Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Sawa, pia waweza linganisha upande wa timu zipi angalau mara kadhaa zinafika mbali.
Kama ni ligi kutokuwa na mwenyewe ndio ubora, hata ligi ya Kenya haina mwenyewe.
Ligi ya EPL sikatai, ndio yenye MSISIMKO mkubwa.
Ina msisimko na pia ina ushindani wa wao kwa wao. Swala la ubora ni subjective kidogo.
 
but mbona hizi timu zikikutana na timu za nje eg SEVILLA,MONACO, hali inakuwa tete????????
Ndio maana nikasita kuweka ubora kwenye hoja, lakini kama ukiangalia vizuri, timu za Uingereza zinapata tabu kwa timu za Uhispania na Ujerumani. Ila wakikutana na Italia inakuwa rahisi zaidi.
 
Talent peke yake haitoshi kukupa vikombe, pesa peke yake haitoshi kukupa vikombe. Its the combination of both. Manu wamekusanya kikosi ghali zaidi lakini wameshindwa kuchukua hata kombe moja sawa na Arsenal ambayo ina average players.
asenali ina average players!!!! hujui maana ya hilo neno naona..
 

Hivi Nani Mshabiki Maandazi Hapa Kama Sio Wewe?

Yana Hata Msimu unaofuata Wa 2018/19 Haujafika Basi Dunia Nzima Tumeshajua Kama Bingwa Ni Bayern Halafu Unajadili Ubora?

Bingwa Asiye na Mpinzani Wewe Unaita Anacheza Ligi Bora?
Mkuu Ubora Kwanza Unaanzia Kwenye Ushindani!!

You Can't be serious bro!
 
Huu usajili wa griezman naomba ufanikiwe haraka kwenda barca maana jamaa wakimpata tu basi wanamtoa dembele kwa mkopo so tukifanikiwa kumpata ousmane kwa msimu ujao aaaaah tutakuwa vizuri sana.......

waliopo ktk rada zetu ni makipa sergio ricco wa sevilla,bernad leno wa liverkusen,mabeki lichtsteiner wa juve,alex vidal,soyuncu,socratis wa bvb,john evance, viungo ni steven N'zonzi,jean seri wa nice,pellegrin wa roma,
 
Inakuwaje wewe kama uko ligi yenye upinzani, ukicheza na hao maboya wanakupeleka puta?? Iko hivi, EPL ina upinzani kwa timu zake zenyewe kwa zenyewe ila inapokuja wao kushindana na wa ligi nyingine wao ni maboya tu.

Alafu usochanganye haya maneno, yana tofauti kubwa sana. UBORA na MSISIMKO.
 
Kwa bajeti ipi mkuu wachezaji hawa?? Au tunachukua kwa mikopo??
 
mkuu lakini mbona la riga tunajua kuwa mapapa ni wawili tu ambao bila ya kuwataja nadhani kila mtu anawajua na ligi yao ni bora?sasa hii ina tofauti gani na seria a na bundasliga ambapo mambo ni hayohayo,kwa upande wangu mi naona epl ndio ipo kipekee maana unaweza kuta WOLVESAMPTON au CARDIFF CITY wanapanda daraja then wanachukua kombe
 
huyo Lichtsteiner naona deal linaelekea kuwa done
 
Kwa bajeti ipi mkuu wachezaji hawa?? Au tunachukua kwa mikopo??
yap OUSMANE anatolewa kwa mkopo baada ya kuonekana kuwa kiwango chake kimesuasua toka aanze kuitumikia barca na taarifa zaidi zinadokeza kuwa jamaa amekuwa ana utovu wa nidhamu kwani anapenda sana starehe kupindukia na hii imepelekea kiwango kushuka na kukosa nafasi ktk kikosi cha kwanza licha ya usajili wake kuwa ghali sana......Hivyo barca kama wanataka kumpa talaka rejea ili aende akajirekebishe ili kama akishindwa kubadilika na kurejea ktk kiwango chake basi atapigwa bei...lakini hili litafanyika iwapo tu mipango yao ya kumsajili ANTONIO GRIZMAN itakamilika
 
wekeni vigezo vya ubora wa ligi tupime hapahapa ubishi uishe
 
wekeni vigezo vya ubora wa ligi tupime hapahapa ubishi uishe
 
wekeni vigezo vya ubora wa ligi tupime hapahapa ubishi uishe
 
Arsenal atatufaa kama hana nidhamu??
 
huyo Lichtsteiner naona deal linaelekea kuwa done
yah jamaa anatakiwa aje kumsaidia bwana mdogo pale ubavu wa kulia maana dogo ametuka sana msimu uliopita na hali hii ilimpelekea kuchoka mpaka muda mwingine kuonekana anacheza chini ya kiwango so hii itakuwa backup nzuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…