Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Tetesi
Borussia Dortmund inamtaka mshambuliaji raia wa Ufaransa wa timu ya Arsenal Olivier Giroud, mwenye umri wa miaka 31, kama sehemu ya kubadilishana na mchezaji raia wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, mwenye umri wa 28, - au wasitishe mpango huo hadi msimu wa joto. (Mirror)
 

Mpaka hapo deal imekufa kifo cha mende.
 
Thierry Henry kwa sasa amepachikwa majina mengi ya kejeli na mashabiki wa Arsenal kutokana na madai ya kumshawishi Alexis Sanchez kujiunga na Manchester United.

Wengine wamekuwa wakimuita nyoka msaliti na mengine mengi. Kocha huyo msaidizi wa timu ya taifa ya Ubelgiji na mchezaji wa zamani wa Arsenal amekana kuwa hakuwahi kumshauri Sanchez kufanya maamuzi hayo.

Henry ametoa taarifa hiyo kupitia mtandao wake wa Twitter, ameandika, “Ninajua sihitaji kuelezea hili kwa mashabiki wengi wa Arsenal lakini kinyume na uvumi hakuna muda wowote nilimwambia Alexis Sanchez aondoke Arsenal. Sikujua kwamba angeenda kusajiliwa na Man Utd mpaka nilipoona kwenye habari kama wengine.”

Baada ya kukamilisha usajili wa kujiunga na Man United, Alexis Sanchez alithibitisha kwa kuandika ujumbe kuwa alipokea ushauri wa kuondoka Arsenal na kujiunga na Manchester kutoka kwa Henry.

“Nakumbuka leo, mazungumzo niliyokuwa nayo na Henry, mchezaji wa kihistoria wa Arsenal, ambaye alibadilisha klabu kwa sababu hiyo hiyo na leo ni wakati wangu,” aliandika Sanchez.
 
Najaribu kuwaza ni yupi atakuwa mbadala wa Alexis Sanchez pale ghala la kuhifadhia silaha nakosa majibu.
Ndo kusema arsenal inaenda kupotea Kwenye ulingo wa michezo!!!!!

Karbuni wadau Kwenye uzi huu
 
Yaani arsenal ipotee kwa kuondokewa na sanchez? Tafakari upya
 
Huyu jamaa bure kabisa, Sanchez??? Arsenal wamepita weng kuliko Sanchez na waliondoka na arsenal bado ipo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…