Arsenal (The Gunners) | Special Thread

kuna kipindi nilisikia ataongelea hatma yake mwezi march au april ilikuaje tena?
any way in wenger we trust
 
GRANIT XHAKA NJE
ARSENAL Vs MANCHESTER UNITED

Katika mkutano na waandishi, Wenger alibainisha kuwa Lucas Perez hatacheza kwenye kikosi chake kadhalika Xhaka hatacheza dhidi ya Man United

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amebainisha kuwa kiungo wake Granit Xhaka hatacheza dhidi ya Manchester United wikiendi ijayo.

Licha ya maoni mbalimbali tangu alipotua Emirates akitokea Borussia Monchengladbach msimu uliopita majira ya joto, Xhaka ameanza mechi 33 katika michauno yote msimu huu lakini ataukosa mchezo utakaopigwa kunako dimba la Emirates Jumapili.

Katika mechi waliyofungwa 2-0 na Tottenham Hotspur, Mswisi huyo alikwatuliwa kwenye kifundo cha mguu na ingawa aliendelea hadi dakika ya 65, ameshindwa kufanya mazoezi wiki hii.

Kulingana na maelezo yake kwenye mkutano na waandishi wa habari, Wenger alibainisha kuwa Lucas Perez hatacheza kwenye kikosi chake licha ya kufanya mazoezi siku kadhaa zilizopita, lakini kulikuwa na habari njema kuhusu Shkodran Mustafi.

Beki huyo wa kati amekosekana tangu Aprili 10, lakini Wenger amedokeza kuwa anaweza kucheza sasa baada ya kufanya mazoezi ya kawaida.
 
Ahsante sana Mkuu. Haya mambo ukimwambia mtu ambaye haelewi mambo ya upenzi wa michezo anakushangaa sana. Utasikia, "Sasa si uhamie Chelsea tu, kila siku timu yenyewe inafungwa fungwa tu lakini bado unaishabikia" lol! hahahahahahaha

Nimekuelewa najua machungu unayopitia ushabiki na upenzi kwa hali kama hii unakuwa katika madhila makubwa pole sana BAK
 
ARSENE WENGER AMEENDELEA KUGOMEA MASWALI KUHUSU MUSTAKABALI WAKE DHIDI YA ARSENAL

Ametania wanahabari kwamba mwenyewe alifanya makosa alipoahidi kwamba atakuwa amefanya uamuzi wake kuhusu mkataba mpya kufikia sasa.

Wenger mwenye umri wa miaka 67 amekuwa mkufunzi mkuu wa Gunners tangu 1995 na mkataba wake wa sasa unafikia kikomo mwishoni mwa msimu huu.

Mwezi Februari alitangaza kwamba angeamua kuhusu mkataba mpya ifikapo mwenzi machi au Aprili cha kushangaza mpaka sasa ni mwezi mei na bado ameendelea kukaa kimya mpaka wanahabari walipo muuliza kuhusu uwamuzi wake dhidi ya mkataba mpya
Akizungumza kabla ya mechi ya Jumapili dhidi ya Manchester United,Mfaransa huyo alitania "Hii ina maana kwamba nilikosea na amekataa kuzungumzia hii habari tena kuhusu mkataba mpya"

kwa kipind cha hivi karibuni baadhi ya mashabiki wamekuwa wakiandamana na mabango (WENGER OUT) kumpinga arsene wenger aliedumu na arsenal kwa mda mrefu
mashabiki wa arsenal ambao wamekuwa wakiandana wamekuwa wakibeba mabango yenye ujumbe ambao unaashiri kumchoka meneja huyo [HASHTAG]#wengerout[/HASHTAG] [HASHTAG]#wexit[/HASHTAG] [HASHTAG]#timeforchanges[/HASHTAG]
 
Ahsante sana Mkuu. Haya mambo ukimwambia mtu ambaye haelewi mambo ya upenzi wa michezo anakushangaa sana. Utasikia, "Sasa si uhamie Chelsea tu, kila siku timu yenyewe inafungwa fungwa tu lakini bado unaishabikia" lol! hahahahahahaha
Yaah mahaba ni kitu kilicho jificha hakionekani utashangaa unakuta timu zinacheza huzijui but pana moja automatically unajikuta umeipenda nakuelewa sana BAK
 
Reactions: BAK
MATUMAINI YA ARSENAL KWA ALEXANDRE LACAZETTE YAANZA KUOTA MBAWA
Straika anayeripotiwa kuwindwa na Arsenal Alexandre Lacazette anataka kujiunga na Atletico Madrid, majira ya kiang azi kwa mujibu wa taarifa kutoka, L’Equipe.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa ambaye ameitumikia Lyon kwa takribani maisha yake yote ya soka mpaka sasa anafikiria kuihama klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu na vilabu vingi vinahitaji saini yake vikiwemo Atletico, Arsenal, West Ham na Paris Saint-Germain.

Hata hivyo Gunners wanatarajia kumkosa straika huyo baada ya kuchagua kuhamia Atletico Madrid. kwa mujibu wa jarida la nchini Ufaransa la L'Equipe.

Atletico walijaribu kumsajili mshambuliaji huyo majira ya kiangazi yaliyopita lakini Rais wa Lyon Jean-Michel Aulas alizuia uhamisho huo.

Lyon wanatarajia kupokea kiasi cha Euro Milioni 60 pindi watakapomuuza Lacazette majira haya ya kiangazi.

Hata hivyo Arsenal nao wamefanya mawasiliano na wakala wa Lacazette kuhusu nia yao ya kutaka kupata saini yake.
 
Jaman arsenal leo nawaombea ushindi ...tuko pamoja leo wadau ...msizingue! OOhooo
 
#MECHI_YA_LEO

ARSENAL vs MANCHESTER UNITED

UWANJA: Emirates stadium

MUDA: 6:00 Pm EAT (12 Jion)
 
HT
Arsenal 0-0 Utd
Duh worse display ever,honestly we dont deserve UCL spot this time maana timu imekufa matokeo yoyote ni kawaida kabisa hata Manure nao wako hoi
 
Man U walianza kipindi cha pili kwa kupaki basi.
Wanaiogopa nafasi ya 6 hahahaaaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…