehu (kibabe sana). Ingekuwa enzi za Emery leo tungepigwa bao nyingi sana!.. Lakini trend inaonyesha tunaimarika kidogo kidogo na hiyo ndio furaha yetu! Kwa mfano katika mechi tatu zinazofuata tukishinda mbili na kutoa draw moja yatakuwa mafanikio makubwa sana.. Ni kweli hatuna back up pale mchezaji anapoumia lakini hatulalamiki maana hata tukilalamika hapa akina Edu hawatasikia. Lakini pia kwa kocha tulie nae ameahasema kabisa anataka beki na midfield, sasa kama ameshasema malalmiko ya nini? Mimi niliposikia Arteta anasema anataka beki moja kwa moja nikajua tumepata kocha mwenye akili. Arsenal hatujawahi kuwa na shida ya forward toka enzi za akina Henry, Van persie, Giroud na hata hawa tulionao wapo fire sana!. Yaani hata Martinel ni bora sana ukilinganisha na baadhi ya mafoward wa timu kadhaa pale Epl.. Sasa kama ni hivyo tatizo tetu ni lipi?.. Tatizo letu ni beki mkuu!.. Hata ile the invisibles walimaliza msimu kwa kuwa tulifanya figisu tukamsajili Sol camblle toka Tottenham, na kuanziq hapo timu nzima ikabadilika kabisa na wakaenda msimu mzima bila kufungwa. Hata hii liverpool ya sasa siri ni beki. Kabla ya Van dijk hawakuwa imara kama sasa!. Mimi nilivyoona klop anavunja recors kwa kisajili beki kwa pesa ya forward nikajua huyu kocha anajua na ana akili kubwa na toka wampate Van dijk kuwashinda Liverpool imekuwa kama kupanda mlima kilimanjaro, kamuulize Messi atakuambia shughuli ya Van dijk. Hata Man City tatizo lao ni beki, na siku wakilipatia tiba hilo klop atapata tabu sana.. Ninachotaka kukwambia ni kuwa timu ikipata mchezaji hata mmoja tu ambaye ni sahihi timu itarudi katika ubora wake wa siku siku!. Usione Liverpool wanashinda ukafikiri wana back up kubwa, ukweli ni kuwa hakuna injury kubwa hasa kwa wachezaji tegemeo.. Sio kama sisi kila siku majeruhi. Nakuhakikishia siku Van Dijk akipata injury kwa miezi mitatu tu watapoteza point za kutosha.. Sisi hatulalamiki sana kuhusu usajili kwa vile tunajua angalau tukipata beki mbili kariba ya akina Kolibally au upamecano na mid mbili za maana (holding midfielder 1 na box to box midfilder 1) tutafika mbali sana!. Timu huwa inajengwa taratibu kwa strategy, tumpe muda mwalimu wetu na tumwamini.. Wachezaji hawa hawa tulionao wanatosha kuwa back up kama tukipata wachezajo wazuri wa kupngeza katika timu. Siamini kama Arteta anaweza tena kutuletea beki za £10, wewe subiri tumalize huu msimu utasikia tumeleta beki wa £60 na kuendelea!.. Pole mkuu kwa maumivu unayopata, ngoja tutafute namba ya simu ya Arteta ili uwe unamlalamikia yeye moja kwa moja!. Maana kwa kweli unatuchosha.. Watumie hata email uwaeleze matatizo yao, ilakulalamika hapa ni kazi bure labda kama unataka Mods wa JF wakanunue wachezaji unaotaka.. Pole sana mkuu tupo pamoja, angalia usije ukajinyonga tukamisi maandishi yako ya herufi kubwa.
Sent using
Jamii Forums mobile app