Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Kipindi cha pili kinaanza, hakuna timu iliyofanya mabadiliko.

Arsenal: Ospina, Bellerin, Mustafi, Koscielny, Monreal, Xhaka, Cazorla, Walcott, Ozil, Iwobi, na mbele ni Alexis Sanchez.

Basel : Vaclik, Lang, Suchy, T Xhaka, Balanta, Traore, Bjarnason, Zuffi, Fransson, Doumbia, na Steffen
 
I don't care wengine mnavyosema kwa maoni yangu Xhaka bado hajani convince kama Coquelin
 
Tutajutia hizi nafasi tunazozikosa. Inatakiwa tuwapige magoli mengi.
 
Dakika ya 60 inakwenda na Arsenal wanaongoza kwa goli 2 -0

Kuna dalili ya goli la tatu, tusubiri.
 
WTF, Sanchez amekosa magoli kama 5 sasa.. Ingekuwa Giroud mngekuwa mshakemea mapepo
 
Naona kama vile Arsenal wanacheza vizuri dakika 45-60 za mwanzo baada ya hapo wanakuwa kama wamechoka.... Come on Arsenal!!!!
 
Arsenal wamefanya mabadiliko na Mohamed Elneny na Alex Oxlade Chamberlain wanaingia badala ya Alex Iwobi na Theo Walcott.
 
Kieran Gibbs anatoka na anaingia Nacho Monreal

Dakika inakwenda ya 76

326adc2c-85cc-481c-9b87-5564de97aec0.jpg

David Ospina yupo imara.

3518bbe7-3694-447d-8c53-d760fa252418.jpg

Alexis Sanchez amekosa goli la wazi kabisa.

Kwa ujumla Mohamed Elneny ameleta uimara sehemu ya kati na Arsenal wanaonekana watamaliza kwa ushindi.
 
yani tulikuwa na tatizo la foward..tukamsajili huyo foward amabaye ni lucas perez lakini cha ajabu anawekwa bench hata kama anaingizwa sub anapewa dk 3..wenger anaboa mda mwingine
 
Hivi Ox atalalamika kwa nini anasota benchi? Mtu una nafasi kubwa ya kutoa pasi afu una dema dema... 2 points is better than 1 point
 
That's it Arsenal 2 Basel 0

Game over next tunakwenda Burnley
 
Back
Top Bottom