Habari za Usajili.
Aaron Ramsey anazungumza na timu tano za nje ya Uingereza.
View attachment 982566
Aaron Ramsey yupo huru kuzungumza na timu yoyote itakayota kumsajili kuanzia tarehe 1 mwezi huu wa January.
Mchezaji huyo wa kiungo wa Arsenal na timu ya taifa ya Wales anaruhusiwa kusaini mkataba mpya au kukubalia mkataba mpya kuanzia leo hii kabla ya mkataba wake naArsenal ahujamalizika mwezi Julai mwaka huu.
Ramsey yupo huru kuzungumza na timu za Bayern Munich, Inter Milan, Juventus, Paris St-Germain na Real Madrid.
Arsenal walimwekezea mezani Ramsey mapendekezo ya mkataba mpya wa miaka minne mwezi September mwaka jana, lakini badae wakaancha nao kutokana na sabau za kifedha na kimpira.
Kocha wa Arsenal Unai Emery alitaka amtumie Ramsey katika uundaji wa timu mpya lakini hali hiyo imekuwa ngumu kwa Ramsey kutoweza kufuata mpango huo mpya wa Emery na pia Arsenal kutopenda kugharamia mikataba yenye gharama kubwa kwa wachezaji ambao ufanisi wao uwanjani hauridhishi,.
Ikakumbukwa kuwa wakti wa usaili kocha Emery alikuja na taarifa za kila mchezaji wa Arsenal taarifa ambayo ilijaa vigezo vyite ambavyo wachezaji wanatakiwa kufuata.
Hadi sasa wachezaji Mesut Ozil na Aaron Ramsey viwango vyao vya uchezaji na ufanisi bado havijaweza kumashawishi kocha Emery kuendela kuwatumia uwanjani.
Juventus ya Italia imempa offer Ramsey ya mkataba wa miaka minne wenye mshahara wa wastani wa pauni milioni 5.8 kwa mwaka, ambapo kama akicheza nusu ya mechi zote basi atapewa mshahara wa pauni milioni 6.3.
Endapo atacheza asilimia 70 ya mechi za timu hiyo na kuweza kuwa mmja wa wachezaji waandamizi Ramsey atalipwa mshahara wa pauni milioni 7 kwa mwaka sawa na pauni 138,000 kwa wiki.
Ramsey tayari amezungumza na PSG ambao wanataka kubadilishana na Arsenal mchezaji wa kiungo Adrien Rabiot lakini Ramsey anapendelea kwenda timu ya Juventus.