Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Unai emery Leta Umtiti leta Zaha wajekufanya kaz,duh kolasinac hamna kitu.

Kolasinac unamwonea.

Tatizo ni Ozil ambae hakuweza kufanya kazi aliyokuwa akifanya Aaron Ramsey ya kuunganisha mashambulizi na kufuata mpira unapopotezwa kwa adui.

Kolasinac alikuwa akishambulia sana upande wa kulia wa Chelsea ila Aubameyang na Lacazette nao hawakuwa wakitulia pale kwenye eneo la hatari la Chelsea.
 
Ozil anahitaji kiungo imara na sisi kumiliki mpira, tusipokuwa na possession,Ozil utamuonea bure
 
Wale viwete wenu wabahatishaji wanaoshangilia goli kwa kushikana mikono hawakucheza
 
Unai naye mshenzi tu. Czech alishaagwa pamoja na Ramsey na tunaambiwa anakwenda Chelsea kuwa mkurugenzi wa michezo. Unamchezesha wa nini????. Hovyo kabisa
Leno game ya leo angefanya kitu zaidi ya Czech,japo kufungwa kwetu Siwezi kumbebesha gunia la misumari
 
Ozil anahitaji kiungo imara na sisi kumiliki mpira, tusipokuwa na possession,Ozil utamuonea bure

Unai Emery ni kocha mzuri na ana nia njema ya kutaka ushindi kwa Arsenal, ila amerithi timu mbovu timu yenye wachezaji legelege.

Arsenal msimu wa 2017/18 ilifungwa magoli 50 na msimu huu magoli 51 very poor defensive record.

Tunasubiri mwenye timu Stan Kroenke aingize mkono mfukoni atoe fedha za kutosha ili Emery asajili wachezaji anaowataka yeye.

Ozil msimu ujao atakuwa akitokea bench.
 
Aondoke tu
 
Stan kroenke si wakumtegemea aisee,ila kama kocha hakuweka masharti wakati anapewa kazi itakula kwetu,maana bila beki strong wawili,holding midfielders 2 tutaendelea kuteseka na vitimu vya kijinga jinga tu
 
Na Ndugu zenu Tottenham wajiandae na Heavyweight kama yenu
 
Chelsea 1 vs Arsenal 4
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…