Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal wakamilisha usajili wa Sokratis Papastathopoulos kutoka Borussia Dortmund.

kama ilivyokuwa ikitarajiwa Arsenal jana walikamilisha usajili wa mchezaji huyo ambae amesaini mkataba wa miaka mitatu.




Sokratis anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na Arsenal baada ya beki mwingine
Stephan Lichsteiner na kipa Bernd Leno.



Sokratis anaungana na beki Calum Chambers ambae wiki ilopita alisaini mkataba wa muda mrefu na wataziba nafasi za Per Mertesacker aliestaafu na Laurent Koscielny ambae ni majeruhi na anatarajiwa kurudi uwanjani mwakani.

Per Mertesacker anakuwa meneja wa kitalu au shule ya vijana kwa jina la Arsenal Academy.
 
Usajili Updates: Arsenal kukamilisha usajili wa kiungo Lucas Torreira hivi karibuni.


Lucas Torreira.

Arsenal hivi karibuni wanatarajiwa kukamilisha usajili wa mchezaji kiungo mkabaji Lucas Torreira baada ya fainali za kombe la Dunia kufikia tamati.

Mchezaji huyo wa kiungo wa Samprodia ya Italy anatarajiwa kusaini mkataba utaogharimu kiasi cha pauni milioni 26.

Kwa sasa Torreira anajiandaa pamoja na timu yake ya taifa ya Uruguay kucheza na Ufaransa siku ya Ijumaa kwenye hatua ya robo fainali za kombe la dunia.
 
Arsenal wafanya mazoezi mafupimafupi


Unai Emery akiwa uwanjani London Colney tayari kuanza mpango wake wa mazoezi.

Emery amemleta kocha wa magolikipa aitwae Javi Garcia ambae pichani anazungumza na kipa namba moja wa Arsenal Petr Cech.


Emery akiwa na kocha msaidizi Steve Bould ambe amebakizwa baada ya kuondolewa jopo la wasaidizi wa Arsene Wenger.

Beki mshahara mpya Sokratis Papastathopolous akiwa mazoezini.
 
Huyu lazima tumpate---
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…