Jinsi Arsenal itakavyopangwa kuikabili Chelsea.
Katika mechi ambazo Arsenal imeifunga Chelasea chini ya kocha Unai Emery, imetumia mtindo wa 4-4-2 ambao hitwa Diamond.
Ni mtindo ambao washambuliaji Aubameyang na Lacazette wanakuwa mbele na nyuma yao wanasimama Granit Xhaka, Matteo Guendouzi na Lucas Torreira.
Lakini mtindo wa diamond hauwezi kutumika kwa kuwa Aaron Ramsey na Henrikh Mkhitaryan hawapo hivyo kurudi kwenye mtindo wa 3-4-1-2 ambapo Matteo Guendouzi atasimama nyuma ya Mesut Ozil au Alex Iwobi na washambulaji Aubameyang na Lacazette.
Arsenal pia watajaribu kuwabana Chelsea wasitoke ndani ya eneo lao hivyo kumbana Jorginho asitoke pasi nyingi kueleke kwa Hazard au Higuaín.
Lakini wakati huohuo Arsenal itabidi iwe macho na David Luis na mipira yake mirefu ama kueleka kwa Pedro au Cesar Azpilicueta au katikati kwenye nafasi kwa mmoja wa wachezaji wa kiungo khasa Matteo Kovacic au Ross Barkley.
Arsenal pia inaweza kucheza mtindo wa mabeki watatu walinzi wa kati watatu, lakini Ainsley Maitland-Niles sio beki imara bado hivyo kutoa mwanya kwa Eden Hazard kupika mashambulizi upande wa kulia wa Arsenal kati ya Niles na Shkodran Mustafi.
Mchoro unaonyesha Hazard akiwachanganya mabeki namba mbili na nne wa Arsenal kwenye mechi ambayo Arsenal ilifungwa goli 3-2 pale Stamford Bridge.
Hivyo kocha Emery atamuamuru Lucas Torreira ashuke nyuma kumsaidia dogo Maitland -Niles na kufanya kuwepo watu wawili wanaomchunga Hazard asilete madhara.
Chelsea wakiona Hazard amebanwa basi watamtumia Alonso kwenda pembeni zaidi ili kuwachanganya mabeki wa Arsenal na kuleta nafasi kwa Hazard.
Katika mechi hii Aubameyang na Hazard ndo waamuzi wa mchezo kwamba wapi ushindi utaenda.
Timu zote zimepata muda mzuri wa kupumzika na Arsenal ikiwa Baku tangu Jumamosi huku Chelsea ikiwasili siku ya jumatatu.
Chelsea tayari ipo kwenye champions league na inaipa nafasi zaidi Arsenal kucheza kwa ari ya kutaka kushinda kombe hili la Europa ambalo mara ya mwisho kulinyakua ilikuwa ni mwaka 1994.
NB: Tafsiri fupi na Mchoro ni kwa hisani ya gazeti la Telegraph.