Arsenal (The Gunners) | Special Thread

good move to cement the defense after Gallas and Senderos departure
 
Yeah hes only 31 and French!

Mkuu, heshima mbele.

Huyu Sebastiene ana umri wa miaka 30 na moja ya masharti ambayo amewapa Arsenal mpaka wameamua kumsajili ni kwamba anataka mkataba wa miaka 3 kwahio itamchukua hadi akiwa na miaka 33 ambao ni umri wa William Gallas ambae amekubali paycut kwa Spurs.

Ukiangalia wachezaji wote waloondoka Arsenal hivi karibuni wana mushkheri ukianzia na Adebayo ambae hakuanza mechi na Spurs, Vieira ambae mpaka sasa pumzi inakuwa hafifu, Henry anajitahidi sana, Sol Campbel ndio kabisa akifungwa tera hawezi ku-recover defencevely na Robert Pires huingia kipindi cha pili kila mechi ya Villa-Real, mzee Wenger anafanya biashara na Arsenal finacially kwa sasa mambo si mabaya.

Ukumbuke Wenger ana masters degree tu, ya Economics na anaifanyia kazi pale Emirates. Sisi wapenzi wa Arsenal (maana hakuna wanachama) tunaamini mwaka huu lazima tuchukue walau kombe la CL.

Lol
 
Longo longo mingi! Kama mpenda soka umeandika cha maana hapo mwisho.....una maana champions League ama Carling cup?
 
Longo longo mingi! Kama mpenda soka umeandika cha maana hapo mwisho.....una maana champions League ama Carling cup?

...ahaa haha!, ...ewe bana we ni mshari sana siku hizi.
Hivi umekuwaje lakini?
 
...ahaa haha!, ...ewe bana we ni mshari sana siku hizi.
Hivi umekuwaje lakini?

Hapana mkuu! Jamaa anasifia MA in Econimics kwa kocha lol! Kocha ni vikombe tu si longo longo. Tafuteni GoliKipa sana good cover huko nyuma
 
Longo longo mingi! Kama mpenda soka umeandika cha maana hapo mwisho.....una maana champions League ama Carling cup?

Lol,

Namaanisha Champions League. Yote si kujaribu mkuu?

Unajua nikwambie kitu kimoja Chelsea ina bahati sana kwamba mmeamua kutumia resources mlizo nazo. Lakini kuna tofauti kubwa sana na Arsenal na Chelsea.
 
Tofauti ni kubwa sana! Mwaka jana mumechangia goli 5 na points kama sita.....thank you guys! Hope mwaka huu mtafanya hiyo favor
 
Tofauti ni kubwa sana! Mwaka jana mumechangia goli 5 na points kama sita.....thank you guys! Hope mwaka huu mtafanya hiyo favor

Katika mechi yoyote ya mpira kwa sasa ni kwamba kama moja ya timu inamiliki mpira kwa kiasi kikubwa na ikashindwa kutumia "advantage" hiyo kufunga magoli basi inaweza kuadhibiwa kirahisi.

Ukiangalia mechi ya Chelsea na Wigan, Wigan walitawala mwanzoni na kutishia Chelsea lakini ilipogota dakika ya 34 Malouda akafunga tena kirahisi sana.
 
Unaongea kama vile unasema sizitaki mbichi hizi, typical Arsenal fan. Hao wachezaji wote uliowataja pamoja na wengine mliowaondoa kwamba ni "wazee" ni proven winners na wangekuwepo mngekuwa mmepata angalau Carling Cup au FA. Anyway, it's good to see you become a feeder club.
 
Mimi ni typical Arsenal fan mkuu, ninaamini katika "philosopy" ya kukuza vipaji na kuviendeleza na always money don't buy a success huo ndio msimamo wa sisi Arsenal fans.

Tunajua Arsene Wenger anafanya nini na wapi club hii inaelekea. Arsene Wenger ana uwezo (ability) ya kutumia kiasi kidogo cha fwedha alichonacho kuiendesha timu na timu zingine "soon" zitafuata hii "approach" kwani wachezaji na ma-agents huko tuendako wanataka kutawala hii biashara ya usajili ambapo wanaweza kutamka kiasi chochote wanachotaka na hasa wale wachezaji wa Uingereza.

Arsenal wameweza kujenga uwanja mpya wenye viti 60,000 ambao kila mechi wanaleta paundi millioni 3, na hio ni mbali ya mauzo ya jezi na vitu vingine vidogo vidogo "merchandise". Uwanja wa ule wa zamani pale Highbury umetoa apartments karibu 2000 ambazo zote zimeishauzwa.

Club ya Arsenal sasa ina nafasi nzuri sana financially kuliko waasimu wake Man United, Chelsea ambapo mzee Roman amesema hatoi pesa zaidi msimu huu na wachezji waliopo wanatosha na labda kama ni kununua wawe wale wenye umuhimu sana kama Ramires.

Kama umeona hata Man United na Chelsea wote msimu huu wamesita kidogo kufanya manunuzi makubwa ya wachezaji kwani wanaona hii approach ya Wenger.

Lakini pamoja na hayo tunaamini msimu huu tuna timu ya kufanya kisichotarajiwa.
 
Just for the record mkuu, uwanja wa zamani ni Highbury....., Ashburton Grove ndio Emirates mnakocheza sasa.
 
Just for the record mkuu, uwanja wa zamani ni Highbury....., Ashburton Grove ndio Emirates mnakocheza sasa.

Asante sana mkuu! Huwa sielewi kwanini watu wengine hupenda kuandika vitu wasivyo vijua makusudi kabisa? Ona huyo jamaa alivyokuwa analisha wenzake sumu? typical Fat Arse -Anal fans.
 
Rev Masanilo maneno yako ni mazito mno. Huwezi kutumia kosa dogo ku-label mtu mkuu. Tujaribu kuwa waungwana.
 
Rev Masanilo maneno yako ni mazito mno. Huwezi kutumia kosa dogo ku-label mtu mkuu. Tujaribu kuwa waungwana.

Kiongozi no offense hapo!

Haya mkuu umeishajua kutoka kwa Mzee Peasant, fikiria kwa mtu aliyekuwa hajui kabisa! hahahahahahah pole watani. Mechi ijayo mwacheza na nani?
 
Tarehe 28 tunakwenda Blackburn halafu 11 September tupo home tutacheza na Bolton halafu tarehe 18 tunakwenda Sunderland.

Mechi hizo zote ni ngumu lakini tunaweza kupata point zote tisa hata kwa goli moja tu.
 
Mechi rahisi hizo sema nyie mnakuwa na mchecheto mkikutana na Manchester citeh ama Utd walau mtapata hata 7, si unajua sisi bado tuna 100% records so far ....twa cheza na Stoke then Westham hahahah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…