Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Tumeshatinga kwenye nafasi ya nne kwa uzembe tu, kama hatukuwa makini tunaweza kabisa kuendelea kushuka na kujikuta kwenye nafasi ya sita au ya saba. 🙁🙁🙁 Wameshaharibu siku hawa.
Poleeee..... nishakwambia hama hutaki.... njoo nikufariji wangu.
 
Reactions: BAK
Hata wachezaji wanapoteza confidence waliyokuwa nayo hivyo kuanza kufanya vibaya katika mechi ambazo tunastahili kushinda. Timu nyingine ikipata goli ari inaongezeka ya kutafuta goli linguine zaidi ili kuwademoralize wapinzani, siye tukajiona tumeshashinda na kuamua kulinda kagoli kamoja.

Sasa hivi mtakuwa mnashinda mechi kwa manati. Mwisho wa msimu mtaanza kugombania muingie top 4.
 
LOL! tuna timu nzuri sana ila tatizo ni strategy yetu mbovu ya kutaka kulinga kagoli kamoja huku zikiwa zimebaki dakika chungu nzima. Saa nyinine huwa namuonea huruma Sanchez jinsi anavyojituma uwanjani halafu matokeo yenyewe ni kupigwa bao.
Kwa kweli mna timu nzuri ila mna magonjwa yenu yale yale ya kila siku.
 
Magonjwa yanayosababishwa na kocha ambaye mikakati yake imepitwa na wakati. Yaani nilikuwa nashangaa mno kuwaona wameamua wote kurudi nyuma kucheza kama vile zimebaki dakika mbili au tatu mpira kwisha.

Kwa kweli mna timu nzuri ila mna magonjwa yenu yale yale ya kila siku.
 
Unategemea ushindi kweli
 

Attachments

  • Screenshot_2016-12-18-21-19-15.png
    11.3 KB · Views: 33
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…