Arsenal (The Gunners) | Special Thread



GOAL!


Alexis Sancheeeeeeeez Arsenal 1-0 up

Goli limefungwa dakika ya 12

Kazi ya Ozila hiyo ambae alimpsia Alex Oxlade Chamberlain.

Ni ushirikano wa wachezaji hawa watatu nyota ambapo Sanchez anakimbia kuelekea kulia akimuashiria Chamberlain amwekee chapati kwenye sahani na bila ajizi anauweka mpira kimiani upande wa kushoto mwa kipa Stoyanov.
 

Dyakov akijaribu kuwatoka Santi Cazorla na Francis Coquelin.

Dakika inakwenda ya 24 na Arsenal wanatawala huu mchezo na wanapaswa kuongeza magoli zaidi.
 
hawa jamaa (Bulgarians) ni wazuri. Tukiwachukulia rahisi rahisi watatuondoa...
 
Dakika inakwenda ya 36 na goli bado ni kwa Arsenal 1 Ludogorets 0

Mesut Ozil amepwaya sana leo hajachangamka.

Sancez, Walcott na Chamberlain ndiyo wanashughulika.
 
GOAL!



Walcoooot dakika ya 42

Theo Walcott anafunga goli safi kabisa baada ya kupokea pasi murua kutoka kwa beki wa kushoto Kieran Gibbs.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…