MSHAMBULIAJI wa Ujerumani, Mesut Ozil amemweka pabaya Andres Iniesta baada ya kumfanyia mambo makubwa kwenye mechi yao ya kirafiki.
Mshambuliaji huyo wa Arsenal, alifanya mambo makubwa na adimu na kutoa asisti katika mchezo uliopigwa huko Dusseldorf, Ujerumani na kumalizika kwa sare ya 1-1.
Ozil alikuwa akipokea mipira kwenye chaki akiwepo mchezaji huyo wa Hispania, inaonekana kwamba hawezi kumtoka, lakini alikuwa akimtoka hapo hapo.
Alikuwa akitoa mapende kwa miguu yote huku akimwacha Iniesta akiwa anahaha uwanjani.
Kwa upande wa Iniesta,naye alikuwa akifanya vitu vyake kwani alisaidia kutoa pasi kwa Rodrigo ambaye alifunga bao la mapema kabisa, dakika ya sita.
Ozil, amerejea kwenye klabu yake ya Arsenal baada ya kuondolewa kwenye mechi ijayo na Brazil. Mshambuliaji huyo wa zamani wa Real Madrid atakuwa na kikosi cha Gunners Aprili Mosi dhidi ya Stoke City huko Emirates.