Alichosema Tony Adams kuhusu Gunners....
Nahodha wa zamani wa kikosi cha Arsenal Tony Adams amesema kwamba kikosi cha sasa cha Arsenal hakina uwezo wa kutwaa taji la EPL na anaona utawala wa Wenger kuisha kwa machozi.
Kocha wa Arsenal ameongeza muda wa kuitumikia klabu hiyo kwa kufikia miaka 21 yani miaka miwili zaidi kwa kusaini mkataba mpya.
Hata hivyo Adams ambaye aliiongoza Gunners kutwaa mataji manne ya EPL amesema kwamba "alisali" ili Wenger asiongeze mkataba baada ya kutwaa taji la FA dhidi ya Chelsea na amekiri kwamba kama hakutokuwa na maboresho ya wachezaji wa kiwango cha hali ya Dunia basi anaona mafanikio aliyowahi kuyapata Wenger hapo karibuni yatapakazwa matope.
"Naamini hiki kikosi hakiwezi kutwaa ubingwa katika miaka miwili ijayo . Na huenda heshima yake ikaharibika kwa muda mfupi sana na nafikiri hiyo itakuwa hudhuni kubwa sana hasa ukizingatia makubwa aliyofanya klabuni ."