*Emery asema David Luiz kichwa, Spurs wajiandae*
Lakini, kocha Emery anaamini Luiz ataamsha dude katika mechi yake ya kwanza ya North London derby msimu tangu alipotua kwenye kikosi hicho cha Emirates. Luiz alijizuia asionyeshwe kadi ya pili ya njano uwanjani Anfield, wakati Mo Salah alipopita mbele yake kasi sana kwenda kufunga bao la pili, kitu ambacho kocha Emery amekipongeza na kusema ni ukomavu mkubwa.
LONDON, ENGLAND.KOCHA wa Arsenal, Unai Emery amesema beki wa kati David Luiz atarudi kwenye ubora wake na kuonyesha makali yake kwenye mechi ya kibabe dhidi ya Tottenham Hotspur kwenye Ligi Kuu England kesho Jumapili.
Beki huyo mpya wa Arsenal, Luiz aliyenaswa kw Pauniu 8 milioni kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi, amebebeshwa lawama kwamba alihusika kwenye mabao yote mawili aliyofunga Mohamed Salah kwenye mechi ya kipigo cha 3-1 kutoka kwa Liverpool wikiendi iliyopita.
Lakini, kocha Emery anaamini Luiz ataamsha dude katika mechi yake ya kwanza ya North London derby msimu tangu alipotua kwenye kikosi hicho cha Emirates. Luiz alijizuia asionyeshwe kadi ya pili ya njano uwanjani Anfield, wakati Mo Salah alipopita mbele yake kasi sana kwenda kufunga bao la pili, kitu ambacho kocha Emery amekipongeza na kusema ni ukomavu mkubwa.
Emery alisema: “Tunaweza kuzungumzia baadhi ya makosa kwa mchezaji mmoja mmoja. Lakini, pia tunaweza kuyazungumzia maamuzi mazuri ya mchezaji katika mechi. Kwenye ile penalti alionyeshwa kadi ya njano, hivyo kama angemchezea rafu Salah wakati anaenda kufunga bao la pili, angeonyeshwa kadi ya pili ya njano. Hivyo, uamuzi wake ulikuwa wa kutumia akili zaidi.
“Haikuwa rahisi kwake kufanya vile. Amejiunga nasi wiki tatu tu zilizopita, amelazimika kuzoea mazingira kwa haraka sana. Amenifurahisha kwa sababu amefanya uamuzi mzuri sana, ukomavu.”