Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

nakweli hata kwenye jamii usipo hudhuria misiba ni ishu mbaya sana
kulikoni hata harusi
Jamii yetu hii bora ukache kuhudhuria sherehe,musiba usipofika utaanza kuitwa mchawi.

Sasa hawa wenzetu hatuna ubaya nao hebu Ngoja tuendelee kuhani.

Lete karata za titanic tuendelee kuwafariji...najua kesho asbuhi kutandua musiba tutakunywa uji wa mchele hapa.
 
ngoja nikachukue pilipili nyumbani kwa ajili ya chakula cha msibani
 
sister unajua mimi nilivyo Gunners damu damu. Nimechoshwa na matokeo ambayo si kuyaridhisha miaka nenda miaka rudi kama sikosei tangu 1996. Nimeamua kusitisha upenzi wangu mkubwa kwa muda mpaka hapo Babu atapopewa red card na owners au yeye new kuamua kufungasha virago vyake. Hata game ya jana sikuwa na mchecheto wa kuiangalia hata kwa sekunde moja. It is very sad for Arsenal fans all over the World.

wenyeji hata hawapo, BAK
 
aiseee pole sana, asa sasa hivi wapi unapata faraja ya mpira???? hakuna katimu ambako kamekuwa substitute ya Arsenal.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Poleni wakuu niliwaombea ushindi ila ndo hivo hamkushinda. Mmepambna lakini haikuwa bahati yenu ...bado arsenal ni timu nzuri sana, Wenger anastahili kuifundisha.
 
Hahahahaha lol! Mchepuko siyo lol! Bado zile mechi za haja huwa sizikosi na kuna wakati zinakuwa nyingi hata nashindwa kuamua niangalie ipi hivyo hubaki kwenye ile ambayo naona ina ushindani mkubwa na kuchungulia kidogo kwenye zile nyingine. Labda mchepuko naweza kusema ni RMA kwenye la liga na UEFA.

aiseee pole sana, asa sasa hivi wapi unapata faraja ya mpira???? hakuna katimu ambako kamekuwa substitute ya Arsenal.
 
Hahahahaha lol! Mchepuko siyo lol! Bado zile mechi za haja huwa sizikosi na kuna wakati zinakuwa nyingi hata nashindwa kuamua niangalie ipi hivyo hubaki kwenye ile ambayo naona ina ushindani mkubwa na kuchungulia kidogo kwenye zile nyingine. Labda mchepuko naweza kusema ni RMA kwenye la liga na UEFA.
hapo sawa, si mbaya sana kuwa na substitute kupunguza makali ya uchungu.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
KIUNGO wa Malaga na timu ya taifa ya hispain U 21,Pablo Fornals amesitisha kwa muda mpango wa kujiunga na Valencia baada ya kupata taarifa kuwa Arsenal inataka kumsajili ili akawe mbadala wa muda mrefu wa kiungo wake majeruhi,Santi Cazorla.

Hivi karibuni Fornals mwenye umri wa miaka 21 aliripotiwa kuwa kwenye mazungumzo na Valencia ambao ni wapinzani wakubwa wa Malaga lakini taarifa kutoka nchini Hispania zinasema kiungo huyo amesitisha kwa muda mazungumzo hayo ili kuona kama Arsenal itapeleka ofa kwa ajili yake.

Kocha wa Arsenal Mfaransa,Arsene Wenger ameripotiwa kuanza mapema kumsaka mbadala wa Cazorla na anamuona Fornals mwenye mabao sita msimu huu kama mtu sahihi wa kukiongezea nguvu kikosi chake.

Kwa mujibu wa habari kutoka gazeti la michezo la Plaza Deportiva habari zinasema Arsenal inaweza kumpata Fornals kwa dau dogo la Pauni 10 Milioni.

Ikiwa Arsenal itafanikiwa kumsajili Fornals itakuwa imefikisha wachezaji watatu waliowahi kuchezea Malaga.Wengine ni Santi Cazorla na Nacho Monreal.
bc3d41cfdada55c96d7b9bb49b3d88b4.jpg
 
Hahahahaha lol! Mchepuko siyo lol! Bado zile mechi za haja huwa sizikosi na kuna wakati zinakuwa nyingi hata nashindwa kuamua niangalie ipi hivyo hubaki kwenye ile ambayo naona ina ushindani mkubwa na kuchungulia kidogo kwenye zile nyingine. Labda mchepuko naweza kusema ni RMA kwenye la liga na UEFA.
Nimekuelewa najua machungu unayopitia ushabiki na upenzi kwa hali kama hii unakuwa katika madhila makubwa pole sana BAK
 
  • Thanks
Reactions: BAK
ARSENE WENGER ASISITIZA KUTAKIWA ANG’OKE ARSENAL HAWEKI MOYONI!

_AJITETEA REAL MIAKA 5 , LIVERPOOL MIAKA 20 BADO KUWA BINGWA!_

MENEJA wa Arsenal Arsene Wenger amesisitiza kutakiwa aondoke haweki Moyoni na hata yeye binafsi hujichukia wakifungwa.

Wenger, mwenye Miaka 67, hajabainisha kama atasaini Mkataba Mpya mwishoni mwa Msimu huu baada ule wa sasa kumalizika akiwa ameitumikia Arsenal Miaka 20 lakini kipindi hiki anasakamwa mno na Mashabiki ang’oke baada ya Klabu hiyo kushuka nje ya 4 Bora ya EPL, Ligi Kuu England na kutupwa nje ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.

Tangu Wenger atue Arsenal Mwaka 1996 Timu hiyo imekuwa ikimaliza EPL ikiwa kwenye 4 Bora lakini Msimu huu sasa wapo Nafasi ya 6 wakiwa Pointi 6 nyuma ya Timu ya Nne Man City huku wakiwa wamebakisha Gemu 5.

Huku akisubiri Jumapili kumkaribisha Jose Mourinho na Man United yake hapo Jumapili huko Emirates kwenye Mechi ya EPL, Wenger amesisitiza kupondwa kwake hakuweki Moyoni.

Wenger amenena: “Mie niko kama Watu wote wengine, na napenda nipendwe lakini hilo naliacha. Kwa kweli najichukia mwenyewe kama Meneja kupita yeyote kama sishindi Gemu. Sipendi kufungwa!”

Arsenal hawajatwaa Ubingwa wa England tangu 2004 lakini wametwaa FA CUP mara 2 katika Misimu Mitatu iliyopita.

Lakini Wenger amenyoosha kidole kwa Wapinzani kuonyesha ni ngumu kutwaa Ubingwa.

Ameeleza: “Watu wanataka ushindi. Kama hutwai Ubingwa, FA CUP, CHAMPIONZ LIGI, ni maafa. Lakini sie tumebeba FA CUP mara 2 katika Miaka Mitatu na kumaliza Ligi Nafasi za 2, 3 na 4. Safari hii tupo tena Fainali ya FA CUP. Kwa ujumla hatufurahii kwani tunataka tushinde kila kitu!”

Ameongeza: “Lazima ukubali kwamba hata Real Madrid hawajatwaa Ubingwa kwa Miaka Mitano sasa. Ni Klabu kubwa ni ngumu. Liverpool hawajakuwa Bingwa Miaka 20!
813c90dbe0623aa1398e6bfbdae60a7d.jpg

[/U]
 
Back
Top Bottom